Njoo, Unifuate
Kufundisha Watoto Wadogo


“Kufundisha Watoto Wadogo,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2019 (2019)

“Kufundisha Watoto Wadogo,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2019

Kufundisha Watoto Wadogo

Kama una watoto wadogo katika familia yako, hizi ni baadhi ya shughuli zinazoweza kuwasaidia kujifunza:

  • Sikiliza au igiza hadithi. Watoto wadogo wanapenda hadithi—kutoka kwenye maandiko, kutoka kwenye maisha yako, kutoka kwenye historia ya Kanisa, au kutoka kwenye magazeti ya Kanisa. Tafuta njia za kuwashirikisha kwenye usimuliaji wa hadithi. Wanaweza kushikilia picha au vitu, kuchora picha ya kile wanachosikia, kuigiza hadithi, au hata kusaidia kusimulia hadithi. Wasaidie watoto wako kutambua kweli za injili katika hadithi unazowasimulia.

  • Soma maandiko. Watoto wadogo wanaweza kushindwa kusoma sana, lakini bado unaweza kuwahusisha katika kujifunza kutoka kwenye maandiko. Unaweza kuhitaji kuzingatia kwenye mstari mmoja, kifungu muhimu, au neno moja. Wanaweza hata kukariri vifungu vifupi kutoka kwenye maandiko kama watavirudia mara chache. Wanaposikia neno la Mungu, wataguswa na Roho.

  • Tazama picha au angalia video. Unapowaonyesha watoto wako picha au video inayohusiana na kanuni ya injili au hadithi ya maandiko, waulize maswali yanayowasaidia kujifunza kutoka kwenye kile wanakichoona. Kwa mfano, unaweza kuuliza, “Je, ni nini kinatokea katika picha au video hii? Kinakufanya ujisikie vipi?” Gospel Library app, Biblevideos.lds.org, medialibrary.lds.org, na children.lds.org ni mahali pazuri pa kutafuta picha na video.

  • Imba. Nyimbo za Kanisa na nyimbo kutoka Kitabu cha Nyimbo za Watoto na ufundishe mafundisho kwa nguvu zaidi. Tumia kielezo cha mada nyuma ya Kitabu cha Nyimbo za Watoto kutafuta nyimbo zinazohusiana na kanuni za injili unazofundisha. Wasaidie watoto wako kuhusisha ujumbe wa nyimbo na maisha yao. Kwa mfano, unaweza kuuliza maswali kuhusu maneno au virai katika shairi. Kwa kuongezea kwenye kuimba, watoto wako wanaweza kuonyesha vitendo vinavyoendana na nyimbo au kusikiliza nyimbo zikiimbwa taratibu wakati wanafanya shughuli zingine.

  • Buni. Watoto wanaweza kujenga, kuchora, au kupaka rangi kitu kinachohusiana na hadithi au kanuni wanazojifunza.

  • Shiriki katika masomo ya vielezo. Somo rahisi la vielezo linaweza kuwasaidia watoto wako kuelewa kanuni ya injili ambayo ni ngumu kuelewa. Unapotumia masomo kwa vielezo, tafuta njia za kuwafanya watoto wako washiriki. Watajifunza zaidi kutoka kwenye matukio ya kuingiliana kuliko kwenye kuangalia tu onyesho likifanyika.

  • Kuigiza-nafasi. Watoto wanapoigiza-nafasi ya aina fulani watakayokutana nayo katika maisha halisi, wanaelewa vizuri zaidi jinsi kanuni ya injili inavyohusika kwenye maisha yao.

  • Rudia shughuli. Watoto wadogo wanaweza kuhitaji kusikia mawazo mara nyingi ili kuyaelewa. Usiogope kurudia hadithi au shughuli mara kwa mara. Kwa mfano, unaweza kusimulia hadithi ya maandiko mara nyingi katika njia tofauti—kusoma kutoka kwenye maandiko, kufanya muhtasari kwa maneno yako mwenyewe, kuonyesha video, kuwaacha watoto wako wakusaidie kusimulia hadithi, kuwaalika waigize hadithi, na kadhalika.

    wazazi wakiwafundisha watoto wadogo