Agano la Kale 2022
Machi 28–Aprili 3. Kutoka 7–13: “Ikumbukeni Siku Hii, Ambayo Mliondoka kutoka Misri”


“Machi 28–Aprili 3. Kutoka 7–13: ‘Ikumbukeni Siku Hii, Ambayo Mliondoka kutoka Misri,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2022 (2021)

“Machi 28–Aprili 3. Kutoka 7–13,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2022

Musa, Haruni, na Farao

Kielelezo cha Musa na Haruni katika baraza la Farao, na Robert T. Barrett

Machi 28–Aprili 3

Kutoka 7–13

“Ikumbukeni Siku Hii, Ambayo Mliondoka kutoka Misri”

Unaposoma na kutafakari Kutoka 7–13, andika mawazo yanayo kuja kwako. Unapofanya hivyo mara kwa mara, uwezo wako wa kutambua minong’ono ya Roho Mtakatifu utakua.

Andika Misukumo Yako

Tauni baada ya tauni iliitesa Misri, lakini Farao alikataa kuwaachilia Waisraeli. Na bado Mungu aliendelea kuonyesha uwezo Wake na kumpa fursa Farao ya kukubali “kwamba Mimi ni Bwana” na “hakuna yeyote kama mimi duniani kote” (Kutoka 7:5; 9:14). Wakati huo, Musa na wana wa Israeli lazima walikuwa wakiangalia kwa msangao kwa maonyesho haya ya uwezo wa Mungu kwa niaba yao. Hakika ishara hizi za mwendelezo zilithibitisha imani yao kwa Mungu na ziliimarisha utayari wao wa kumfuata nabii wa Mungu Hata hivyo, baada ya tauni tisa za kutisha kushindwa kuwaachia huru Waisraeli, ilikuwa tauni ya kumi—kifo cha mzaliwa wa kwanza, ikijumuisha mzaliwa wa kwanza wa Farao—ambayo mwishowe ilimaliza ufungwa. Hii ilionekana kutosheleza kwa sababu kwa namna yoyote ile kifungo cha kiroho, hakika kuna njia moja ya kuepuka. Bila kujali chochote kingine tulichowahi kujaribu wakati uliopita, kwetu sisi kama ilivyokuwa kwa wana wa Israeli. Ni kwa dhabihu ya Yesu Kristo pekee, Mzaliwa wa Kwanza—damu ya Mwana Kondoo asiye na doa—ndiyo itakayotuokoa sisi.

ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Kutoka –11

Ninaweza kuchagua kulainisha moyo wangu.

Ni matumaini yangu kwamba mapenzi yako kamwe si ya kuigiza kupingana na mapenzi ya Mungu kama yalivyokuwa ya Farao. Bado, sisi sote tunazo nyakati ambazo mioyo yetu haiko laini kama inavyopaswa kuwa, hivyo basi kuna jambo la kujifunza kutokana na matendo ya Farao yaliyoandikwa katika Kutoka 7–10. Unaposoma kuhusu tauni hizi katika sura hizi, ni kitu gani kinajionyesha wazi kuhusu majibu ya Farao? Je, unaona mwelekeo wowote unaoelekea kuwa na moyo mgumu ndani yako? Tafakari kile unachojifunza kutoka kwenye milango hii kuhusu inamaanisha nini kuwa na moyo laini.

Fahamu kwamba ya Tafsiri Joseph Smith ya Kutoka 7:3, 13; 9:12; 10:1, 20, 27; 11:10 inafafanua kwamba Bwana hakuufanya mgumu moyo wa Farao—Farao yeye mwenyewe ndiye aliufanya moyo wake uwe mgumu (ona maelezo ya chini ya kila mstari).

Je, unajifunza nini kutoka kwenye maandiko yafuatayo kuhusu kukuza moyo laini? 1 Nefi 2:16; Mosia 3:19; Alma 24:7–8; 62:41; Etheri 12:27.

Ona pia Michael T. Ringwood, “An Easiness and Willingness to Believe,” Liahona, Nov. 2009, 100–102.

Kutoka 12:1–42

Pasaka ni alama ya Upatanisho wa Yesu Kristo.

Njia pekee kwa ajili ya Waisraeli kuepushwa na tauni ile ya kumi, iliyoelezwa katika Kutoka 11:4–5, ilikuwa ni kufuata kwa usahihi maelekezo ambayo Bwana alimpatia Musa katika Kutoka 12, sherehe inayojulikana kama Pasaka. Pasaka inatufundisha kupitia alama kwamba kama vile Bwana alivyowakomboa Waisraeli kutoka utumwani Misri, anaweza pia kutukomboa sisi kutoka kwenye utumwa wa dhambi. Je unapata nini katika maelekezo na alama za Pasaka ambazo zinakukumbusha juu ya Yesu Kristo na Upatanisho Wake? Je alama hizi na maelekezo vinapendekeza nini kwako kuhusu jinsi ya kupokea baraka za Upatanisho Wake? Kwa mfano, je, kuweka damu ya mwanakondoo kwenye miimo ya mlango kunawakilisha nini? (mstari wa 7). Ina maana gani kwako kuwa “mmevaa viatu vyenu miguuni, na fimbo zenu mkononi”? (mstari wa 11).

Ona pia Mafundisho na Maagano 89:21.

watu wakila sakramenti

Sakramenti inatusaidia sisi kumkumbuka Mkombozi wetu, Yesu Kristo.

Kutoka 12:14–17, 24–27; 13:1–16

Sakramenti hunisaidia kukumbuka kukombolewa kwangu kupitia Yesu Kristo.

Mwokozi alitaka Waisraeli daima wakumbuke kwamba Yeye amewakomboa wao, hata baada ya kifungo chao kuwa ni kumbukumbu ya mbali. Hii ndiyo sababu aliwaamuru kuzingatia karamu ya Pasaka kila mwaka. Unaposoma maelekezo yake katika Kutoka 12:14–17, 24–27; 13:1–16, fikiria kuhusu kile unachokifanya ili kukumbuka baraka za Mungu kwako wewe. Je, ni kwa jinsi gani wewe unaweza kuhifadhi kumbukumbu hiyo “kwa vizazi vyako vyote”? (ona Kutoka 12:14, 26–27).

Ni mifanano gani unayoiona kati ya madhumuni ya karamu ya Pasaka na sakramenti? Je, ni kwa jinsi gani kusoma kuhusu Pasaka kunakukumbusha juu ya sakramenti na kuleta maana zaidi kwenye ibada hiyo? Fikiria kile unachoweza kufanya ili “daima umkumbuke” Yesu Kristo (Moroni 4:3; 5:2; ona pia Luka 22:7–8, 19–20).

Ungeweza pia kutafakari vitu vingine ambavyo Bwana anakutaka uvikumbuke; ona, kwa mfano, Helamani 5:6–12; Moroni 10:3; Mafundishon na Maagano 3:3–5, 10; 18:10; 52:40.

Ona pia Yohana 6:54; “Always Remember Him” (video), ChurchofJesusChrist.org; “The Sacrament of the Lord’s Supper,” katika Teachings of Presidents of the Church: Howard W. Hunter (2015), 197–206.

family study icon

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Kutoka 7–12.Pengine baada ya kusoma kuhusu tauni ambazo Bwana alituma kwa Wamisri kama ishara ya uweza Wake, familia ingeweza kushiriki njia ambazo kwazo Bwana anaonyesha uweza Wake leo.

Kutoka 8:2832; 9:27–28, 34–35.Mistari hii inaweza kutumika ili kuanzisha mjadala kuhusu umuhimu wa kushika maneno yetu. Pengine wanafamilia wanaweza kushiriki uzoefu wao juu ya wakati walipowaona watu wengine wakifanya kile walichokubaliana kuwa watafanya.

Kutoka 12:1-42.Baada ya kusoma Kutoka 12:1–42 pamoja, ungeweza kuandika kwenye vipande vya karatasi vitu mnavyoweza kufanya kama familia ili kukumbuka Upatanisho wa Yesu Kristo. Kwa sababu ya damu ya mwanakondoo juu ya miimo ya mlango (ona mstari wa 23) ilimwakilisha Mwokozi, ungeweza kuweka makaratasi haya kuzunguka mlango katika nyumba yako. Mngeweza pia kula baadhi ya vyakula kutoka kwenye Pasaka, kama vile mkate usiotiwa chachu (crakers au tortillas) au mboga chungu za majani (parsley au horseradish), na jadilianeni jinsi Pasaka inavyotusaidia sisi kukumbuka jinsi Mungu alivyowakomboa watu Wake. Kwa mfano, mikate isiyotiwa chachu iliwakumbusha kwamba hapatakuwa na muda kwa ajili ya mkate kabla ya wao kukimbia kutoka kifungoni. Mboga za majani machungu ziliwakumbusha uchungu wa kifungo.

Kutoka 12:14, 24–27.Pengine ungeweza kurejelea mistari hii kama familia kabla ya mkutano ujao wa sakramenti. Je, ni kwa jinsi gani mistari hii inahusiana na sakramenti? Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kwa ukamilifu kabisa kufanya sakramenti kuwa “kumbukumbu” ya kile ambacho Mwokozi amefanya kwa ajili yetu sisi?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “In Memory of the Crucified,” Nyimbo za Kanisa, na. 190.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Fundisha masomo ya vitendo. Waalike wanafamilia kutafuta vitu ambavyo vinawasaidia kuelewa kanuni zinazopatikana katika maandiko mnayosoma. Kwa mfano, vitu laini na vitu vigumu vingewasaidia washiriki wa familia kujadili tofauti kati ya kuwa na moyo laini na moyo mgumu

Familia ya Kiebrania na mlo wa Pasaka

Kielelezo cha mlo wa usiku wa Pasaka na Brian Call