Agano la Kale 2022
Machi 28–Aprili 3. Kutoka 7–13: “Kumbuka Siku hii, Ambayo Ulitoka Misri”


“Machi 28–Aprili 3. Kutoka 7–13: ‘Kumbuka Siku hii, Ambayo Ulitoka Misri,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Kale 2022 (2021)

“Machi 28–Aprili 3. Kutoka 7–13,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2022

Musa, Haruni na Farao

Mchoro wa Musa na Aaron katika baraza la Farao, na Robert T. Barrett

Machi 28–Aprili 3

Kutoka 7–13

“Kumbuka Siku hii, Ambayo Ulitoka Misri”

Unaposoma Kutoka 7–13, fikiria kuhusu jinsi ukweli katika sura hizi unavyoimarisha imani yako kwa Yesu Kristo. Unawezaje kusaidia watoto unaowafundisha kuwa na uzoefu kama huo?

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Weka picha kadhaa ambazo zinawakilisha vitu katika Kutoka 7–13 (kama vile chura, inzi, na mwanakondoo) chini ya kitambaa kwenye meza. Alika watoto kadhaa wachukue moja ya picha kutoka chini ya kitambaa, na waalike darasa kushiriki kile walichojifunza kuhusu picha hii nyumbani wiki hii.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Kutoka 7–11

Bwana ana nguvu juu ya vitu vyote.

Waisraeli walikuwa uhamishoni na hawakuweza kujiweka huru, lakini Bwana alionyesha nguvu Zake na akawaokoa. Je, unawezaje kutumia hadithi hii kuwasaidia watoto kumuamini Bwana na nguvu Zake?

Shughli Yamkini

  • Soma mistari iliyochaguliwa kwenye Kutoka 7–11 ili kuwafundisha watoto kuhusu mapigo kumi ambayo Bwana alituma juu ya Wamisri (ona pia ”Musa Nabii,” katika Hadithi za Aganao la Kale). Waalike watoto kuchora picha ambazo zinaonyesha badhi ya mapigo. Waombe watoto washike picha zao unapo pitia tena mapigo. Soma vifungu vya maneno kwenye Kutoka 7:5 na 9:14 elezea ni kwa nini Bwana alituma mapigo huko Misiri.

  • Shiriki na watoto jinsi Bwana amekuonyesha “ya kuwa hakuna kama [Yeye] ulimwenguni yote” (Kutoka 9:14). Acha watoto washiriki jinsi wanavyojua kuwa Bwana ni mwenye nguvu.

Kutoka 12:1–13; 13:10

Sakramenti inanisaidia kumkumbuka Yesu.

Pasaka iliwafundisha Waisraeli kuhusu Mwokozi na dhabihu ambayo angefanya siku moja kwa ajili yetu. Leo, tunachukua sakramenti kukumbuka dhabihu ya Yesu.

watu wakichukua sakramenti

Sakramenti inatusaidia kumkumbuka Yesu Kristo.

Shughli Yamkini

  • Kutumia Kutoka 12:1–13, waambie watoto yale ambayo Bwana aliwaambia Waisraeli kufanya ili waweze kuokolewa kutoka kwa pigo la mwisho (ona pia “Pasaka,” katika Hadithi za Agano la Kale). Onyesha picha ya Yesu Akimbeba Mwanakondoo Aliyepotea (Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 64) na onyesha kufanana kati ya mwanakondoo aliyetumiwa katika Pasaka na Yesu Kristo, Mwanakondoo wa Mungu.

  • Waombe watoto kutaja vitu tunavyofanya kukumbuka matukio muhimu kama siku za kuzaliwa na likizo. Soma Kutoka 13:10,na uelezee kwamba Bwana aliwataka wana wa Israeli kusherehekea Pasaka kila mwaka ili kuwasaidia kukumbuka kuwa aliwaokoa kutoka kwa Wamisri. Je, ni njia gani kadhaa tunazoweza kukumbuka kuwa Yesu alituokoa kutoka dhambini na kifo?

  • Kama ikiwezekana, tembelea meza ya sakramenti na watoto, na uzungumze jinsi sakramenti inatusaidia kumkumbuka Yesu Kristo. Imbeni pamoja “The Sacrament” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 72) au wimbo mwingine kuhusu kipawa cha Roho Mtakatifu. Wasaidie watoto kutambua hisia za amani walizonazo wanapofikiria kuhusu Mwokozi, na waalike watafute hisia hizo wakati wanachukua sakramenti.

  • Wape watoto vipande vya karatasi na maneno “Naweza kumkumbuka Yesu Kristo wakati wa sakramenti kwa …” iliyoandikwa juu. Waalike watoto kuchora picha wanazoweza kutazama wakati wa sakramenti ili kuwasaidia kumkumbuka Yesu.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Kutoka 7–11

Bwana ana nguvu ya kuniokoa.

Watoto wanakabiliwa na changamoto na wanahitaji Bwana kuwasaidia. Hadithi ya mapigo kumi ambayo Bwana alituma ili kuwaachilia Waisraeli inaweza kuwasaidia watoto kuelewa kuwa Yeye pia ana nguvu ya kuwasaidia.

Shughli Yamkini

  • Mpe kila mtoto karatasi iliyogawanywa katika sehemu kumi, na uwaombe watoto kuchora picha za mapigo yaliyoelezewa katika mistari hii: Kutoka 7:17–18; 8:1–4; 8:16–17; 8:20–22; 9:1–6; 9:8–9; 9:22–23; 10:4–5; 10:21–22; 11:4–7. Je, mapigo yanatufundisha nini kuhusu nguvu ya Mungu? Kwa nini ni muhimu kujua kuhusu nguvu Zake?

  • Waulize watoto kuhusu nyakati walipoona wanahitaji msaada wa Bwana. Anawezaje kutusaidia katika hali hizi? Watie moyo waongee kuhusu nyakati wakati wao au familia zao walipata nguvu ya Bwana katika maisha yao. Toa ushuhuda wako kuwa Bwana ana nguvu ya kutusaidia.

Kutoka 8:28–32; 9:7

Bwana anaweza kunisaidia kuwa na moyo laini.

Farao alichagua kuufanya moyo wake kuwa mgumu wakati Bwana alipomwambia awaachilie wana wa Israeli. Unawezaje kuhamasisha watoto unaowafundisha kuchagua kuwa na moyo laini kwa hivyo kuwa tayari kumtumikia Bwana na kufanya mapenzi Yake?

Shughli Yamkini

  • Leta darasani moja ya kitu ambacho ni kigumu, kama vile mwamba, na kingine ambacho ni laini, kama sponji. Soma na watoto mistari michache kuelezea jinsi Farao alivyojibu mapigo yaliyotumwa na Bwana (ona Kutoka 8:28–32; 9:7), na uwaulize watoto ni kitu gani kinachowakilisha moyo au mtazamo wa Farao. Inamaanisha nini kuwa na moyo laini? (ona Mosia 3:17).

  • Pamoja na darasa, tengeneza orodha ya hatua kadhaa ambazo zinaweza kuonyesha kuwa na moyo mgumu (kwa mfano, kupigana na ndugu au kutokuwa na hamu ya kusali). Je, tunawezaje kumuonyesha Bwana tunataka kuwa na mioyo laini?

Kutoka 11:5–6; 12:1–13

Pasaka inaashiria nguvu ya upatanisho ya Yesu Kristo.

Pasaka iliwafundisha wana wa Israeli kuwa Bwana amewaokoa kutoka Misiri. Pasaka pia ni ishara ya dhabihu ya upatanisho wa Yesu Kristo, ambayo inatuokoa kutoka katika dhambi na kifo. Leo, sakramenti inatusaidia kukumbuka dhabihu ya Yesu Kristo kwa ajili yetu. Kufundisha watoto kuhusu Pasaka kunaweza kuwasaidia kuwa na uzoefu wenye maana zaidi na sakramenti.

Shughli Yamkini

  • Waombe baadhi ya watoto kusoma Kutoka 11:5 kujifunza mapigo ya mwisho ambayo Bwana aliyatuma kwa Wamisri. Waombe watoto kusoma Kutoka 12:3, 5–7, 13 kujifunza jinsi wana wa Israeli walivyookolewa kwenye yale mapigo.

  • Ili kuwasaidia watoto kuelewa kuwa Mwokozi ni Mwanakondoo ambaye atatuokoa, onyesha picha ya mwanakondoo. Alika watoto wasome Kutoka 12:3–7 ili kujua ni kondoo wa aina gani Mungu alitaka watu watumie kwa chakula cha Pasaka. Je, mwanakondoo huyu anafananaje na Yesu Kristo? (Kwa mfano, Yesu alikuwa mkamilifu, na Yesu akamwaga damu yake ili kutuokoa.) Ni ishara gani zingine ambazo hutusaidia kufikiria kuhusu Yesu Kristo?

  • Soma sala za sakramenti pamoja (ona Mafundisho na Maagano 20:77, 79), na tazama video “Always Remember Him” (ChurchofJesusChrist.org). Je, sakramenti inafananaje na Pasaka? Je, tunaweza kufanya nini ili kufikiria kuhusu Yesu wakati wa sakramenti?

  • Shirikiana na watoto moja ya nyimbo unazopenda za sakramenti (ona Nyimbo za kanisa, na. 169–96), na uzungumze kuhusu jinsi inavyokusaidia kukumbuka sadaka ya Mwokozi. Waalike watoto kushiriki wimbo ambao hufanya hivyo kwao.

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kushiriki na familia zao kitu walichojifunza kuhusu Yesu Kristo wakati wa Msingi leo.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wasaidie watoto kupata taswira ya hadithi hii. Watoto wanapokuwa na taswira ya kuona kile wanachojifunza, wana uwezekano mkubwa wa kuikumbuka. Tafuta njia za kuwasaidia watoto kuibua hadithi katika maandiko kwa kutumia vifaa vya kuona kama picha, michoro, video, karagosi, au kichekesho kifupi.