Agano la Kale 2022
Aprili 18–24. Kutoka 18–20: “Yote Ambayo Bwana Amesema Tutayafanya”


“Aprili 18–24. Kutoka 18–20: ‘Yote Ambayo Bwana Amesema Tutayafanya,’” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi: Agano la Kale 2022 (2021)

“Aprili 18–24. Kutoka 18–20,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2022

Picha
mlima

Mlima huko Misri kwa asili unaaminika kuwa Mlima Sinai.

Aprili 18–24

Kutoka 18–20

“Yote Ambayo Bwana Amesema Kama Tutayafanya”

Unaposoma Kutoka 18–20, fikiria juu ya kanuni ambazo zitakuwa na maana zaidi kwa watoto. Unaweza kuhamasishwa kusisitiza kanuni nyingine zaidi ya zile ziliyopendekezwa hapo chini.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike watoto kushiriki moja ya Amri Kumi (au rejea amri chache pamoja nao) na kwa nini wanaona kuwa ni muhimu kutii amri hiyo.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Kutoka 18:8–12

Kushiriki ushuhuda wangu kunaweza kubariki wengine.

Jethro alifurahi wakati Musa aliposhiriki yale ambayo Bwana alikuwa amewafanyia wana wa Israeli. Hadithi hii inaweza kuhamasisha watoto unaowafundisha kushiriki na wengine kile wanachojua kuwa ni kweli.

Shughuli Yamkini

  • Wasomee watoto maneno yafuatayo katika Kutoka 18:8: “Na Musa akamwambia mkwewe yote ambayo Bwana alikuwa amefanya.” Waulize watoto ikiwa wanakumbuka kile Bwana alifanya ili kuwasaidia wana wa Israeli kutoroka kutoka Misri. (Ili kuwasaidia kukumbuka, onyesha picha au kurasa za shughuli kutoka masomo yaliyopita). Je, ni vitu gani Bwana amefanya kutusaidia? Saidia watoto kujua kwamba kama Musa, tunaweza kuwaambia watu wengine juu ya mambo makubwa ambayo Bwana ametufanyia.

  • Darasa la msingi linaweza kuwa mahali pazuri kwa watoto kufanya mazoezi ya kushiriki ushuhuda rahisi. Shiriki ushuhuda wako pamoja nao, na uwasaidie miongoni mwao kweli zingine za injili ambazo wanaziamini.

Kutoka 20:3–17

Mungu hutoa amri kwa sababu anataka niwe na furaha.

Amri ni maagizo ya Baba wa Mbinguni ya kuleta amani katika maisha haya na furaha katika umilele. Unawezaje kuhamasisha watoto kutii amri za Mungu?

Shughuli Yamkini

  • Onyesha picha kutoka “Amri Kumi” (katika Hadithi za Agano la Kale), na waalike watoto kushiriki vile wanavyojua kuhusu hadithi hizo. Wasaidie kuelewa sehemu yoyote ya hadithi hii ambayo hawaielewi vizuri.

  • Unaposoma baadhi ya amri katika Kutoka 20:3–17 kwa watoto (au fafanua kwa maneno wanayoweza kuelewa), waalike wakupe ishara ya kukubali kama amri inahusu jambo ambalo tunapaswa kufanya na ishara ya kukataa kama ni kuhusu jambo ambalo hatupaswi kufanya. Shiriki ushuhuda wako kuhusu furaha inayotokana na kutii amri za Mungu (ona Mosia 2:41).

  • Imba pamoja na watoto wimbo kuhusu jinsi Baba wa Mbinguni anavyotubariki wakati tunapotii amri zake, kama vile“Keep The Commandments””(Kitabu cha Nyimbo za Watoto 146–47). Alika watoto wasikilize maneno ili kujua ni baraka gani tunaweza kupata tunapotii.

Kutoka 20:12

Naweza kuwaheshimu wazazi wangu.

Kuheshimu wazazi ni zaidi ya kuwatii tu. Saidia watoto kuelewa njia zingine wanazoweza kuwaheshimu wazazi wao.

Shughuli Yamkini

  • Wasaidie watoto kujifunza msemo “waheshimu baba yako na mama yako” (Kutoka 20:12). Ikiwa inahitajika, fafanua kwamba “kumheshimu” mtu kunaweza kumaanisha kuwaonyesha heshima au kuwaletea furaha. Je, Yesu alifanya nini kumheshimu Baba Yake wa Mbinguni? Ni kwa vipi alimuheshimu mama yake? (ona Luka 2:48–51; Yohana 19:26–27). Wasaidie watoto wafikirie mambo wanayoweza kufanya kuheshimu wazazi wao, na waalike waigize maoni yao.

  • Alika watoto watengeneze kadi ya shukrani kwa wazazi wao. Wangeweza kuandika au kuchora ndani ya kadi kitu ambacho watafanya ili kuheshimu wazazi wao.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Kutoka 18:13–26

Ninaweza kusaidia “kubeba mzigo” wa kufanya kazi ya Bwana.

Musa alijifunza kwamba kujaribu kuwaongoza wana wa Israeli peke yake “haikuwa nzuri” (Kutoka 18:17). Kupendana na kuhudumiana kunaweza kusaidia kupunguza mizigo ya viongozi wetu.

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kuchora duara nyingi kwenye ubao kuwakilisha washiriki wa kata. Chora duara lililoandikwa askofu. Je, kwa nini itakuwa shida ikiwa Askofu ndiye pekee anayesaidia kila mtu? Someni pamoja Kutoka 18:13–26 kujua ni ushauri gani Yethro alitoa wakati Musa alikuwa akijaribu kufanya kila kitu mwenyewe. Waulize watoto kuweka alama duru zingine kuwakilisha viongozi wengine wa kata na washiriki ambao wanamsaidia Askofu kuwatumikia wengine. Je, Viongozi hawa wengine na waumini hufanyaje kuufanya mzigo wa Askofu kuwa mwepesi? Je, tunawezaje kufanya hivyo kwa viongozi wetu wa kata? kwa wazazi wetu nyumbani?

  • Wasaidie watoto kuandaa orodha ya viongozi katika kata yako. Kama darasa, chagua jina moja na mjadili kile mtu huyu anafanya kukamilisha kazi ya Bwana na kile watoto wanaweza kufanya ili kusaidia.

    Picha
    mwanamume akishikana mikono na mwanamke

    Kutumikia watu wengine ni njia mojawapo ya kusaidia katika kazi ya Bwana.

Kutoka 20:1–7

Ni muhimu kumuweka Bwana kwanza katika maisha yangu.

Sote tuna vitu ambavyo tunaweza kujaribiwa kuweka mbele za Mungu maishani mwetu. Unawezaje kuwasaidia watoto kuelewa ni nini maana ya kumuweka Baba wa Mbingu kwanza?

Shughuli Yamkini

  • Someni pamoja Kutoka 20:1–7, na fafanua kuwa kitu chochote tunachotanguliza mbele kabla ya Mungu maishani mwetu kinaweza kuwa kama “miungu mingine” na “picha zilizochongwa” zilizotajwa katika mistari ya 3–4. Waulize watoto kwa nini Baba wa Mbinguni anataka tumuweke Yeye kwanza. Anatuahidi baraka gani ikiwa tutafanya hivyo? Waulize watoto jinsi tunavyoweza kumuonyesha Baba wa Mbingu kuwa Yeye ni muhimu zaidi kuliko kitu chochote katika maisha yetu.

  • Fikiria kazi ambayo ina hatua ya kwanza muhimu, kama vile kuosha mikono yetu kabla ya kula au kuweka soksi kabla ya kuvaa viatu. Ni nini kinachoweza kutokea ikiwa hatujafanya vitu muhimu kwanza? Je, ni kwa jinsi gani hili ni kama kumuweka Baba wa Mbingu kwanza maishani mwetu? Shiriki ushuhuda wako wa jinsi ulivyobarikiwa kwa kumuweka Mungu kwanza, na waalike watoto kushiriki ushuhuda wao pia.

  • Imba pamoja na watoto wimbo kuhusu Baba wa Mbinguni, kama vile “My Heavenly Father Loves Me” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 228–29). Je, tunajifunza nini kutoka kwenye wimbo kuhusu ni kwa nini ni muhimu kumuweka Baba wa Mbinguni katika maisha yetu?

Kutoka 20:3–17

Mungu hutoa amri kwa sababu anataka niwe na furaha.

Watoto watakuwa na uwezo zaidi wa kushika amri ikiwa wataziona kama njia za upendo wa Mungu na kama fursa za kuelezea upendo wao kwake.

Shughuli Yamkini

  • Tayarisha vipande vya karatasi vyenye amri kutoka kitabu cha Kutoka 20:3–17 ndani yake. Andika nambari moja hadi kumi kwenye ubao, na uwaalike watoto kuviweka vipande kwa mpangilio sahihi kwenye ubao. Ongea kuhusu jinsi tunavyoweza kufuata amri hizi. Kwa maoni, wangeweza kuangalia makala ya Mada za Injili“Amri Kumi” (topics.ChurchofJesusChrist.org).

  • Waalike watoto kuchora picha za maneno muhimu kutoka kwenye amri ili kuwasaidia kuzikumbuka.

  • Eleza hadithi juu ya Chloe kutoka kwa ujumbe wa Dada Carole M. Stephens“If Ye Love Me, Keep My Commandments” (Liahona, Nov. 2015, 118–20). Hadithi hii inatusaidiaje kuelewa ni kwa nini Bwana hutupatia amri? Kuwa mtiifu kunaonyeshaje upendo wetu kwa Mungu?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Alika watoto wafikirie kitu ambacho wangependa kufanya kwa sababu ya kile walichojifunza darasani. Wasaidie kufanya ukumbusho rahisi wa nini watafanya ambacho wanaweza kwenda nacho nyumbani.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Saidia watoto kumtambua Roho. Watoto wanaweza kutambua ushawishi wa Roho. Wafundishe kuwa hisia za amani, upendo, na za dhati wanazokuwa nazo wakati wanapozungumza au kuimba kuhusu Yesu Kristo na injili yake zinatoka kwa Roho Mtakatifu.

Chapisha