Agano la Kale 2022
Aprili 11–17. Pasaka: “Atakimeza Kifo katika Ushindi”


“Aprili 11–17. Pasaka: “Atakimeza Kifo katika Ushindi,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Kale 2022 (2021)

“Aprili 11–17. Pasaka,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2022

Picha
kaburi na jiwe likiwa limeviringishwa mbali na mlango

Mchoro wa kaburi tupu na Maryna Kriuchenko

Aprili 11–17

Pasaka

“Atakimeza Kifo Katika Ushindi”

Unapojiandaa kufundisha, tafakari jinsi unavyoweza kuwasaidia watoto kupata uelewa wa kina na ushuhuda wa Upatanisho wa Yesu Kristo.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waulize watoto ni nini familia zao hufanya kusherehekea Pasaka. Je, Wanafanya nini kukumbuka Ufufuo wa Yesu Kristo?

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Yesu Kristo ni Mwokozi wangu.

Jumapili ya Pasaka ni hafla nzuri ya kuwafundisha watoto juu ya Upatanisho wa Mwokozi huko Gethsemane na kifo chake msalabani. Hii inaweza kuwasaidia kuhisi upendo wa Yesu kwao.

Shughuli Yamkini

  • Onyesha picha ya Mwokozi katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia au picha zingine za dhabihu ya Mwokozi (ona Kitabu cha Sanaa cha Injili, na. 56, 57, 58), na acha watoto washiriki kile wanachojua kuhusu matukio yaliyoonyeshwa kwenye picha. Waambie watoto juu ya mateso ya Yesu huko Gethsemane na msalabani (ona Mathayo 26:36–46; 27:35–50; Luka 22:39–46; Yohana 19:16–30; “Sura ya 51: Yesu Akiteseka katika Bustani ya Gethsemane,” katika Hadithi za Agano Jipya, 129–32). Toa ushuhuda wako kwamba Yesu Kristo alikuwa tayari kuteseka na kufa kwa ajili yetu kwa sababu anatupenda. Waalike watoto kushiriki jinsi wanavyohisi kuhusu Yesu Kristo.

  • Wasomee watoto Yohana 10:9 ukisisistiza maneno ya Yesu “Mimi ni mlango.” Kwa sababu Yesu aliteseka kwa ajili ya dhambi zetu, akafa, na kufufuka, aliwezesha kila mmoja wetu kuishi na Mungu tena. Tumia mlango wa darasa lako kufundisha kuwa Yesu ni kama mlango unaoturuhusu kurudi kwa Baba wa Mbingu.

  • Soma Isaya 53:6 kwa watoto, na waonyeshe picha au mchoro wa kondoo. Acha mmoja wa watoto aweke picha kwenye kona ya mbali ya chumba. Fafanua kwamba tunapofanya maamuzi mabaya, tunapotea kutoka kwa Baba wa Mbinguni kama kondoo anayepotea. Halafu mualike mtoto arudishe kondoo, na shuhudia kwamba kwa sababu Yesu Kristo aliteseka na alikufa kwa ajili yetu, anaweza kuturudisha kwa Baba wa Mbinguni. (Unaweza kuonyesha picha ya Yesu kama mchungaji, kama vile picha ya 64 kwenye Kitabu cha Sanaa cha Injili.)

  • Imbeni kwa pamoja wimbo kuhusu Yesu Kristo, kama vile “I Feel My Savior’s Love” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 74–75). Wasaidie kutambua hisia zozote za amani na upendo wanapokuwa wanaimba. Pia elezea maneno kwenye wimbo yanayoelezea upendo wa Mwokozi. Je, tunawezaje kushiriki upendo Wake na wengine?

Yesu alikufa na akafufuka kwa ajili yangu.

Unawezaje kuwasaidia watoto kujifunza kwamba kwa sababu ya Ufufuo wa Yesu Kristo, sisi na wapendwa wetu tutafufuliwa siku moja?

Picha
Kristo msalabani

Siku ya Majivu Golgotha, na J. Kirk Richards

Shughuli Yamkini

  • Waambie watoto kuhusu kifo cha Yesu na Ufufuko (ona Marko 15–16). Tumia picha zilizo katika muhtasari wa juma hili, picha za 57–60 katika Kitabu cha Sanaa ya Injili, au “Sura ya 54: Yesu Kafufuka” katika Hadithi za Agano jipya (kurasa za 139–44) kuwasaidia watoto kuibua taswira ya hadithi.

  • Saidia watoto kuelewa kwamba ufufuko unamaanisha kuwa baada ya kufa tutaishi tena milele tukiwa namwili mkamilifu na hatutakufa tena. Shiriki ushuhuda wako wa Ufufuo, na waache watoto wafanye kazi kwenye ukurasa wa shughuli wa wiki hii. Alika watoto wautumie ukurasa kushiriki na familia zao hadithi ya Ufufuo wa Yesu.

  • Soma Alma 40:23. kwa watoto. Waonyeshe mkono wako ndani ya glavu. Waambie kwamba mkono wako ni kama roho na glavu ni kama mwili wa kufa. Ondoa glavu kuonesha kuwa tunapokufa, roho zetu zitaiacha miili yetu. Vaa glavu tena kuwakilisha Ufufuo.

  • Imbeni wimbo kuhusu Ufufuo wa Yesu Kristo, kama vile “Did Jesus Really Live Again?” au “Jesus Has Risen” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 64, 70). Toa ushuhuda wako kwamba kwa sababu ya Yesu Kristo tutaishi tena na kuwa na miili mikamilifu baada ya kufa.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Yesu aliteseka kwa ajili yangu.

Unapojifunza Upatanisho wa Mwokozi, tafakari jinsi unavyoweza kusaidia watoto kuelewa jinsi Mwokozi anavyoweza kuwabariki na kuwatia nguvu.

Shughuli Yamkini

  • Wagawanye katika makundi matatu na kila kundi lipe mojawapo ya mafungu yafuatayo ya maandiko: Isaya 53:4–12; Alma 7:11–13; and Mafundisho na Maagano 19:16–19. Waalike watoto watafute maneno na misemo ambayo yanaelezea mambo ambayo Yesu Kristo aliteseka kwa ajili yetu. Waombe waandike majibu yao kwenye ubao na washiriki jinsi wanavyohisi juu ya Mwokozi baada ya kusoma maandiko haya.

  • Andaa vipande vya karatasi. Kwenye nusu ya karatasi, andika marejeleo ya maandiko ya Agano la Kale ya unabii juu ya Yesu Kristo. Kwenye nusu nyingine, andika marejeleo ya maandiko ya Agano Jipya kuhusu jinsi unabii huu ulivyotimizwa. (Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia inaonyesha baadhi ya mifano.) Waalike watoto kusoma vifungu na kulinganisha unabii na utimilifu wao.

  • Saidia watoto kukariri makala ya tatu ya imani. Je, andiko hili linatufundisha nini kuhusu Upatanisho wa Yesu Kristo na mpango wa Baba wa Mbingu kwa watoto wake?

  • Waulize watoto jinsi watakavyoelezea Upatanisho wa Yesu Kristo kwa mtu. Watie moyo watumie maandiko, nyimbo, au picha kuelezea maana ya dhabihu ya upatanisho ya Mwokozi kwao. Ni kwa jinsi gani tumebrikiwa kwa sababu ya Upatanisho wa Mwokozi?

Yesu alikufa na akafufuka kwa ajili yangu.

Ukweli wa ufufuo wa Yesu Kristo unaweza kutuletea tumaini kubwa na furaha—haswa tunapopata kifo cha mpendwa. Unawezaje kuwasaidia watoto kupata faraja katika Ufufuo?

Shughuli Yamkini

  • Onyesha picha ya 57–59 katika Kitabu cha Sanaa ya Injili. Waombe watoto kulinganisha picha na vifungu vifuatavyo: Mathayo 27:29–38; Mathayo 27:59–60; and Yohana 20:10–18. Kisha waalike watoto wasimulie hadithi ya kifo cha Yesu, mazishi, na Ufufuo kwa maneno yao wenyewe.

  • Soma Ayubu 2:14 pamoja na watoto. Alika watoto washiriki jinsi watakavyojibu swali la Ayubu. Wasaidie kupata maandiko yanayoshuhudia ufufuo (ona Mwongozo wa Maandiko,“Ufufuko,” scriptures.ChurchofJesusChrist.org).

  • Soma Musa 1:39 pamoja na watoto. Waulize ikiwa wanajua tofauti kati ya “kutokufa” na “uzima wa milele.” Waalike watafute majibu katika aya ya kwanza ya “Uzima wa Milele” (Mada za Injili, topics.ChurchofJesusChrist.org). Nani atapata kutokufa? Ni nini kinachohitajika kupata uzima wa milele? Toa ushuhuda wako kwamba zawadi zote mbili muhimu zinawezekana kwa sababu ya Upatanisho wa Yesu Kristo.

  • Imba pamoja wimbo wa Pasaka au wimbo wa Kanisa wa Pasaka, kama vile “He Sent His Son” (Kitabu cha Nyimbo cha Watoto, 34–35) or “He Is Risen!” (Nyimbo za Kanisa, na. 199). Alika watoto washiriki jinsi wanavyohisi wakati wanaimba nyimbo hizi. Nyimbo hizi zinatufundisha nini juu ya Baba wa Mbingu na Yesu Kristo? Alika watoto waandike shuhuda zao za Mwokozi na kuzishiriki nyumbani na familia zao.

Picha
ikoni ya kujifunza

Kuhimiza Kujifunza Nyumbani

Ili kuwasaidia watoto kushiriki na familia zao yale waliyojifunza darasani, watie moyo kuimba wimbo nyumbani wiki hii kuhusu Upatanisho wa Yesu Kristo.

Kuboresha Mafundisho yetu

Watoto wanaweza kutambua ushawishi wa Roho. Fundisha watoto kwamba hisia walizonazo wakati wanapozungumza au kuimba juu ya Yesu Kristo na injili Yake zinatoka kwa Roho Mtakatifu na kwamba hisia hizi zinaweza kujenga ushuhuda wao.

Chapisha