Agano la Kale 2022
Maelekezo kwa ajili ya Muda wa Kuimba na Mawasilisho ya Watoto Kwenye Mkutano wa Sakramenti


“Maelekezo kwa ajili ya Muda wa Kuimba na Mawasilisho ya Watoto Kwenye Mkutano wa Sakramenti,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Kale 2022 (2021)

“Maelekezo kwa ajili ya Muda wa Kuimba na Mawasilisho ya Watoto Kwenye Mkutano wa Sakramenti,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watoto: 2022

Picha
watoto wakifanya vitendo wakati wakiimba kanisani

Maelekezo kwa ajili ya Muda wa Kuimba na Mawasilisho ya Watoto Kwenye Mkutano wa Sakramenti

Wapendwa Urais wa Msingi na Viongozi wa Muziki,

Nyimbo za watoto wa Msingi ni zana yenye nguvu sana katika kuwasaidia watoto kujifunza kuhusu mpango wa furaha wa Baba wa Mbinguni na ukweli wa msingi wa injili ya Yesu Kristo. Wakati watoto wanapoimba kuhusu kanuni za injili, Roho Mtakatifu atashuhudia juu ya ukweli wa kanuni hizo. Maneno na muziki vitakaa katika akili na mioyo ya watoto maisha yao yote.

Tafuta msaada wa Roho unapojiandaa kufundisha injili kupitia muziki. Toa ushuhuda wako juu ya ukweli mnaoimba. Wasaidie watoto waone jinsi muziki unavyoshabihiana na kile wanachopitia na kujifunza nyumbani na katika madarasa ya Msingi. Watoto na familia zao watabarikiwa kwa juhudi zako za dhati.

Tunawapenda na tunatoa shukrani zetu kwa huduma ya kujitolea ambayo mnatoa ili kuwaimarisha na kuwalinda watoto wetu wa thamani.

Urais Mkuu wa Msingi

Maelekezo kwa Ajili ya Muda wa Kuimba

Dakika 5 (Urais wa Msingi): Sala ya kufungua, andiko au makala ya imani, na hotuba moja

Dakika 20 (kiongozi wa muziki): Muda wa kuimba

Urais wa Msingi na kiongozi wa muziki huchagua nyimbo kwa ajili ya kila mwezi ili kuimarisha kanuni watoto wanazojifunza katika madarasa yao na nyumbani. Orodha ya nyimbo ambazo zinaimarisha kanuni hizi imejumuishwa katika mwongozo huu. Nyimbo hizi pia zimependekezwa katika muhtasari kwenye Njoo, Unifuate—Kwa Ajili Ya Msingi na Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia.

Unapofundisha nyimbo kwa watoto, waalike waeleze kile ambacho tayari wamejifunza kuhusu hadithi na kanuni za mafundisho katika nyimbo unazofundisha. Unaweza kutaka kurejelea mihutasari ya Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi ambayo watoto wanajifunza katika madarasa yao. Hii itakusaidia wewe kuzijua hadithi na kanuni ambazo wanajifunza ili kwamba uweze kufikiria jinsi ya kuwasaidia kujifunza kupitia muziki.

Wakati wa kuimba, unaweza pia kurejelea nyimbo ambazo watoto walishajifunza hapo awali na nyimbo wanazofurahia kuziimba. Wakati ukifanya marejeo, waalike watoto watoe mawazo na hisia zao kuhusu ukweli unaopatikana katika nyimbo.

Kitabu cha Nyimbo za Watoto ni nyenzo ya msingi ya muziki katika Msingi. Nyimbo kutoka kitabu cha nyimbo za Kanisa na nyimbo kutoka kwenye gazeti la Rafiki au Liahona pia zinafaa. Mara chache watoto wanaweza kuimba nyimbo za kizalendo au za sikukuu ambazo zinafaa kwa ajili ya Jumapili na kwa umri wa watoto. Matumizi ya muziki wowote tofauti kwenye Msingi lazima yaidhinishwe na uaskofu (ona General Handbook: Serving in The Church of Jesus Christ of Latter-day Saints, 12.3.4, ChurchofJesusChrist.org).

Muhtasari wa Msingi

Kila wiki, Msingi hujumuisha:

Muda wa kuimba:Dakika 25

Mapumziko:Dakika 5

Madarasa:Dakika 20

Viongozi wa Msingi wenye idadi kubwa ya watoto wanaweza kuwagawa katika makundi mawili na kuwa na kundi moja katika madarasa ya Msingi wakati kundi lingine wakiwa katika muda wa kuimba. Kisha makundi mawili haya yangeweza kubadilishana nafasi. Katika hali kama hizo, viongozi wanaweza kuhitaji kubadilisha muda uliooneshwa hapo juu ili kuendana na hali zao.

Muziki uliopendekezwa kwa ajili ya Muda wa Kuimba

Januari

  • “I am a Child of God,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 2–3

  • I Know My Father Lives,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto,5

  • “When He Comes Again,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 82–83

Februari

  • “Follow the Prophet,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 110–11 (ubeti wa 3)

  • “He Sent His Son,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 34–35

  • “Choose the Right,” Nyimbo za Kanisa, na.239

Machi

  • Love One Another,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 136–37

  • “Help Me, Dear Father,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto,99

  • “‘Give,’ Said the Little Stream,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto,236.

Aprili

  • Redeemer of Israel,” Nyimbo za Kanisa, na.6

  • Did Jesus Really Live Again?Kitabu cha Nyimbo za Watoto,64

  • Keep the Commandments,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 146–47

Mei

  • I Will Walk with Jesus” (music.ChurchofJesusChrist.org)

  • “Search, Ponder, and Pray,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto,109

  • “I Love to See the Temple,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto,95

Juni

  • “I Will Be Valiant,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto,162

  • A Child’s Prayer,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 12–13

  • “I’m Trying to Be Like Jesus,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 78–79

Julai

  • “The Holy Ghost,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto,105

  • I Know My Father Lives,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto,5

  • “I Love to See the Temple,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto,95

Agosti

  • My Redeemer Lives,” Nyimbo za Kanisa, na.135

  • “I Feel My Savior’s Love,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 74–75

  • “Teach Me to Walk in the Light,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto,177.

Septemba

  • Kindness Begins with Me,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto,145

  • Keep the Commandments,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 146–47

  • I Will Walk with Jesus” (music.ChurchofJesusChrist.org)

Oktoba

  • “I Feel My Savior’s Love,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 74–75

  • I Hope They Call Me on a Mission,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto,169

  • “Families Can Be Together Forever,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 188

Novemba

  • “Follow the Prophet,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 110–11 (ubeti wa7)

  • We Thank Thee, OGod, for a Prophet,” Nyimbo za Kanisa, na.19

  • I Want to Live the Gospel,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto,148.

Desemba

  • “When He Comes Again,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 82–83

  • Seek the Lord Early,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto,108

  • Away in a Manger,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 42–43

Picha
watoto watatu wakiwa wameshikilia picha za Yesu mbele ya chumba cha kanisa

Kutumia Muziki Kufundisha Mafundisho

Muda wa kuimba umekusudiwa kuwasaidia watoto wahisi ushawishi wa Roho Mtakatifu wakati wanapojifunza ukweli wa injili. Mawazo yafuatayo yanaweza kukuvutia wakati ukipanga njia za kufundisha kanuni za injili zipatikanazo katika nyimbo za kanisa na nyimbo za Msingi.

Soma maandiko yanayohusiana. Katika Kitabu cha Nyimbo za Watoto na Kitabu cha Nyimbo za Kanisa, marejeleo kwa ajili ya maandiko yanayohusiana yamejumuishwa pamoja na nyimbo nyingi za watoto na nyimbo za Kanisa. Wasaidie watoto wasome baadhi ya vifungu hivi, na wazungumze kuhusu jinsi maandiko yanavyohusiana na wimbo. Ungeweza pia kuorodhesha marejeleo machache ya maandiko ubaoni na waalike watoto kulinganisha kila rejeleo na wimbo au mstari kutoka kwenye wimbo.

Jaza nafasi zilizo wazi. Andika mstari wa wimbo ubaoni kwa kuacha baadhi ya maneno muhimu. Kisha waombe watoto waimbe wimbo, na kusikiliza maneno ambayo yatajaza nafasi zilizoachwa wazi. Wakati wakijaza kila nafasi iliyo wazi, jadilini ni kanuni zipi za injili wanajifunza kutokana na maneno yanayokosekana.

Tumia dondoo kutoka kwa Viongozi wa Kanisa. Waalike watoto wasikilize dondoo kutoka kwa kiongozi wa Kanisa ambayo inafundisha kanuni sawa ya injili kama ile iliyoko kwenye wimbo wa Msingi. Waombe wainue mikono yao wakati wanaposikia kitu ambacho kinawasaidia wao kuelewa ukweli ambao wanauimba. Waombe kushiriki kile walichosikia.

Toa ushuhuda. Toa ushuhuda mfupi kwa watoto kuhusu ukweli wa injili unaopatikana kwenye wimbo wa Msingi. Wasaidie watoto waelewe kwamba kuimba ni njia mojawapo wanayoweza kutoa ushuhuda na kumhisi Roho.

Simama kama shahidi. Waalike watoto wafanye zamu kusimama na kuelezea kile wanachojifunza kutoka kwenye wimbo wanaoimba au jinsi wanavyohisi kuhusu ukweli uliofundishwa katika wimbo. Waulize wanahisi vipi wakati wanapoimba wimbo, na wasaidie watambue ushawishi wa Roho Mtakatifu.

Tumia picha. Waombe watoto wakusaidie kupata au kutengeneza picha ambazo zinaendana na maneno muhimu au vifungu vya maneno katika wimbo. Waalike waeleze ni jinsi gani picha zinahusiana na wimbo na kitu ambacho wimbo unafundisha. Kwa mfano, kama wewe ndio unafundisha wimbo “When He Comes Again” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 82–83), ungeweza kuweka picha kuzunguka chumba ambazo zinaonyesha maneno muhimu kutoka kwenye wimbo (kama vile malaika, theluji, na nyota). Waombe watoto wakusanye picha na wazinyanyue juu katika utaratibu sahihi wakati mkiimba wimbo kwa pamoja.

Shiriki somo la vitendo. Unaweza kutumia vitendo ili kuhamasisha mjadala kuhusu wimbo. Kwa mfano, wimbo “Seek the Lord Early” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,108) unazungumza kuhusu kumtafuta Bwana. Unaweza kuficha picha ya Mwokozi katika chumba na mwalike mtoto aitafute. Baada ya mtoto kuipata picha, jadilini mambo aliyoyafanya ili kuipata. Hii inaweza kuelekeza kwenye majadiliano kuhusu mambo yaliyotajwa katika wimbo ambayo tunaweza kufanya ili kumtafuta Mungu.

Alika kuelezea uzoefu binafsi. Wasaidie watoto waunganishe kanuni zilizofundishwa kwenye wimbo na uzoefu ambao wamekuwa nao wa kanuni hizo. Kwa mfano, kabla ya kuimba “I Love to See the Temple” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,95), ungeweza kuwaomba watoto wainue mikono yao kama wamewahi kuona hekalu. Waalike wafikirie wakati wakiimba kuhusu jinsi wanavyoweza kuhisi wanapoliona hekalu.

Uliza maswali. Kuna maswali mengi ambayo unaweza kuuliza wakati mnaimba nyimbo. Kwa mfano, unaweza kuwauliza watoto wanajifunza nini kutoka kwenye kila mstari wa wimbo. Pia unaweza kuwaomba wafikirie maswali ambayo yanajibiwa na wimbo. Hii inaweza kuongoza kwenye majadiliano kuhusu ukweli unaofundishwa katika wimbo.

Sikiliza majibu. Waombe watoto wasikilize majibu ya maswali. Kwa mfano, wimbo “He Sent His Son” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 34–35) una maswali na majibu. Unaweza kuwauliza watoto maswali na kisha watake wasikilize majibu wakati wakiimba.

Kuwasaidia Watoto Wajifunze na Wakumbuke Nyimbo za Msingi na Nyimbo za Kanisa

Watoto hujifunza wimbo kwa kusikiliza na kuuimba tena na tena. Mara zote yaimbe maneno ya wimbo mpya kwa watoto—usiyasome tu au kuyakariri. Hii huwasaidia watoto kuunganisha sauti ya muziki na maneno. Baada ya wimbo kufundishwa, urejelee wimbo katika njia tofauti za kufurahisha kwa mwaka mzima. Chini ni baadhi ya mawazo ya kuwasaidia watoto kujifunza na kurejelea nyimbo.

Tengeneza mabango. Onesha mabango yakiwa na maneno kutoka kwenye kila mstari au picha ambayo huwakilisha maneno. Wakati watoto wakiimba, funika baadhi ya maneno au picha mpaka waweze kuimba mstari mzima bila bango. Pia unaweza kuwaalika watoto wakusaidie kutengeneza mabango.

Onesha kwa mfano mpangilio wa sauti. Ili kuwasaidia watoto kujifunza sauti ya muziki wa wimbo, weka mkono wako kwa upana, na wakati ukiimba maneno, peleka mkono wako juu kuonesha sauti ya juu na chini kuonesha sauti ya chini.

mwangwi. Waalike watoto wawe mwangwi wa sauti yako kwa kurudia kile unachokiimba. Waimbie watoto kifungu kifupi cha maneno au mstari, kisha waache waimbe kwa kurudia.

Tumia njia tofauti tofauti. Imba nyimbo katika njia tofauti tofauti, kama vile kwa kunong’ona, kwa kuimba midomo ikiwa imefumba, kwa kupiga makofi mapigo ya muziki, kwa kubadilisha kasi ya muziki, au kuimba ukiwa umekaa au kusimama. Pia ungeweza kutengeneza mchemraba kwa karatasi na, kwenye kila upande wa mchemraba, andika njia tofauti ya kuimba. Mwalike mtoto kuzungusha mchemraba kuchagua njia gani watoto wataimba wimbo.

Imbeni katika makundi. Lipe kila darasa au mtu mmoja mmoja kifungu cha maneno cha kuimba wakati wamesimama, na kisha waache wabadilishane vifungu hivyo mpaka kila darasa au kila mtu awe amepata zamu ya kuimba kila kifungu.

Tumia matendo ya mikono. Waalike watoto wafikirie kuhusu matendo rahisi ya mikono ili kuwasaidia kukumbuka maneno na ujumbe wa wimbo. Kwa mfano, mnapoimba “Reverently, Quietly” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,26), unaweza kuwaalika watoto kukunja mikono yao, kuinamisha vichwa vyao, na kugusa mioyo yao wakati wanapoimba mistari husika katika wimbo.

Wasichana wanaimba, wavulana wanaimba. Chora picha ya mvulana na picha ya msichana, na zibandike katika fimbo tofauti. Wakati mkiupitia upya wimbo, inua mojawapo ya picha kuonesha nani anatakiwa kuimba sehemu hiyo ya wimbo.

Kikapu cha kurushia vitu. Weka vikapu au vyombo vingine vyenye namba mbele ya darasa—vyombo vingi kulingana na idadi ya beti za wimbo fulani. Mwalike mmoja wa watoto kurusha kifuko chenye mbegu au karatasi iliyokunjwa ndani ya au karibu na chombo chenye namba. Watake watoto waimbe ubeti wenye namba sawa na ile iliyo kwenye chombo.

Oanisha picha na kifungu cha maneno. Andika kila mstari wa wimbo kwenye kipande tofauti cha karatasi, na kisha tafuta picha ambayo inawakilisha kila mstari. Weka picha kwenye upande mmoja wa chumba na karatasi upande mwingine. Imbeni wimbo, na waombe watoto waoanishe picha na maneno.

Picha
watoto wawili wakiimba kanisani

Miongozo kwa ajili ya Mawasilisho Kwenye Mkutano wa Sakramenti

Chini ya maelekezo ya askofu, mawasilisho ya watoto kwenye mkutano wa sakramenti kwa kawaida hufanyika katika robo ya nne ya mwaka. Kama urais wa Msingi na kiongozi wa muziki, pangeni kukutana mapema katika mwaka pamoja na mshauri katika uaskofu mwenye kusimamia Msingi ili kuanza kujadili mipango ya mawasilisho. Mnapokuwa mmekamilisha mipango, pata ruhusa yake kwa ajili ya mawasilisho hayo.

Uwasilishaji sharti uwaruhusu watoto kuwasilisha kile ambacho wao na familia zao wamejifunza kutoka kwenye Agano la Kale nyumbani na katika Msingi, ikijumuisha nyimbo za Msingi walizoimba katika kipindi cha mwaka. Kwa sala fikiria kanuni zipi za injili na nyimbo zinaunga mkono kile ambacho wamejifunza. Katika mwaka mzima, weka kumbukumbu ya hotuba za watoto na uzoefu binafsi kwa ajili ya matumizi wakati wa mawasilisho. Waalike watoto kushiriki maandiko, hadithi na shuhuda zao katika mawasilisho. Wakati ukipanga uwasilishaji, fikiria njia ambazo zitasaidia mkusanyiko kufokasi kwa Baba wa Mbinguni na kwa Mwokozi na mafundisho Yao.

Matawi yenye idadi ndogo ya watoto yanaweza kufikiria njia ambazo wanafamilia wanaweza kushiriki pamoja na watoto wao. Mshiriki wa uaskofu anaweza kuhitimisha mkutano kwa hotuba fupi.

Wakati ukiandaa mawasilisho, kumbuka mwongozo ufuatao:

  • Mazoezi yasichukue muda usio wa lazima kutoka kwenye madarasa ya Msingi au familia.

  • Vitu vya kuona, mavazi maalumu, na mawasilisho ya kimtandao havifai kwa ajili ya mkutano wa sakramenti

Ona General Handbook: Serving in The Church of Jesus Christ of Latter-day Saints, 12.2.1.2, ChurchofJesusChrist.org.

Chapisha