Agano la Kale 2022
Aprili 4–10. Kutoka 14–17: “Simama Imara, na Uone Wokovu wa Bwana”


“Aprili 4–10. Kutoka 14–17: ‘Kutoka 14–17: “Simama Imara, na Uone Wokovu wa Bwana,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Kale 2022 (2021)

“Aprili 4–10. Kutoka 14–17,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2022

Picha
Bahari ya Shamu

Bahari ya Shamu

Aprili4–10

Kutoka 14–17

“Simama imara, Uone Wokovu wa Bwana”

Unaposoma Kutoka 14–17, andika misukumo ya kiroho unayopokea. Misukumo hii inaweza kukusaidia kupanga kufundisha maandiko na kweli ulizojifunza kutoka kwa watoto.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Kutoka 14–17 imejaa na hadithi za kukumbukwa. Waalike baadhi ya watoto kushiriki hadithi wanayoijua kutoka sura hizi, pamoja na kitu walichojifunza kutoka kwake.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Kutoka 14:5–22

Bwana alimwokoa Musa na watu wake.

Kugawanya Bahari Nyekundu ulikuwa muujiza ambao uliwaonyesha Musa na Waisraeli jinsi Bwana alivyo na nguvu. Kujua kuhusu nguvu Yake kunaweza kuwasaidia watoto kumwamini Yeye.

Shughuli Yamkini

  • Fikiria njia za kushiriki hadithi ya Waisraeli kuvuka Bahari Nyekundu kwa njia ya kufurahisha na ya kukumbukwa. Kwa mfano, wewe au mshiriki mwingine wa kata angeweza kuvalia mavazi kama Musa na kusimulia hadithi kutoka kwenye Kutoka 14:5, 9–10, 13–16, 19–22. Watoto wangeweza kufanya viti ni kama Bahari Nyekundu, na wanaweza kumfuata mtu anawakilisha Musa wakati anafanya njia kati yao. Au watoto wanaweza kujifanya kama maji na kusogea kutenganisha pande za chumba wakati Musa anagawanya. Sisitiza kwamba Bwana alimpa Musa nguvu ya tenganisha bahari ili Waisraeli waweze kuokolewa kutoka utumwani.

  • Waalike watoto wapake rangi ukurasa wa shughuli unarejelea hadithi kutoka kweny Kutoka 14:5–22. Kisha wangefanya kazi pamoja ya kuelezea hadithi kwa kutumia ukurasa wa shughuli.

Kutoka 15:23–25; 16:14–15; 17:1–6

Bwana atatoa mahitaji yangu.

Simulizi za Bwana kutoa chakula na maji kwa Waisraeli nyikani zinatufundisha kuwa anaweza kutupatia mahitaji yetu. Tafakari ni nini unaweza kufanya ili kuwashirikisha watoto katika kujifunza hadithi hizi.

Picha
mwanamke akikusanya mana

Mana kutoka kwa Mungu iliwalisha Waisraeli kimwili, tunahitaji pia lishe ya kiroho ya kila siku. Fresco na Leopold Bruckner

Shughuli Yamkini

  • Wasaidie watoto kuigiza matukio katika Kutoka 15:23–25; 16:14–15; 17:1–6, kujifanya kuwa Musa au Waisraeli. Ikiwezekana , leta kitu cha kusaidia kusimulia kila hadithi, kama vile tawi (kuponya maji huko Mara), jagi au sufuria (kujaza mana), na kijiti na mwamba (kwa ajili ya maji huko Horebu). Je, Mungu aliwatunzaje Waisraeli? Je, Yeye hututunza vipi kila siku?

  • Kwa kifupi shiriki hadithi katika Kutoka 15:23–25; 16:14–15; 17:1–6 (ona pia “Musa Akiwaongoza Waisraeli,” katika Hadithi za Agano la Kale). Je, tunajifunza nini kuhusu Mungu kutoka kwenye hadithi hizi? Tunajifunza nini kuhusu Mungu kutoka mistari hii?

Kutoka 17:8–16

Naweza kumkubali nabii wetu.

Hadithi ya Haruni na Huri ya kushikilia mikono ya nabii Musa inaweza kulinganishwa na juhudi zetu za kumkubali nabii wetu aliye hai.

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto watatu kusimama mbele ya chumba na wamuwakilishe Musa, Haruni, na Huri wakati unasimulia hadithi hiyo kutoka kwenye Kutoka 17:8–16. Je, tunaweza kufanya nini leo kumsaidia nabii wetu, kama vile Haruni na Huri walivyomsaidia nabii Musa?

  • Onyesha picha ya nabii aliye hai, na uwaulize watoto yeye ni nani. Saidia watoto kukumbuka mambo kadhaa ambayo nabii amefundisha hivi karibuni. Waulize watoto kushiriki njia kadhaa wanazomfuata nabii. Imba pamoja mistari michache ya “Follow the Prophet,” pamoja na mstari wa mwisho (Children’s Songbook, 110–11).

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Kutoka 14:5–22

Naweza kujifunza kila wakati kumfuata Roho.

Musa alijua kwa ufunuo jinsi ya kuwaongoza Waisraeli kuvuka Bahari Nyekundu Mafundisho na Maagano 8:2–3). Hadithi hii inawezaje kuwasaidia watoto unaowafundisha kujifunza kutenda kuhusu ufunuo binafsi?

Shughuli Yamkini

  • Onyesha picha ya Musa akitenganisha maji ya Bahari Nyekundu katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo Unifuate—Kwa Watu Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Waombe watoto kurejea Kutoka 14:5–22 na kushiriki kile wanachokijua kuhusiana na hadithi hii. Ni kipi Mafundisho na Maagano 8:2–3 inaongeza kwenye uelewa wetu wa hadithi hii? Simulia kuhusu wakati ambapo Roho Mtakatifu alikwambia kitu katika akili zako au moyo wako na waalike watoto washiriki uzoefu wao.

  • Wakumbushe watoto hadithi ya Nefi akifuata roho mtakatifu alipoenda kupata bamba za shaba (ona 1Nefi 4:1–6). Wasaidie watoto kuona kwamba Musa pia alipaswa kufuata Roho wakati alipoongoza watu wake kuvuka Bahari Nyekundu. Wasaidie watoto waandike mstari mpya kwenye “Ujasiri wa Nefi” (Kitabu cha Nyimbo za watoto, 120–21) kuhusu jinsi Bwana alivyompa njia Musa wakati alipoonyesha ujasiri na kumfuata Roho. Imbeni mstari mpya kwa pamoja.

Kutoka 15:23–25; 16:14–15; 17:1–6

Bwana atatoa mahitaji yangu.

Ikiwa tutamgeukia Yesu Kristo, anaweza kutusaidia wakati wa hali ngumu katika maisha yetu, kama vile Yeye alivyowasaidia wana wa Israeli.

Shughuli Yamkini

  • Gawanya darasa katika jozi au vikundi vidogo, na wape kila kikundi kusoma moja ya vifungu vifuatavyo: Kutoka 15:23–25; 16:14–15; 17:1–6. Waulize watoto katika kila kikundi kuchora picha zinazowakilisha kile walichosoma katika aya hizi, na kisha waombe washiriki wengine wa darasa kubaini wamechora nini. Saidia watoto kutambua kile hadithi hizi zinafundisha kuhusu Yesu Kristo. Je, watu wanayo majaribu gani leo? Je, Baba wa Mbingu na Yesu Kristo hutusaidiaje na majaribu yetu?

  • Unapokariri hadithi hizi, waulize watoto kwa nini mkate na maji vilikuwa muhimu sana kwa wana wa Israeli? Je, ni nini kingefanyika ikiwa wasingekuwa na vitu hivi? Saidia watoto kuelewa kwamba mkate na maji ya sakramenti ni muhimu kiroho kwetu (ona Yohana 4:13–14; 6:35, 48–51). Unaweza kuwaomba watoto kushiriki hisia zao kuhusu sakramenti.

Kutoka 17:8–16

Tumebarikiwa tunapowakubali viongozi wetu wa Kanisa.

Wana wa Israeli walishinda katika vita dhidi ya Amaleki pale tu Musa alipokuwa ameinua mikono yake angani. Je, tunaweza kujifunza nini kuhusu kuwakubali viongozi wetu kutoka kwenye hadithi hii?

Shughuli Yamkini

  • Kuwasaidia watoto kurudia hadithi katika Kutoka 17:8–16, andika ubaoni: Nani alimsaidia Musa kipindi cha mapigano? Walifanya nini? Matokeo yalikuwa yapi? Waalike watoto kutafuta majibu katika mistari. Hadithi hii inafundisha nini kuhusu jinsi tunavyoweza kusaidia ufalme wa Mungu kufanikiwa? Je, tunaweza kufanya nini kuunga mkono, kukuza na kuwafuata viongozi wetu wa Kanisa?

  • Alika watoto wasome Kutoka 17:8–16 na wachore picha ya kile walichosoma. Watie moyo waandike juu ya mchoro wao ujumbe wanaojifunza kutoka kwenye hadithi. Kwa nini huu ni ujumbe muhimu kwetu leo?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Alika watoto wachague moja ya hadithi kutoka kwenye majadiliano yako ya leo. Wasaidie kufikiria kuhusu kitu wanachoweza kufanya wakati wa wiki ijayo ili kutumia yale ambayo hadithi hiyo inafundisha.

Kuboresha Mafundisho Yetu

Watoto wanapenda hadithi Watoto wanaelewa vizuri zaidi kanuni za injili wakati wanaweza kuziona kwenye maisha ya watu halisi. Unaposhiriki hadithi za maandiko, fikiria kushiriki uzoefu kutoka kwenye maisha yako ambayoo hufundisha kanuni sawa. Unaweza pia kuwaalika watoto kushiriki uzoefu wao.

Chapisha