“Waisraeli wakiwa Nyikani,” Hadithi za Agano la Kale (2022)
“Waisraeli wakiwa Nyikani,” Hadithi la Agano la Kale
Waisraeli wakiwa Nyikani
Kujifunza kumtegemea Bwana
Mara baada ya Waisraeli kuondoka Misri, walilalamika kuwa hawakuwa na chakula cha kutosha. Walisema ilikuwa bora kuwa watumwa Misri kuliko kufa na njaa nyikani.
Kuwafundisha Waisraeli kumtumaini Yeye, Bwana alituma mkate kutoka mbinguni kwa ajili yao waokote kila siku. Waliita mkate huo mana. Ulikuwa mtamu kama asali. Bwana hakuleta mkate siku ya Sabato, siku ya saba ya juma. Hivyo siku ya sita, aliwaambia waokote wa kutosha kula siku mbili.
Kwa muda fulani, Bwana pia alituma kwale kwa ajili ya kuliwa na Waisraeli. Asubuhi waliokota mana, na jioni waliokota kwale. Bwana aliwataka Waisraeli kujifunza kumtumaini Yeye. Katika njia hii, ndivyo alivyowatunza huko nyikani.