“Yusufu na Baa la Njaa,” Hadithi za Agano la Kale (2022)
“Yusufu na Baa la Njaa,” Hadithi za Agano ;a Kale
Yusufu na Baa la Njaa
Nafasi ya kaka ya kuunganisha familia yake
Familia ya Yakobo walikuwa wenye njaa kwa sababu ya ukosefu wa chakula. Hivyo Yakobo aliwatuma wanawe kwenda Misri kununua chakula. Alimwacha mwanawe mdogo, Benyamini, nyumbani. Aliogopa kumpoteza Benjamini kama alivyompoteza mwanawe Yusufu miaka mingi kabla. Yeye hakujua kwamba wanawe wakubwa walikuwa wamemuuza Yusufu kama mtumwa.
Wakati huo, Yusufu alikuwa kiongozi mkubwa katika Misri. Alikuwa na madaraka ya kuuza chakula wakati wa njaa. Wakina kaka walikutana na Yusufu na wakamwomba awauzie chakula Wao hawakumtambua.
Yusufu aliwatambua, lakini alijifanya hawatambui. Aliwauliza kuhusu familia yao ili kuona kama baba na kaka yake Benyamini walikuwa wako hai.
Kisha Yusufu akawapa nduguze chakula. Akawaambia wasirudi tena kwa ajili ya chakula zaidi isipokuwa wamemleta mdogo wao, Benyamini, pamoja nao.
Familia ilipoishiwa chakula tena, Yakobo alijua itambidi ampeleke Benyamini pamoja na wanawe tena Misri. Yakobo bado alikuwa mwoga kuhusu kumruhusu Benyamini aende. Lakini Yuda, mmoja wa wakina kaka, akaahidi kuwa angemtunza salama Benyamini.
Wakina kaka waliporejea Misri, Yusufu alifanya ionekane kana kwamba Benyamini aliiba kikombe kile cha fedha. Alitaka kuona kama kaka zake wakubwa walikuwa wamebadilika. Yuda aliomba na kumsihi Yusufu asimwadhibu Benyamini badala yake amwadhibu yeye Yuda.
Yusufu alifurahi kuona kwamba kaka zake walikuwa wamebadilika. Walimpenda Benyamini vya kutosha kiasi cha kumlinda. Hivyo basi, mwishowe, Yusufu akawaambia kuwa yeye ni nani.
Yusufu aliwasamehe kaka zake kwa kumuuza yeye utumwani. Yusufu aliwaambia kwamba hiyo ilikuwa njia ya Bwana kuisaidia familia yao kuokoka na baa la njaa.
Kaka zake Yusufu walirudi kwa baba yao, Yakobo, na kumwambia yale yote ambayo yametokea. Yakobo alihamishia familia yake yote huko Misri.
Farao akiikaribisha familia ya Yakobo. Akawapa ardhi na wanyama ili waweze kuwa na chakula kingi. Familia ya Yakobo iliishi kwa amani kwa muda mrefu.