Scripture Stories
Elisha Anamponya Naamani


“Elisha Anamponya Naamani,” Hadithi za Agano la Kale (2022)

“Elisha Anamponya Naamani,” Hadithi za Agano la Kale

2 Wafalme 5

Elisha Anamponya Naamani

Ni muujiza mkubwa ulioje uliofuatia imani

Picha
Naamani kitandani, yu mgonjwa

Mbali kule katika Shamu aliishi mtu aliyeitwa Naamani. Alikuwa jemedari mkuu katika jeshi la Shamu. Lakini Naamani alikuwa na ugonjwa mkali wa ngozi unaoitwa ukoma.

2 Wafalme 5:1

Picha
Msichana wa Kiisraeli akiongea na mke wa Naamani

Mtumishi wa mke wa Naamani alikuwa msichana wa Kiisraeli. Msichana huyu alikuwa na imani katika Bwana. Alsema kwamba kama Naamani angeweza kumtembelea nabii Elisha, Naamani anaweza kuponywa kutokana na ugonjwa wake.

2 Wafalme 5:2–4

Picha
Naamani akisafiri kumtafuta Elisha

Naamani alisafiri umbali mrefu ili kumtafuta Elisha. Naamani alifikiri angeponywa kwa muujiza mkubwa.

2 Wafalme 5:5–8

Picha
Naamani akizungumza na mtumishi wa Elisha

Naamani alikuja nyumbani kwa Elisha pamoja na watumishi wake, farasi, na magari ya kukokotwa na farasi. Elisha alimtuma mtumishi wake kumpa Naamani maelekezo ya Bwana. Bwana angemponya Naamani kama angejiosha yeye mwenyewe katika mto Yordani mara saba.

2 Wafalme 5:9–10

Picha
Naamani akinung’unika kando ya mto

Naamani alikasirika kwa sababu alitaka nabii wa Bwana atoke nje na kumponya yeye haraka. Naamani alinungunika kwamba Mto Yordani haukuwa mkubwa kama mito mikubwa iliyoko Shamu.

2 Wafalme 5:11–12

Picha
Mtumishi akiongea na Naamani kando ya mto

Lakini mtumishi wa Naamani alimwuliza Naamani kwa nini asifanye kazi rahisi kama hiyo. Hata kama ilikuwa haileti maana kwa Naamani, lakini nabii wa Bwana amemtaka yeye alifanye hilo.

2 Wafalme 5:13

Picha
Naamani ndani ya Mto Yordani, ameponywa

Naamani akakoma kuwa na kiburi na akawasikiliza watumishi wake. Alijiosha yeye mwenyewe mara saba katika Mto Yordani. Kisha Bwana akamponya Naamani, kama Elisha alivyosema. Naamani alijua kwamba Elisha alikuwa nabii na kwamba kweli Bwana yupo.

2 Wafalme 5:14–15

Chapisha