Scripture Stories
Isaya Nabii


“Isaya Nabii,” Hadithi za Agano la Kale (2022)

“Isaya Nabii,” Hadithi za Agano la Kale

Isaya 6–79; 53–54

Isaya Nabii

Unabii kuhusu Bwana Yesu Kristo.

Picha
Isaya akiwa ameitwa na Bwana

Waisraeli mara nyingi walishindwa na walitaka Bwana awalinde. Siku moja ndani ya hekalu, Bwana alimwita mtu aliyeitwa Isaya ili awafundishe watu kuhusu kuja kwa Kristo. Isaya aliwapenda watu na akawafundisha kuhusu jinsi ambavyo Kristo angewaokoa.

Isaya 6:1–8

Picha
Isaya akitoa unabii juu ya kuzaliwa kwa Yesu

Isaya alijifunza kwamba Yesu Kristo angekuja siku moja kuwaokoa watu Wake kutokana na dhambi. Lakini sio kila mtu angemtambua Yeye kama Mwokozi wao. Isaya alihuzunika sana kwa sababu alijua kuwa watu wengi hawangeamini katika Yesu Kristo.

Isaya 6:9–13; 7:14; 53:1–9

Picha
Isaya akiandika kuhusu Ujio wa Pili wa Kristo

Lakini Isaya pia alitoa unabii juu ya Ujio wa Pili wa Yesu Kristo. Yesu Kristo atarudi tena na kuwa Mfalme wa Dunia yote. Atarudi tena na kukamilisha mpango wa Baba Yake kwa kuleta ukarimu na amani milele. Isaya alisema kila mmoja angejua kuwa Yesu Kristo ni Mwokozi wao.

Isaya 9:6–7; 54:1–10

Chapisha