“Ndoto za Yusufu zenye Mwongozo wa Kiungu,” Hadithi za Agano la Kale (2022)
“Ndoto za Yusufu zenye Mwongozo wa Kiungu,” Hadithi za Agano la Kale
Ndoto za Yusufu zenye Mwongozo wa Kiungu
Mahangaiko ya familia katika kupendana
Raheli na Yakobo waliomba kwa miaka mingi ili wapate mtoto wa kiume. Bwana alijibu maombi yao Yusufu alipozaliwa. Yusufu alikuwa mwana mpendwa wa Yakobo, na akampatia Yusufu koti maalumu. Wana10 wakubwa wa Yakobo waliona wivu.
Wakati Yusufu alipokuwa na umri wa takribani miaka 17, alipata mwongozo wa kiungu katika ndoto kwamba alikuwa akikusanya nafaka shambani pamoja na kaka zake. Fungu la nafaka la Yusufu likasimama wima. Lakini mafungu ya nafaka ya kaka zake yakaliinamia fungu la Yusufu. Yusufu alipowaambia kaka zake kuhusu ndoto hiyo, wakamkasirikia.
Baadae, Yusufu akapata mwongozo mwingine wa kiungu kwa njia ya ndoto. Katika ndoto hii, jua, mwezi, na nyota 11 zilimsujudia yeye. Yusufu aliwaambia familia yake kuhusu ndoto hiyo. Ndoto hii ilifanya isikike kama Yusufu angekuwa mtawala juu ya familia. Kaka zake Yusufu wakawa wamemkasirikia zaidi. Hawakuzipenda ndoto zake.
Siku moja kaka zake Yusufu walikuwa mbali na nyumbani wakiwalisha kondoo. Yakobo alimtuma Yusufu kwenda kuwaangalia.
Baadhi ya kaka zake Yusufu walitaka kumuua. Walilichukua koti la Yusufu na yeye wakamtupa shimoni.
Yusufu alipokuwa shimoni, kaka zake waliwaona wasafiri wakienda Misri. Kaka zake wakaamua kumuuza Yusufu kama mtumwa kwa wasafiri wale kwa vipande 20 vya fedha.
Kisha kaka zake Yusufu wakaweka damu ya mbuzi kwenye koti lake. Wakina kaka wakaenda kwa baba yao, Yakobo, na wakamwonyesha lile koti. Wakamdanganya Yakobo na kumwambia kwamba mnyama wa porini amemuua Yusufu.
Yakobo alilia kwa sababu alifikiri kuwa Yusufu alikuwa amekufa.
Lakini Yusufu alikuwa bado yu hai Alikuwa mbali sana na nyumbani katika Misri, akiishi kama mtumwa.