“Malaki Nabii,” Hadithi za Agano la Kale (2022)
“Malaki Nabii,” Hadithi za Agano la Kale
Malaki Nabii
Kuishi sheria ya zaka
Wayahudi walilipa zaka kwa kutoa sehemu moja ya kumi ya mazao na wanyama wao kwa Bwana. Bwana aliwabariki walipolipa zaka. Lakini baadhi ya Wayahudi walianza kutoa mkate mbovu au mnyama asiyeona au mgonjwa kama zaka. Wakabakisha kilicho bora kwa ajili yao wenyewe.
Mwanzo 14:20; 28:22; Kumbukumbu la Torati 12:6, 11, 17; Malaki 1:7–8, 12–13
Bwana hakupendezwa. Malaki nabii, aliwaambia Wayahudi walikuwa wakimwibia Bwana walipokuwa siyo waaminifu katika kulipa zaka. Malaki aliwaambia watubu.
Bwana aliwapa Wayahudi ahidi. Kama watatoa zaka ya uaminifu, Bwana angewamwagia baraka kubwa kutoka mbinguni.