Scripture Stories
Samweli Nabii


“Samweli Nabii,” Hadithi za Agano la Kale (2022)

“Samweli Nabii,” Hadithi za Agano la Kale

1 Samweli 2–3

Samweli Nabii

Kijana aliyeitwa na Bwana

Picha
Eli akizungumza na watu

Kwa miaka mingi, Waisraeli hawakuwa na nabii wa Bwana wa kuwaongoza. Badala yake, waamuzi waliongoza Israeli kwa miaka mingi. Wakati wa kipindi hiki, Hanna alimleta kijana wake mdogo Samweli kuishi na Eli, kuhani na mwamuzi wa Israeli. Samweli alimsaidia Eli hekaluni.

1 Samweli 2:11, 18, 26; 3:1

Picha
Wana wa Eli wakiiba bidhaa

Wana wawili wa Eli pia walihudumu hekaluni, lakini waliiba matoleo yaliyokusudiwa kwa ajili ya Bwana. Baadhi ya watu walimlalamikia Eli, lakini Eli hakuwaadhibu wana wake.

1 Samweli 2:12–17, 22–23

Picha
Samweli

Usiku mmoja Samweli alisikia sauti ikimwita. Alidhani ilikuwa ya Eli, hivyo Samweli alikwenda kwa Eli. Lakini Eli hakumwita. Eli alimwambia Samweli arudi kulala.

1 Samweli 3:3–5

Picha
Samweli akizungumza na Eli

Samweli alisikia sauti ikimuita mara ya pili. Alikwenda kwa Eli na kumuuliza kile alichohitaji. Lakini Eli hakumwita. Eli alimwambia Samweli arudi kulala.

1 Samweli 3:6

Picha
Eli akizungumza na Samweli

Samweli alisikia sauti ikimwita mara ya tatu. Alikwenda tena kwa Eli na kumuuliza kile alichohitaji. Mara hii, Eli alijua kwamba alikuwa ni Bwana aliyekuwa akizungumza na Samweli. Eli alimwambia Samweli arudi kulala. Eli alisema ikiwa Bwana ataita tena, Samweli alipaswa kusikiliza.

1 Samweli 3:8–9

Picha
Samweli akizungumza na Mungu

Samweli alisikia sauti ikimwita tena. Safari hii Samweli alimwomba Bwana azungumze na alisema kuwa angesikiliza. Bwana alimwambia Samweli kwamba ilikuwa makosa kwa Eli kuwaruhusu wana wake waovu kuhudumu hekaluni. Familia ya Eli haingeruhusiwa kuhudumu hapo tena.

1 Samweli 3:10–14

Picha
Samweli na Eli wakizungumza

Siku iliyofuata, Eli alimuuliza Samweli kile Bwana alichosema. Samweli alimwambia. Eli alifahamu kwamba Bwana alizungumza kupitia Samweli.

1 Samweli 3:15–18

Picha
Samweli akiwatazama watu

Habari zilienea kote katika nchi ya Israeli. Watu walifahamu kwamba Bwana alimchagua Samweli kuwa nabii Wake.

1 Samweli 3:19–20

Chapisha