Hadithi za Maandiko
Debora Nabii Mke


“Debora Nabii Mke,” Hadithi za Agano la Kale (2022)

“Debora Nabii Mke,” Hadithi za Agano la Kale

Waamuzi 4–5

Debora Nabii Mke

Ni kiongozi aliyewasaidia Israeli kumtumaini Bwana

Debora nabii mke

Debora alikuwa nabii mke, kiongozi mwaminifu Muisraeli aliyekuwa akiongozwa na Bwana. Watu wake walikuwa wameacha kushika amri za Bwana, na Wakanaani ndio waliokuwa wakiwatawala. Baada ya miaka ishirini, Waisraeli walianza kusali kwa ajili ya msaada wa Bwana.

Waamuzi 4:1–5

Debora akisali

Bwana alisikia sala zao. Alimwambia Debora kulikusanya jeshi la Waisraeli ili kupigana dhidi ya Wakanaani.

Waamuzi 4:6

Debora akizungumza na askari

Jeshi la Wakanaani lilikuwa na askari wengi na magari ya kukokotwa na farasi. Hii ilifanya jeshi la Waisraeli kuogopa, lakini siyo Debora. Yeye alijua kuwa Bwana angewasaidia.

Waamuzi 4:3, 7

Baraka akimwomba Debora aje

Baraka alikuwa kiongozi wa jeshi la Waisraeli. Yeye hakutaka kupigana. Lakini alifikiri kwamba endapo Debora akienda na jeshi, Bwana angewalinda. Debora akakubali kwenda. Akatoa unabii kwamba mwanamke angemshinda Sisera, kiongozi wa jeshi la Wakanaani.

Waamuzi 4:8–9

Debora na jeshi wakiwa juu ya mlima

Jeshi la Waisraeli walikusanyika juu ya mlima, na Wakanaani walikusanyika katika bonde. Debora alimwambia Baraka ashuke kutoka mlimani. Akaahidi kwamba Bwana angekuwa pamoja nao.

Waamuzi 4:12–14

Magari ya kukokotwa na farasi yakafagiliwa na dhoruba

Bwana alituma mvua, na magari ya Wakanaani ya kukokotwa na farasi yakafagiliwa na maji. Wakanaani wengi wakazama katika mto, lakini Sisera akakimbia.

Waamuzi 4:15, 17; 5:4–5, 19–22

Yaeli anamwalika Sisera katika hema

Mwanamke aliyeitwa Yaeli aliishi katika hema hapo jirani. Alimwona Sisera akikimbia na akamwambia ajifiche katika hema lake. Yaeli alijua kwamba alikuwa kiongozi wa jeshi la Wakanaani na akamwua ili kwamba asiweze kuwaumiza watu zaidi.

Waamuzi 4:15–21

Debora anaangalia mji wenye amani

Unabii wa Debora ukawa kweli. Sisera alishindwa na mwanamke shujaa. Debora aliimba wimbo ili kuwasaidia Waisraeli kukumbuka jinsi Bwana alivyowaokoa. Waisraeli walishika amri na waliishi kwa amani kwa miaka 40.

Waamuzi 5:1, 24–27, 31