“Shadraka, Meshaki, na Abednego,” Hadithi za Agano la Kale (2022)
“Shadraka, Meshaki, na Abednego,” Hadithi za Agano la Kale
Danieli 1; 3
Shadraka, Meshaki, na Abednego
Jaribu hatari la imani
Mfalme Nebukadreza alitengeneza sanamu kubwa, ya dhahabu na kuwalazimisha watu wake waiabudu. Ikiwa wangekataa, wangetupwa kwenye tanuru la moto.
Marafiki wa Danieli Shadraka, Meshaki, na Abednego walimpenda Mungu na hawangemwabudu mungu wa uongo wa mfalme. Mfalme alikuwa na hasira juu yao.
Marafiki watatu walimwambia mfalme kwamba wangemwabudu Mungu pekee. Waliamini Mungu angeweza kuwalinda. Lakini hata ikiwa Asingewalinda, wangesimamia kile walichokiamini.
Mfalme alikuwa na ghadhabu juu ya Shadraka, Meshaki, na Abednego. Alisababisha watupwe ndani ya tanuru la moto. Lakini mfalme alipotazama ndani ya tanuru, alishangazwa kuona kiumbe wa mbinguni ndani ya moto akiwa na wanaume watatu. Hawakuunguzwa na moto.
Mfalme aliwaita Shadraka, Meshaki, na Abednego, na walitoka nje ya tanuru. Moto haukuwadhuru au hata kuchoma nguo zao.
Shadraka, Meshaki, na Abednego walitii amri za Mungu, hata wakati maisha yao yalipokuwa hatarini. Mfano wao ulimsaidia mfalme kumwamini Mungu.