Hadithi za Maandiko
Danieli na Ndoto ya Mfalme


“Danieli na Ndoto ya Mfalme,” Hadithi za Agano la Kale (2022)

“Danieli na Ndoto ya Mfalme,” Hadithi za Agano la Kale

Danieli 2

Danieli na Ndoto ya Mfalme

Ujumbe wa ajabu wa Mungu kwa mfalme

mfalme akiota ndoto

Mfalme wa Babeli aliota ndoto iliyomfadhaisha. Aliamuru kwamba makuhani wake na watu wenye hekima wamwambie maana ya ndoto ile.

Danieli 2:1–3

mfalme akifikiria

Mfalme hangewaambia ndoto. Alisema ikiwa makuhani na wenye hekima kweli walikuwa na nguvu, wangeweza kumwambia kuhusu ndoto na maana yake.

Danieli 2:4–9

mfalme akiwafukuza wenye hekima

Makuhani na wenye hekima walimwambia mfalme kwamba wasingeweza kutafsiri ndoto yake ikiwa asingewaambia kuhusu ndoto ile. Walisema hakuna mtu ambaye angeweza kufanya hilo. Mfalme alikasirika na kusema angewaua wote wenye hekima katika ufalme, ikiwa ni pamoja na Danieli na rafiki zake.

Danieli 2:10–13

Danieli akizungumza na askari

Wakati mlinzi wa mfalme alipokuja kuwachukua Daniel na rafiki zake, Danieli aliomba muda zaidi ili kwamba aweze kumwambia mfalme maana ya ndoto yake. Danieli alijua kwamba Mungu anafahamu na anaona kila kitu, hata ndoto. Danieli aliwaomba rafiki zake kuomba pamoja naye.

Danieli 2:14–18

Danieli akiomba

Mungu alimwonyesha Danieli ndoto ya mfalme katika ono na alimfundisha Danieli kile ilichomaanisha. Danieli alimshukuru Mungu kwa kujibu maombi yake na ya rafiki zake na kwa kuokoa maisha yao. Kisha alikwenda kumwambia mfalme maana ya ndoto.

Danieli 2:19–25

Danieli akizungumza na mfalme

Danieli alisema ndoto ya mfalme ilihusu sanamu kubwa sana ambayo iliharibiwa kwa jiwe lililokatika kutoka kwenye mlima. Sanamu iliwakilisha falme za dunia. Jiwe lililokatika kutoka kwenye mlima liliwakilisha ufalme wa Mungu ambao ungeijaza dunia. Mfalme alifahamu kwamba Danieli alizungumza ukweli.

Danieli 2:26–49