Scripture Stories
Hana


“Hana,” Hadithi za Agano la Kale (2022)

“Hana,” Hadithi za Agano la Kale

1 Samweli 1–2

Hana

Jibu la Bwana kwa mwanamke mwaminifu

Picha
Hana huku akilia anasali hekaluni

Kila mwaka, Hana na mume wake walikuwa wakisafiri kwenda kwenye nyumba ya Bwana, hekaluni. Hana hakuwa na watoto, kwa sababu hiyo alijisikia huzuni sana. Alifunga na kusali kwa ajili ya mtoto wa kiume. Hana alimwahidi Bwana kwamba kama angekuwa na mtoto wa kiume, mwanawe angekua ili amtumikie Yeye.

1 Samweli 1:1–11

Picha
Eli akizungumza na Hana

Kuhani aliyeitwa Eli alimwona Hana akilia. Alimwambia kwamba Bwana angejibu sala yake. Hana alimwamini Bwana na akawa na matumaini.

1 Samweli 1:12, 17–18

Picha
Hana pamoja na mumewe na mtoto Samweli

Mwaka huo, Hana alipata mtoto wa kiume. Alimwita jina lake Samweli.

1 Samweli 1:20–23

Picha
Hana akimleta Samweli kwa Eli hekaluni

Hana alitimiza ahadi yake kwa Bwana. Samweli alipokuwa mkubwa vya kutosha, alimchukua ili akahudumu katika nyumba ya Bwana. Alihudumu pamoja na Eli, kuhani. Hana aliendelea kumtembelea Samweli. Alimletea mavazi ambayo aliyatengeneza kwa ajili yake. Bwana alimbariki Hana na watoto wengine watano.

1 Samweli 1:24–28; 2:21

Chapisha