Scripture Stories
Mapigo ya Misri


“Mapigo ya Misri,” Hadithi za Agano la Kale (2022)

“Mapigo ya Misri,” Hadithi za Agano la Kale

Kutoka 4–5; 7–12

Mapigo ya Misri

Chaguzi za Farao dhidi ya Bwana

Picha
Musa na Haruni wakizungumza na Farao

Musa alimwamini Bwana na kurudi Misri. Musa na Haruni kaka yake walikwenda kwa Farao na kumwomba awaruhusu Waisraeli wawe huru na waondoke Misri. Farao alikasirika na kukataa. Aliwalazimisha Waisraeli kufanya kazi kwa nguvu zaidi.

Kutoka 4:10–16; 5:1–18

Picha
mto ukigeuka kuwa damu

kwa sababu Farao hakumsikiliza Bwana, Wamisri walilaaniwa kwa mapigo mabaya. Kwanza, maji yote ya Misri yalibadilika kuwa damu. Musa alimwomba Farao tena kuwaruhusu Waisraeli waondoke, lakini Farao alisema hapana.

Kutoka 7:14–25

Picha
Vyura wakiwarukia Wamisri

Kisha, Bwana alituma vyura Misri. Walikuwa kila mahala. Farao alisema angewaruhusu Waisraeli waondoke ikiwa vyura wangeondoka. Bwana alisababisha vyura waondoke, lakini Farao hakuwaruhusu Waisraeli waondoke. Kisha Bwana alituma chawa na nzi.

Kutoka 8:1–32

Picha
Wamisri na wanyama waliokufa

Kisha, mifugo wote walioko kondeni wa Wamisri walikufa, lakini hakuna mifugo ya Waisraeli iliyokufa. Kisha Wamisri walipata majipu yenye kufura kwenye miili yao.

Kutoka 9:3–12

Picha
mvua ya mawe na moto vikiiharibu Misri

Dhoruba kubwa pamoja na mvua ya mawe na moto pia vilikuja Misri. Hii ilisababisha maangamizo ya kutisha.

Kutoka 9:22–35

Picha
nzige wakila mazao

Farao bado hangewaruhusu Waisraeli waondoke. Kisha Bwana alituma nzige, na walikula chakula chote cha watu.

Kutoka 10:12–20

Picha
Farao

Kisha kulikuwa na siku tatu za giza. Wakati wa kipindi cha mapigo mengi, Farao aliahidi kuwaruhusu Waisraeli waondoke ikiwa mapigo yangekoma, lakini alidanganya kila mara.

Kutoka 10:21–23, 27

Picha
Musa na familia

Baada ya mapigo tofauti tisa, Farao bado hakuwaruhusu Waisraeli waondoke. Bwana alimwambia Musa pigo lingine baya lingekuja. Bwana aliwaongoza na kuwalinda Waisraeli walipokuwa wakisubiri uhuru wao.

Kutoka 11:4–7; 12:1–13

Chapisha