“Eliya Nabii,” Hadithi za Agano la Kale (2022)
“Eliya Nabii,” Hadithi za Agano la Kale
1 Wafalme 16–18
Eliya Nabii
Imani ya mama na miujiza ya Bwana
Ufalme wa Israeli haukuwa na mvua na maji yalikuwa yakikaribia kuisha. Mfalme Ahabu na Malkia Yezebeli hawakuwapenda manabii wa Bwana. Walisababisha hata baadhi ya manabii kuuawa. Mfalme na malkia waliomba kwa miungu kwa ajili ya mvua. Lakini nabii Eliya aliwaambia kwamba Bwana asingeleta mvua kwa miaka mingi.
1 Wafalme 16:29–33; 17:1; 18:13
Mfalme na malkia walimkasirikia Eliya. Bwana alimuonya Eliya ajifiche kwa sababu maisha yake yalikuwa hatarini.
Bwana alimuongoza Eliya kwenye kijito na kutuma ndege kumletea chakula. Lakini kwa sababu hakukuwa na mvua, kijito kilikauka na Eliya hakuwa na maji.
Bwana alimuongoza Eliya kwa mwanamke kwenye mji wa mbali. Eliya alimuomba maji na mkate. Lakini alikuwa na kiasi cha kuwatosha tu yeye na mtoto wake kwa siku moja zaidi.
Eliya alifahamu kuwa kilikuwa chakula chake cha mwisho. Alimuahidi mwanamke kwamba ikiwa atampa chakula, Bwana angetoa chakula kwa ajili ya familia yake mpaka mvua zitakaporejea.
Mwanamke alimtengenezea Eliya mkate. Kisha unga na mafuta yake viliongezeka! Kulikuwa na chakula cha kutosha kwa ajili ya Eliya na familia ya mwanamke kwa siku nyingi.
Siku moja mtoto wa yule mwanamke aliugua na kufa. Mwanamke alimwuliza Eliya kwa nini Bwana angeruhusu hili litokee kwake.
Eliya alikuwa na ukuhani. Alimbariki mtoto wa mwanamke na kumuomba Bwana kumruhusu mtoto arejee tena kwenye uhai. Mtoto alipumua tena na mwanamke alijua kwamba Eliya alikuwa nabii wa Bwana.