“Yona Nabii,” Hadithi za Agano la Kale (2021)
“Yona Nabii,” Hadithi za Agano la Kale
Yona 1–4
Yona Nabii
Kujifunza kutumaini rehema za Bwana
Yona alikuwa nabii. Bwana alimwambia awaonye watu wa Ninawi kwamba mji wao ungeangamizwa ikiwa hawatatubu.
Lakini watu wa Ninawi walikuwa maadui kwa Waisraeli. Yona hakutaka kuwahubiria. Hivyo alipanda ndani ya merikebu ili kwenda mbali na Ninawi.
Wakati Yona akiwa ndani ya merikebu, tufani kubwa ilikuja. Watu kwenye merikebu walihofia maisha yao. Walimsihi Yona amuombe Bwana ili awaokoe.
Yona alijua kwamba Bwana alituma tufani kwa sababu alikuwa akikimbia kile Bwana alichomuomba kufanya. Yona alitaka kuwaokoa watu waliokuwa ndani ya merikebu. Alisema ikiwa wangemtupa baharini, tufani ingetulia.
Mabaharia hawakutaka kumtupa Yona baharini. Walijaribu kuipeleka merikebu ufukoni, lakini tufani ilikuwa kali. Hatimaye, walimtupa Yona baharini.
Tufani ilikoma. Lakini hapo Yona alikuwa amemezwa na samaki mkubwa.
Yona alikuwa ndani ya tumbo la samaki kwa siku tatu mchana na usiku. Wakati huo, Yona aliomba na kutubu. Alitaka kufanya kile kilicho sahihi na kumsikiliza Bwana. Bwana alisikia maombi ya Yona na akamfanya samaki amtapike Yona kwenye nchi kavu.
Bwana akamwambia tena Yona kuwahubiria watu wa Ninawi. Safari hii Yona alitii. Alienda Ninawi na kuwaambia watu watubu la sivyo Bwana angeangamiza mji wao. Mfalme na watu wake walitubu. Bwana aliwasamehe na hakuiangamiza Ninawi.
Lakini Yona alivunjika moyo kwamba watu hawajaangamizwa. Hakudhani kwamba walistahili kusamehewa.
Ili kumfundisha Yona somo, Bwana aliotesha mti ili kumpa Yona kivuli kutokana na jua. Kisha mti ukafa, na Yona akahisi vibaya kwa ule mti.
Bwana alikuwa akimfundisha Yona somo kuhusu watoto Wake. Yona alijifunza kwamba alipaswa kuwa na huzuni wakati watu hawataki kutubu na kwamba anapaswa kuwa na furaha pale wanapotubu.