Hadithi za Maandiko
Rahabu na Wapelelezi


“Rahabu na Wapelelezi,” Hadithi za Agano la Kale (2022)

“Rahabu na Wapelelezi,” Hadithi za Agano la Kale

Yoshua 26

Rahabu na Wapelelezi

Uchaguzi ambao unaiokoa familia

watu wa mjini wakiangalia kutoka mbali

Mwanamke anayeitwa Rahabu aliishi Yeriko kabla haijatekwa na Waisraeli. Yeye alisikia kwamba Bwana aliyagawanya maji ya Bahari ya Shamu pande mbili kwa ajili ya Waisraeli. Rahabu alijua Bwana angewasaidia Waisraeli kupigana dhidi ya mji wake. Watu huko Yeriko walikuwa waovu.

Yoshua 2:9–11

wapelelezi wakijificha wasionekana na walinzi

Nabii Yoshua aliongoza jeshi la Waisraeli. Aliwatuma wapelelezi wawili ndani ya Yeriko. Lakini wapelelezi wale walionekana, na mfalme wa Yeriko akawatuma askari kuwakamata.

Yoshua 2:1–3

Rahabu akiongea na wapelelezi

Wapelelezi walifika nyumbani kwa Rahabu. Rahabu alikubali kuwasaidia wale wapelelezi, hivyo akawaficha juu ya dari ya nyumba yake.

Yoshua 2:4–6

Rahabu akiwaficha wapelelezi

Watu wa mfalme waliipekua nyumba ya Rahabu lakini hawakuweza kuwapata wale wapelelezi. Baada ya kuondoka, Rahabu aliwaomba wale kuilinda familia yake wakati jeshi lao litakapokuja kupigana na Yeriko. Wale wapelelezi wakaahidi kuwa familia yake ingekuwa salama. Kisha Rahabu akarusha kamba nje ya dirisha lake kwa ajili ya wale wapelelezi kutoroka.

Yoshua 2:3, 12–15

Rahabu na familia wanatoroka Yeriko

Wapelelezi walirudi kwa nabii Yoshua na kumwambia jeshi la Waisraeli lisimdhuru mtu ye yote katika nyumba ya Rahabu. Baadaye, Waisraeli walipoipiga Yeriko, walitunza ahadi yao kwa Rahabu. Ujasiri wa Rahabu uliokoa familia yake Familia yake iliungana na watu wa Bwana.

Yoshua 2:23; 6:25; Waebrania 11:31