Hadithi za Maandiko
Uumbaji wa Dunia


“Uumbaji wa Dunia,” Hadithi za Agano la Kale (2022)

“Uumbaji wa Dunia,” Hadithi za Agano la Kale

Mwanzo 1–2; Musa 1–3; Ibrahimu 3–5

Uumbaji wa Dunia

Nyumba nzuri kwa ajili ya watoto wa Baba wa Mbinguni

Mungu na Bwana wakiumba ulimwengu

Mungu Baba yetu wa Mbinguni aliwasilisha mpango wa wokovu mbinguni. Sote tulishangilia kwa furaha! Tungeweza kuja duniani ili kupokea mwili wa nyama na mifupa. Wakati tukiwa duniani, tungejifunza kumfuata Mwana wa Mungu, Bwana Yesu Kristo. Bwana aliumba dunia kwa kufuata maelekezo ya Mungu.

Mwanzo 1:1; Ayubu 38:4–7; Musa 1:32–33; 2:1; Ibrahimu 3:22–27

sayari katika anga

Mnamo siku ya kwanza, Bwana alitenganisha nuru kutoka kwenye giza. Aliita nuru mchana na giza usiku.

Mwanzo 1:3–5; Musa 2:3–5; Ibrahimu 4:1–5

mawingu na bahari

Mnamo siku ya pili, Aliyagawa maji kati ya mawingu juu ya anga na bahari juu ya dunia.

Mwanzo 1:6–8; Musa 2:6–8; Ibrahimu 4:6–8

msitu kando ya bahari

Mnamo siku ya tatu, Bwana alitengeneza bahari kubwa na nchi kavu. Aliyaita maji bahari na nchi kavu dunia. Aliifanya dunia iwe ya kupendeza kwa maua, matunda, mimea na miti.

Mwanzo 1:9–13; Musa 2:9–13; Ibrahimu 4:9–13

mwonekano wa usiku na mchana

Mnamo siku ya nne, Yeye aliumba jua ili liangaze wakati wa mchana. Kisha Akaumba mwezi na nyota ili ziangaze usiku.

Mwanzo 1:14–19; Musa 2:14–19; Ibrahimu 4:14–19

viumbe wa baharini

Mnamo siku ya tano, Bwana alitengeneza samaki ndani ya bahari na ndege angani. Aliwabariki viumbe ili waongezeke na akawabariki samaki ili wayajaze maji.

Mwanzo 1:20–23; Musa 2:20–23; Ibrahimu 4:20–23

wanyama wa msituni

Mnamo siku ya sita, Yeye aliumba wanyama juu ya ardhi, baadhi ambao walitembea na baadhi ambao walitambaa.

Mwanzo 1:24–25; Musa 2:24–25; Ibrahimu 4:24–25

Adamu na Hawa katika Bustani ya Edeni

Baba wa Mbinguni pamoja na Bwana walishuka chini duniani mnamo siku ya sita. Mwanamume na mwanamke waliumbwa kwa mfano wa Mungu. Baba wa Mbinguni aliwaambia watunzane na wapate watoto. Mwanamume na mwanamke pia waliaminiwa kwenye kutunza ardhi na wanyama.

Mwanzo 1:26–27; Musa 2:26–27; Ibrahimu 4:26–31; 5:7–8

Adamu na Hawa wakiwatazama wanyama

Baba wa Mbinguni alikuwa na furaha kwa kila kitu Walichokiumba. Mnamo siku ya saba, Walipumzika kutokana na kazi Zao zote. Dunia ilikuwa ya kupendeza na iliyojaa uhai.

Mwanzo 2:1–3; Musa 3:1–3; Ibrahimu 5:1–3