“Henoko Nabii,” Hadithi za Agano la Kale (2022)
“Henoko Nabii,” Hadithi za Agano la Kale
Mwanzo 5; Musa 6–7
Henoko Nabii
Jinsi imani katika Bwana ilivyookoa mji
Bwana Yesu Kristo alimuomba Henoko awaambie watu watubu. Lakini Henoko alifikiri asingeweza kuzungumza vizuri. Aliogopa kwamba watu wasingemsikiliza.
Bwana aliahidi kumuimarisha na kumlinda Henoko ingawa baadhi ya watu hawakupenda kile ambacho Henoko alifundisha.
Ahadi ya Bwana ilimpa Henoko ujasiri. Henoko alimtii Bwana na kuwafundisha watu kwa nguvu. Alifundisha kuhusu Yesu Kristo, toba, ubatizo na Roho Mtakatifu. Baadhi ya watu walimwamini Henoko na walitaka kumfuata Bwana.
Henoko alikuwa na mamlaka ya kubatiza kutoka kwa Mungu. Watu wote waliomwamini Henoko walibatizwa na kusogea karibu na Bwana. Hakukuwa na mtu masikini kwa sababu walijaliana. Waliitwa Sayuni kwa sababu waliishi pamoja katika upendo na haki.
Siku moja Bwana alimwonyesha Henoko ono la mambo yote ambayo yangetokea duniani. Henoko aliona maisha, kifo na Ufufuko wa Yesu Kristo. Henoko alijifunza kwamba katika siku za mwisho injili ingerejeshwa. Aliona pia Ujio wa Pili wa Yesu Kristo.
Hatimaye, watu wote katika mji wa Sayuni walimwamini Henoko na wakatubu. Kwa sababu walijaliana na kuishi kwa amani, Bwana aliwachukua wakaishi pamoja Naye.