Scripture Stories
Ibrahimu na Sara


“Ibrahimu na Sara,” Hadithi za Agano la Kale (2021)

“Ibrahimu na Sara,” Hadithi za Agano la Kale

Mwanzo 11–15; 17; Ibrahimu 1–2

Ibrahimu na Sara

Ahadi ya kubariki familia ya mwanadamu

Picha
malaika anamwokoa Ibrahimu kutoka kwa kuhani

Ibrahimu aliishi katika nchi ya Uru. Makuhani waovu wa huko walitaka kumtoa sadaka kwa sanamu zao. Ibrahimu aliomba na Bwana alimwokoa.

Ibrahimu 1:1–20

Picha
Ibrahimu na Sara wakisafiri kwa ngamia

Kisha Bwana akamwamuru Ibrahimu na mke wake Sara kuondoka Uru na kusafiri mpaka kwenye nchi ya mbali sana. Aliahidi kuwabariki katika safari yao.

Mwanzo 12:1–3; Ibrahimu 2:2–4

Picha
Ibrahimu na Sara wakiwaangalia kondoo

Ibrahimu na Sara walimwamini Bwana na kuondoka Uru. Lakini walihisi huzuni kwa sababu hawakuweza kupata mtoto. Bwana aliwapa faraja. Aliwaahidi kwamba wangepata mtoto.

Mwanzo 11:30–31; 15:1–6; 17:2–16; Ibrahimu 2:6–9

Picha
Mungu anamtokea Ibrahimu

Ibrahimu aliomba kwa Bwana ili kujifunza zaidi kumhusu Yeye. Bwana alimtembelea Ibrahimu na kujitambulisha Yeye Mwenyewe kuwa ni Yehova. Yehova alifanya agano na Ibrahimu. Aliahidi kwamba Ibrahimu angepata ukuhani. Yehova pia aliahidi kwamba kupitia familia ya Ibrahimu, familia zote za dunia zingebarikiwa.

Ibrahimu 2:6–11

Picha
Ibrahimu na Sara wakisafiri kwa ngamia

Ibrahimu na Sara walipokuwa wakisafiri, walihitaji kupata chakula. Walijaribu kuishi katika nchi iliyoitwa Kanaani. Hapakuwa na chakula huko, hivyo waliamua kwenda Misri. Lakini kuishi Misri ilikuwa hatari kwao.

Mwanzo 12:10–20; Ibrahimu 2:21–25

Picha
Ibrahimu na Sara wakiwaangalia wanyama

Ibrahimu na Sara waliondoka Misri na kurudi kuishi Kanaani. Walibeba chakula na wanyama kutoka Misri pamoja nao. Kanaani ilikuwa sehemu ya ardhi ambayo Bwana aliwaahidi.

Mwanzo 13:1–4, 12; Ibrahimu 2:19

Picha
Melkizedeki akizungumza na Ibrahimu na Sara

Bwana pia alitunza ahadi Yake kwamba Ibrahimu angepokea ukuhani. Siku moja Ibrahimu na Sara walikutana na mfalme mwenye haki aliyeitwa Melkizedeki. Ibrahimu alilipa zaka kwake.

Mwanzo 14:18–24; Alma 13:15

Picha
Melkizedeki akimbariki Ibrahimu

Ibrahimu alipokea ukuhani kutoka kwa Melkizedeki. Huu ulikuwa ukuhani sawa na ule ambao manabii Adamu na Nuhu walikuwa wamepokea.

Tafsiri ya Joseph Smith, Mwanzo 14:36–40; Ibrahimu 1:2–4; Mafundisho na Maagano 84:14

Picha
Ibrahimu na Sara

Ibrahimu na Sara walikuwa na furaha huko Kanaani, lakini bado walikuwa na hofu kwa sababu hawakuwa na mtoto. Iliwapasa kuamini ahadi ya Bwana kwamba siku moja familia yao ingekua na kubariki dunia yote.

Mwanzo 13:12; 15:3–6

Chapisha