Scripture Stories
Elisha na Jeshi la Bwana


“Elisha na Jeshi la Bwana,” Hadithi za Agano la Kale (2022)

“Elisha na Jeshi la Bwana,” Hadithi za Agano la Kale

2 Wafalme 6

Elisha na Jeshi la Bwana

Magari ya moto ya Bwana

Picha
askari wakiuzunguka mji

Washamu hawakuwapenda Waisraeli. Mfalme wa Shamu alituma jeshi ili kumkamata Elisha nabii. Usiku, jeshi liliuzingira mji ambamo Elisha alikuwako.

2 Wafalme 6:8–14

Picha
Elisha na mtumishi wake wakiliangalia jeshi la Shamu

Mtumishi kijana wa Elisha aliamka na kuliona jeshi la Shamu. Alimuuliza Elisha wanapaswa kufanya nini. Elisha alimwambia yule kijana asiogope. Akamwambia kwamba jeshi linalopigana kwa ajili yao ni kubwa zaidi ya jeshi linalopigana dhidi yao.

2 Wafalme 6:15–16

Picha
Jeshi la mbinguni pamoja na magari ya moto

Elisha akamwomba Bwana amwonyeshe kijana kile alichokiona Elisha. Bwana akamwonyesha jeshi la mbinguni pampoja na farasi na magari ya moto ya kuwalinda wao. Jeshi la Shamu lilitiwa upofu kwa uweza wa Mungu. Hawakupigana tena na Waisraeli.

2 Wafalme 6:17–23

Chapisha