Hadithi za Maandiko
Ibrahimu na Isaka


“Ibrahimu na Isaka,” Hadithi za Agano la Kale (2022)

“Ibrahimu na Isaka,” Hadithi za Agano la Kale

Mwanzo 17; 21–22

Ibrahimu na Isaka

Baba, mwana, na sadaka

Ibrahimu, Sara na mtoto

Ibrahimu na Sara walipata mtoto wa kiume, kama vile Bwana alivyoahidi. Walimpa jina Isaka.

Mwanzo 17:9; 21:1–3

Ibrahimu akimfundisha Isaka

Walimpenda Isaka. Walimfunza kuchagua mema na kumwamini Bwana.

Mwanzo 21:8

Sara na Ibrahimu wakimtazama Isaka

Bwana aliwaahidi Ibrahimu na Sara kwamba kupitia Isaka familia yao ingekua ili kubariki dunia yote. Lakini siku moja Bwana alimwambia Ibrahimu kumchukua Isaka kwenda Mlima Moria na kumtoa Isaka kama sadaka ya kuteketezwa.

Mwanzo 17:1–8; 22:1–2

Ibrahimu na Isaka wakisafiri

Wakiwa njiani kuelekea mlimani, Isaka aliuliza mwana-kondoo wa sadaka ya kuteketezwa alikuwa wapi. Ibrahimu alisema Bwana angetoa mwana-kondoo.

Mwanzo 22:4–8

Ibrahimu na Isaka wakijenga madhabahu

Juu ya Mlima Moria, Ibrahimu alijenga madhabahu na kuweka kuni juu yake.

Mwanzo 22:8–9

Ibrahimu akijiandaa kumtoa Isaka kama sadaka ya kuteketezwa

Kama Bwana alivyoamuru, Ibrahimu alimwomba Isaka kulala juu ya madhabahu. Isaka alimwamini Ibrahimu kama vile Mwokozi Yesu Kristo alivyomwamini Baba Yake.

Mwanzo 22:9

malaika akiwatokea Ibrahimu na Isaka

Wakati Ibrahimu alipokuwa karibu kumtoa Isaka kama sadaka ya kuteketezwa, malaika wa Bwana alimzuia. Ibrahimu alionyesha imani yake kwa Bwana. Ibrahimu alijua kwamba daima angemfuata Bwana.

Mwanzo 22:10–12

kondoo dume amenaswa kwenye kichaka

Ibrahimu alitazama na kumwona kondoo dume amenaswa kwenye kichaka. Bwana alimtoa kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa.

Mwanzo 22:13

Ibrahimu na Isaka wakitazama juu angani

Ibrahimu na Isaka walijifunza kuhusu jinsi ambavyo Baba wa Mbinguni angemtoa Mwana Wake Yesu Kristo kama sadaka. Bwana Yesu Kristo alimwamini Ibrahimu kwa sababu alitii. Ibrahimu aliamini ahadi ya Bwana kwamba siku moja familia yake ingekua kupita idadi ya nyota za angani.

Mwanzo 22:17–18; Yakobo 4:5