“Danieli na Rafiki Zake,” Hadithi za Agano la Kale (2022)
“Danieli na Rafiki Zake,” Hadithi za Agano la Kale
Danieli 1
Danieli na Rafiki Zake
Kukataa kula chakula cha mfalme
Ufalme wa Babeli uliiteka Yerusalemu. Waliwachukua baadhi ya vijana werevu na wenye nguvu kutoka kwa familia zao huko Yerusalemu na kuwaleta Babeli ili wamtumikie mfalme.
Danieli na rafiki zake walikuwa kati ya vijana hawa. Walichaguliwa kutumikia ndani ya jumba la mfalme na kuwa watu wake wenye hekima.
Mfalme aliwapa Danieli na rafiki zake chakula na divai. Lakini wasingekula chakula cha mfalme au kunywa divai. Ilikuwa kinyume na amri za Mungu.
Hii ilimfanya mtumishi wa mfalme ahofie maisha yake. Aliwahudumia Danieli na rafiki zake, na alidhani ikiwa wangekataa chakula cha mfalme, wangekuwa dhaifu kuliko vijana wengine. Ndipo mfalme angekuwa na hasira na kumuua mtumishi yule.
Lakini Danieli alimtumaini Bwana na alitaka kutii amri zake. Danieli alimuomba mtumishi awapatie maji na nafaka kwa siku 10 na kisha kulinganisha afya yao na afya ya vijana wengine. Mtumishi alikubali.
Baada ya siku 10, Danieli na rafiki zake walikuwa wenye afya kuliko vijana wengine wote. Danieli na rafiki zake walifuata amri za Mungu na Mungu aliwafanya wawe watu wenye hekima kuliko wengine wote kwenye jumba la mfalme.