Scripture Stories
Yakobo na Familia Yake


“Yakobo na Familia Yake,” Hadithi za Agano la Kale (2022)

“Yakobo na Familia Yake,” Hadithi za Agano la Kale

Mwanzo 27–33

Yakobo na Familia Yake

Jinsi Bwana anavyotunza ahadi Zake

Picha
Yakobo akitembea na punda

Yakobo aliondoka nyumbani kwake ili kumuepuka kaka yake Esau aliyekuwa na hasira. Baba yake Yakobo alimbariki ili apate na kuoa mwanamke aliyempenda Bwana na kutii amri Zake.

Mwanzo 27:42–46; 28:1–5

Picha
Yesu Kristo akimtokea Yakobo

Wakati Yakobo akisafiri, Bwana alimtokea katika ono. Aliahidi kuwa na Yakobo daima. Yakobo aliahidi kumpa Bwana moja ya kumi ya vyote alivyopokea.

Mwanzo 28:10–16, 20–22

Picha
Yesu Kristo akizungumza na Yakobo

Bwana alimwahidi Yakobo kwamba angekuwa na watoto wengi. Kupitia watoto wa Yakobo, familia za duniani zingebarikiwa kumjua Mwokozi. Familia ya Yakobo katika siku za mwisho inaitwa nyumba ya Israeli.

Mwanzo 28:3–4, 14; 1 Nefi 10:14

Picha
Yakobo na Raheli

Yakobo alisafiri mpaka nchi iliyoitwa Harani. Huko alimpenda mwanamke mwadilifu aliyeitwa Raheli.

Mwanzo 27:43; 29:9–20

Picha
Yakobo akifanya kazi shambani

Yakobo alikubali kufanya kazi kwa Labani, baba yake Raheli, kwa miaka saba ikiwa Labani angemruhusu amuoe Raheli. Labani alikubali. Yakobo alifanya kazi kwa miaka saba.

Mwanzo 29:21–27

Picha
Yakobo, Raheli na Lea

Lakini Labani alitaka Lea, binti yake mkubwa, aolewe kwanza. Wakati wa ndoa, Labani alimwekea mtego Yakobo na akamfanya amuoe Lea. Lakini Yakobo alimpenda Raheli. Aliahidi kufanya kazi miaka mingine saba ikiwa angeweza kumuoa Raheli pia. Labani alikubali, na familia ya Yakobo ilianza kukua.

Mwanzo 29:28–35; 30:3–13, 17–24; Yakobo 2:27–30

Picha
Yakobo akisafiri na familia

Labani hakumlipa Yakobo inavyostahili. Lakini Bwana alimbariki Yakobo kwa wanyama wengi na akamwambia Yakobo arudi nyumbani.

Mwanzo 30:31, 43; 31:1–7, 17–18

Picha
Yakobo

Akiwa njiani kurejea nyumbani, Yakobo alijua kwamba kaka yake Esau na wanaume 400 walikuwa wakija kukutana naye.

Mwanzo 32:3–6

Picha
Yakobo akiificha familia

Yakobo alifikiri kwamba Esau bado alikuwa anamchukia. Yakobo alihofia usalama wa familia yake, hivyo aliwapeleka mahali salama na kumwomba Mungu.

Mwanzo 32:7–24

Picha
Yesu Kristo akizungumza na Yakobo

Yakobo aliomba usiku kucha na mpaka kufikia alfajiri Bwana alimtembelea Yakobo na kumbariki. Bwana alimwambia Yakobo kwamba angekuwa kiongozi mkubwa kwa wengi. Bwana alibadilisha jina la Yakobo kuwa Israeli.

Mwanzo 32:24–30

Picha
Esau anakutana na Yakobo

Punde Esau na watu wake waliwapata Yakobo na familia yake. Esau hakuwa tena na hasira na Yakobo. Alikimbia kukutana na Yakobo na kumkumbatia. Alifurahi kukutana na Yakobo pamoja na familia yake. Yakobo pia alikuwa na furaha kumuona tena Esau.

Mwanzo 33:1–7

Picha
Yakobo na Esau wakiitazama familia

Bwana alitimiza ahadi Zake kwa Yakobo katika kipindi chote cha maisha yake. Yakobo alifika nyumbani akiwa na familia yake na aliishi huko. Tangu hapo na kuendelea, Yakobo aliitwa Israeli, na familia yake iliitwa Waisraeli. Aliendelea kutii amri na kumwabudu Bwana.

Mwanzo 33:17–20

Chapisha