Hadithi za Maandiko
Yeremia Nabii


“Yeremia Nabii,” Hadithi za Agano la Kale (2022)

“Yeremia Nabii,” Hadithi za Agano la Kale

Yeremia 1–52

Yeremia Nabii

Aliitwa kabla ya kuzaliwa kwake

Yeremia Aliyeitwa kama nabii

Yeremia aliishi Yerusalemu wakati akiwa kijana. Siku moja Bwana alikuja kwa Yeremia na akamwita kuwa nabii. Bwana alimwambia Yeremia kwamba alichaguliwa kuwa nabii kabla hajazaliwa. Bwana alijua ya kwamba maisha ya Yeremia yangekuwa magumu. Lakini Yeye alimuahidi Yeremia kwamba daima angelikuwa pamoja naye.

Yeremia 1:1–10

Yeremia Anawaonya watu

Watu katika Yerusalemu hawakutunza ahadi zao kwa Bwana. Kwa sababu ya uovu wao, Yeremia aliwaonya watu kwamba watu hao wangeshindwa vita. Bwana aliwaambia kwamba kama watashika kitakatifu siku ya Sabato, mji wa Yerusalemu haungeangamizwa. Lakini watu hawakusikiliza.

Yeremia 6:1–19; 8–9; 17:21–27

Yeremia akiwa gerezani

Yeremia aliwafundisha watu kwa miaka mingi. Lakini hawakutubu. Badala yake, walimuumiza Yeremia na kumtupa gerezani.

Yeremia 20:2; 26:8–9; 37:15–18; 38:6

Yeremia akiangalia Yerusalemu ikiangamizwa

Yeremia aliwapenda watu wa huko. Alilia kwa sababu ya dhambi zao. Kama vile tu alivyosema, Yerusalemu ikaangamizwa, na watu wakakamatwa mateka.

Yeremia 9:1–8; 25:9–12; 52:1–10

Yeremia anaandika unabii

Yeremia alichukuliwa kwenda Misri. Bwana alimwambia aandike unabii wake. Yeremia alimtii Bwana hata pale mambo yalipokuwa magumu Yeye aliendelea kuwaambia watu wake kutunza ahadi zao.

Yeremia 36:1–2, 27–32