Hadithi za Maandiko
Yoshua Nabii


“Yoshua Nabii,” Hadithi za Agano la Kale (2022)

“Yoshua Nabii,” Hadithi za Agano la Kale

Kumbukumbu la Torati 10; 3134; Yoshua 1; 3–6; 10–11; 2124

Yoshua Nabii

Jaribio la mwisho kabla ya kuingia nchi ya ahadi

Yoshua akisali

Bwana alimwita Yoshua kuwa nabii mpya baada ya nabii Musa kutwaliwa mbinguni. Wakati Waisraeli walipopiga kambi karibu na Mto Yordani, Bwana alisema ulikuwa ni wakati mwafaka kwa wao kuingia katika nchi ya ahadi.

Kumbukumbu la Torati 34:1–9; Yoshua 1:1–4; Alma 45:19

watu waovu katika Kanaani

Nchi ya ahadi ilikuwa katika Kanaani, lakini watu waovu waliishi huko. Bwana alimwambia Yoshua awe hodari na moyo wa ushujaa. Pamoja na msaada wa Bwana, Waisraeli waliweza kushinda vita na kupata nchi ya Kanaani.

Yoshua 1:1–9

Waisraeli kwenye Mto Yordani

Yoshua akakusanya jeshi. Bwana aliwaambia wazibebe zile mbao za mawe ya Amri Kumi na maandiko mengine matakatifu. Makuhani wakabeba vitu hivi vitakatifu katika boksi lililoitwa sanduku la agano. Kisha jeshi likajiandaa kuvuka Mto Yordani. Mto ulikuwa na kina kirefu na maji yaliyokwenda kasi sana.

Kumbukumbu la Torati 10:5; 31:25–26; Yoshua 1:10–11; 3:1–11

Yoshua nabii

Yoshua aliwaahidi Waisraeli kwamba Bwana angewasaidia kuvuka ule mto.

Yoshua 3:10–13

maji yaligawanyika miguuni

Yoshua aliwaambia makuhani walibebe lile sanduku la agano na watembee kuingia majini. Mara wale makuhani walipokanyaga ndani ya mto, maji yaligawanyika.

Yoshua 3:12–17

Waisraeli wakibeba sanduku la agano ndani ya mto mkavu, wengine wakikusanya mawe

Waisraeli wakavuka mto kwenye nchi kavu. Yoshua aliwataka Waisraeli kuchukua mawe 12 kutoka kwenye nchi kavu ndani ya mto. Aliyapanga yale mawe ili yawakumbushe Waisraeli juu ya muujiza wa Bwana siku ile.

Yoshua 3:17; 4:1–24

Waisraeli wakitembea kuelekea mjini

Yoshua aliongoza jeshi la Waisraeli kwenye nchi ya ahadi. Walifika kwenye mji ulioitwa Yeriko. Mji ulikuwa imara sana na wenye kuta ndefu. Bwana alimwambia Yoshua jinsi ya kuiteka Yeriko. Waisraeli wanapaswa watembee kuuzunguka mji kila siku kwa siku sita. Yoshua alimtii Bwana.

Yoshua 5:13–15; 6:1–5

makuhani wakilibeba sanduku la agano, wengine wakipiga mabaragumu

Yoshua aliwaambia makuhani walibebe sanduku la agano mbele ya Waisraeli. Kila siku, jeshi lilitembea kuzunguka Yeriko, na makuhani saba wakipuliza mabaragumu. Waisraeli wengine wote walikuwa wamenyamaza.

Yoshua 6:6–14

Waisraeli wanapiga kelele, ukuta unaanguka

Katika siku ya saba, jeshi lilitembea kuzunguka Yeriko mara saba. Makuhani walipopuliza mabaragumu yao, Yoshua akawaambia Waisraeli wapige kelele kwa sauti kubwa. Ghafla ukuta wa Yeriko ukaanguka chini, na jeshi la Yoshua likautwaa mji.

Yoshua 6:15– 16, 20

Yoshua akiongea na watu jijini

Bwana aliwasaidia Waisraeli, kama alivyoahidi. Jeshi la Waisraeli liliendelea kuiteka nchi ya Kanaani, na Waisraeli wakaanza kuishi humo. Yoshua aliwakumbusha juu ya miujiza na ahadi za Bwana. Aliwaomba Waisraeli kuchagua kumtumikia Bwana.

Yoshua 10:42; 11:23; 21:43–45; 24:15