Scripture Stories
Jeshi la Gidioni


“Jeshi la Gidioni,” Hadithi za Agano la Kale (2022)

“Jeshi la Gidioni,” Hadithi za Agano la Kale

Waamuzi 6–7

Jeshi la Gidioni

Kutumaini Bwana katika vita

Picha
Wamidiani wakiiba chakula

Watu wa Israeli walibarikiwa kwa miaka mingi. Lakini baadaye walichagua kutomtii Bwana. Ili kuwasaidia wamkumbuke Yeye, Bwana aliwaruhusu maadui zao Wamidiani wachukue chakula na wanyama wao. Waisraeli wakatabika na njaa, hivyo wakamkumbuka Bwana na wakamwomba msaada.

Waamuzi 6:1–7

Picha
malaika akizungumza na Gidioni

Gidioni alikuwa mtu aliyetoka kwenye familia maskini. Bwana alimtuma malaika amwite ili kuiweka huru Israeli. Gidioni alijiuliza kwa nini Bwana amemchagua yeye.

Waamuzi 6:11–15

Picha
watu walimkasirikia Gidioni ikifuatia kuangamizwa kwa sanamu

Bwana alimwambia Gidioni avunje maeneo ambayo Waisraeli waliabudu miungu wa uongo. Gidioni alipotii, watu walikasirika.

Waamuzi 6:25–27

Picha
Baba yake Gidioni alimlinda kutokana na watu wenye hasira

Waisraeli walitaka kumuua Gidioni. Lakini baba wa Gidioni aliwashawishi wasimuumize. Gidioni aliwekwa salama.

Waamuzi 6:28–32

Picha
Gidioni akisali

Gidioni hakufikiria kuwa angeliweza kuifanya huru Israeli. Palikuwa na askari zaidi ya 135,000 katika jeshi la Wamidiani. Lakini Bwana alimpa Gidioni hekima na nguvu.

Waamuzi 6:13–16; 8:10

Picha
askari wakiondoka jeshini

Bwana alitaka Waisraeli wajue kwamba wangeweza kushinda kwa nguvu zake Yeye. Ingawa Israeli ilikuwa na askari 32,000, Bwana alimwambia Gidioni kumrudisha nyumbani askari ye yote walioogopa. Baada ya 22,000 kurudi nyumbani, Waisraeli walibakiwa na askari 10,000.

Waamuzi 7:2–3

Picha
askari wakinywa kutoka majini

Bwana alisema kwamba 10,000 bado ni askari wengi sana. Alimwambia Gidioni alipeleke jeshi kwenye maji. Wale waliokunywa maji kutoka majini kwa vinywa vyao watarejeshwa nyumbani. Wale waliotumia mikono yao kunywa maji wangeweza kubaki. Sasa ni wanaume 300 tu ndio waliobakia.

Waamuzi 7:4–7

Picha
Askari wa Waisraeli wenye mabaragumu na taa wameizunguka kambi ya Wamidiani.

Mwishowe, Waisraeli walikuwa tayari kupigana. Bwana alimwonyesha Gidioni jinsi ya kuwashinda Wamidiani. Gidioni aliliambia jeshi lake kutumia mabaragumu na taa ili kuwatishia. Zile kelele na mianga iliwachanganya sana Wamidiani kiasi kwamba walianza kupigana wao kwa wao. Kisha wakalia na kukimbia.

Waamuzi 7:16–22

Picha
Gidioni akiwaongoza askari

Kwa sababu Gidioni alimtumaini Bwana, Waisraeli walilipiga jeshi kubwa la Wamidiani kwa askari 300 tu. Bwana ndiye aliyewafanya huru watu wa Israeli.

Waamuzi 7:23–25

Chapisha