Hadithi za Maandiko
Mfalme Daudi


“Mfalme Daudi,” Hadithi za Agano la Kale (2022)

“Mfalme Daudi,” Hadithi za Agano la Kale

1 Samweli 18–19; 31; 2 Samweli 1; 5; 11–12

Mfalme Daudi

Mapambano ya mfalme

Mfalme Sauli na Daudi wakitazama mji

Mfalme Sauli, mfalme wa Israeli, alivutiwa na ushindi wa Daudi kwa Goliathi. Sauli alimfanya Daudi kuwa kiongozi wa majeshi yake.

1 Samweli 18:5

Daudi

Daudi alimpenda Bwana na daima alitaka kufanya yaliyo sahihi. Watu wa Israeli walimpenda Daudi.

1 Samweli 18:6–7

Sauli akiwa amekasirika

Sauli alipata wivu na kujaribu kumuua Daudi. Lakini Daudi alimfuata Bwana, na Bwana alimlinda dhidi ya Sauli.

1 Samweli 18:6–16; 19:1

Mazishi ya Muisraeli

Waisraeli walipigana kwenye vita vingi. Siku moja Sauli na wana wake walikufa vitani. Daudi aliwapenda na alikuwa na huzuni nyingi alipojua kuhusu vifo vyao. Sasa Waisraeli walihitaji mfalme mpya. Bwana alimchagua Daudi kuwa mfalme. Watu walikuwa na furaha.

1 Samweli 31:2–6; 2 Samweli 1:11–12; 5:1–5

Daudi akiongoza jeshi

Bwana alimbariki Mfalme Daudi na alimwongoza. Kwa msaada wa Bwana, jeshi la Daudi liliwashinda maadui zao.

2 Samweli 5:6–10, 17–25

Daudi akila zabibu

Siku moja wakati ambapo Daudi alipaswa kwenda vitani, yeye alibaki nyumbani. Alimwona mwanamke mrembo. Jina la mwanamke lilikuwa Bath-sheba na Daudi alitaka kumuoa. Lakini alikuwa tayari ameolewa na Uria, askari katika jeshi la Daudi.

2 Samweli 11:1–3

Daudi akizungumza na Uria

Daudi alitaka kumuoa Bath-sheba, hivyo alimpeleka Uria, mume wa Bath-sheba kwenye vita hatari ili kwamba angeuawa.

2 Samweli 11:4–17

Daudi na Bath-sheba

Punde Daudi aligundua kwamba Uria alikufa vitani. Daudi aliwatuma watumishi wake kumleta Bath-sheba nyumbani kwake na akamuoa.

2 Samweli 11:24, 26–27

Nathani akizungumza na Daudi

Lakini Bwana hakufurahishwa kwa kile Daudi alichofanya. Bwana alimtuma Nathani, nabii, kumwambia Daudi jinsi dhambi yake ilivyokuwa kubwa. Daudi alihuzunika kwa kile alichokuwa amefanya kwa Uria na Bath-sheba. Aliomba na kufunga kwa ajili ya msamaha kutoka kwa Bwana.

2 Samweli 11:27; 12:1–13