Scripture Stories
Elisha Nabii


“Elisha Nabii,” Hadithi za Agano la Kale (2022)

“Elisha Nabii,” Hadithi za Agano la Kale

2 Wafalme 2; 4

Elisha Nabii

Miujiza ya Bwana

Picha
Eliya akizungumza na Elisha

Kupitia nabii Eliya, Bwana alimuandaa Elisha kuwa nabii anayefuata. Kisha Bwana alimchukua Eliya mbinguni.

2 Wafalme 2:1–15

Picha
mwanamke akimimina mafuta

Bwana alimsaidia Elisha kutenda miujiza mingi. Elisha wakati mmoja alibariki mafuta ya mwanamke masikini yakajaza vyombo vingi. Kisha mwanamke aliuza mafuta ili kulipa madeni yake.

2 Wafalme 4:1–7

Picha
Elisha akizungumza na familia

Wakati mwingine, mwanamke mwaminifu alimhudumia Elisha na alikuwa mkarimu kwake. Elisha alimwuliza ni nini angeweza kufanya ili kumhudumia. Mwanamke alitumainia mtoto. Elisha alimbariki yeye na mume wake ili wapate mtoto wa kiume.

2 Wafalme 4:8–17

Picha
familia ikisherehekea

Lakini baada ya miaka michache, mtoto aliugua na kufa. Mwanamke alikwenda kumtafuta Elisha kwa sababu alikuwa na imani kwamba Elisha angeweza kumwokoa mtoto wake. Elisha alikuja na kumbariki kijana na akaishi tena. Bwana alimsaidia Elisha kutenda miujiza mingi. Alikuwa nabii mkuu wa Bwana.

2 Wafalme 4:18–37

Chapisha