“Nehemia,” Hadithi za Agano la Kale (2022)
“Nehemia,” Hadithi za Agano la Kale
Nehemia 1–2; 4; 6
Nehemia
Kujenga upya ukuta huko Yerusalemu
Nehemia alikuwa Myahudi aliyeishi huko Uajemi. Alikuwa mtumishi aliyeaminiwa na mfalme. Siku moja Nehemia alisikia kwamba Wayahudi huko Yerusalemu walikuwa wakiteseka. Kuta zilizolinda Yerusalemu zilikuwa zimebomolewa na katu hazijajengwa tena. Yerusalemu ilikuwa hatarini. Nehemia alifunga na kuomba msaada kwa Bwana.
Mfalme alimwuliza Nehemia kwa nini alikuwa na huzuni sana. Alimwambia mfalme kuhusu hatari katika Yerusalemu. Mfalme alisema kwamba angeweza kusaidia. Nehemia aliomba kwenda Yerusalemu na kuujenga upya ule ukuta. Mfalme akamfanya Nehemia kuwa kiongozi na akampatia vifaa alivyohitaji.
Nehemia na Wayahudi walianza kujenga upya kuta. Lakini maadui waliwafanyia dhihaka na kujaribu kuwazuia.
Maadui walijaribu kumtega Nehemia ili aondoke mjini. Lakini Nehemia hakuondoka. Alimtumaini Bwana. Yeye alikuwa anafanya Kazi Kuu.
Nehemia aliwaambia watu wake wasiogope. Wakawaweka walinzi ili kuulinda. Wayahudi waliendelea kuujenga ukuta. Bwana aliwapa nguvu Wayahudi, nao wakaumaliza ukuta katika siku 52. Yerusalemu ilikuwa salama tena.