Hadithi za Maandiko
Nuhu na Familia Yake


“Nuhu na Familia Yake,” Hadithi za Agano la Kale (2022)

“Nuhu na Familia Yake,” Hadithi za Agano la Kale

Mwanzo 6–9; Musa 8

Nuhu na Familia Yake

Safina, gharika na ahadi za Bwana

Nuhu akiwatazama watu

Nuhu na familia yake walimtii Bwana. Watu wengine wote walikuwa waovu sana. Bwana alimwambia Nuhu kwamba gharika ingeifunika dunia ikiwa watu hawakutubu.

Mwanzo 6:5–13; Musa 8:13–17

Nuhu akiwafundisha watu

Nuhu aliwafundisha watu kwamba Bwana aliwapenda na aliwataka watubu na kuwa na imani katika Yesu Kristo. Watu hawakusikiliza.

Musa 8:19–30

Nuhu na familia yake wakijenga safina

Nuhu alikuwa na huzuni kwamba watu hawangetubu. Bwana alimwambia Nuhu kujenga merikebu kubwa iliyoitwa safina. Safina ingewaweka salama familia ya Nuhu wakati wa gharika.

Mwanzo 6:14–18; Musa 8:25

wanyama wakiingia ndani ya safina

Familia ya Nuhu iliingiza chakula ndani ya safina. Bwana alituma angalau wanyama wawili wa kila aina kwa Nuhu. Wanyama waliingia ndani ya safina na siku saba baadaye mvua ilianza kunyesha.

Mwanzo 6:18–22; 7:1–9

safina ikielea juu ya bahari

Kama vile ambavyo Bwana alikua ameonya, mvua ilinyesha kwa siku 40 mchana na siku 40 usiku. Gharika ilifunika dunia

Mwanzo 7:6–23

Nuhu na familia

Familia ya Nuhu pamoja na wanyama wote ndani ya safina walielea kwa usalama juu ya maji.

Mwanzo 7:24; 8:1–3

Nuhu, familia na wanyama juu ya nchi

Wakati gharika ilipokoma, safina ilisimama juu ya ardhi kavu. Nuhu na familia yake walijenga madhabahu ili kumwabudu Bwana na kumshukuru kwa kuwalinda. Bwana aliahidi kamwe kutoleta gharika duniani tena. Alituma upinde wa mvua kama ukumbusho wa ahadi Yake.

Mwanzo 8:13–22; 9:8–17