Hadithi za Maandiko
Kijana Daudi


“Kijana Daudi,” Hadithi za Agano la Kale (2022)

“Kijana Daudi,” Hadithi za Agano la Kale

1 Samweli 16

Kijana Daudi

Kijana mchungaji aliyeitwa kuwa mfalme

Samweli safirini

Bwana alimtuma nabii Samweli kumtafuta mfalme mpya. Sauli ambaye alikuwa mfalme wakati huo, alikuwa ameacha kumfuata Bwana. Bwana alimwambia Samweli asafiri kwenda Bethlehemu na amtafute mtu aliyeitwa Yese. Mfalme mpya angekuwa mmoja wa watoto wa Yese.

1 Samweli 16:1–5

Samweli na wana wa Yese

Wana wakubwa wa Yese walikuwa warefu na wenye nguvu. Lakini Bwana alimwambia Samweli asiwahukumu kwa mwonekano wao.

1 Samweli 16:6–10

Samweli akizungumza na Yese

Samweli alimwuliza Yese kama ana wana wengine. Yese alisema mwanawe mdogo, Daudi, alikuwa akichunga kondoo. Daudi akaletwa kwa Samweli.

1 Samweli 16:11

Samweli na Yese wakimwangalia Daudi mvulana mchungaji wa kondoo

Daudi alikuwa mdogo zaidi kuliko kaka zake na alikuwa mvulana mchungaji tu. Lakini Bwana hakujali Daudi alionekanaje. Bwana alijua moyo wa Daudi ulijaa imani. Yeye alimwambia Samweli kwamba Daudi angekuwa mfalme. Samweli akambariki Daudi. Roho wa Bwana alimtayarisha Daudi kuwa mfalme.

1 Samweli 16:12–13