“Bwana Anaongea na Eliya,” Hadithi za Agano la Kale (2022)
“Bwana Anaongea na Eliya,” Hadithi za Agano la Kale
Bwana Anaongea na Eliya
Kusikiliza sauti ya Bwana
Mfalme Ahabu alimwambia Malkia Yezebeli kwamba Bwana amewashinda makuhani wa Baali. Yezebeli alikasirika akasema angelimuua nabii Eliya.
Ili kukaa salama, Eliya aliondoka nchi ya Israeli. Alisafiri kwa siku 40 mchana na usiku, akifunga huku akienda. Kisha akafika kwenye Mlima Sinai na akalipata pango ajifiche ndani yake. Bwana akamwambia Eliya apande juu ya kilele cha mlima ili Yeye apate kuongea naye.
Upepo mkali ukaja na kuvunja miamba kuzunguka lile pango vipande vipande. Baada ya hilo, tetemeko la ardhi na kuitikisa ardhi. Kisha moto ukaanza. Eliya alisikia sauti kubwa za upepo, tetemeko la ardhi, na moto. Lakini sauti ya Bwana haikuwamo katika hizo sauti kubwa.
Eliya alisikia sauti ya ukimya, tulivu na ndogo. Naye alijua kuwa alikuwa Bwana. Bwana alimwuliza Eliya alikuwa akifanya nini humo.
Eliya alisema alikuwa anajificha ili kuwa salama. Manabii wote walikuwa wameuawa, na watu wamemkataa Bwana.
Bwana alimfariji Eliya na kumwambia kwamba kuna Waisraeli wengi ambao bado wanamwabudu Bwana. Bwana akamwomba arudi nyumbani ili kumwandaa nabii mwingine. Nabii huyu mpya jina lake lilikuwa Elisha.