“Mfalme Yosia,” Hadithi za Agano la Kale (2022)
“Mfalme Yosia,” Hadithi za Agano la Kale
2 Wafalme 22; 2 Mambo ya Nyakati 34–35
Mfalme Yosia
Kutafuta kutii amri za Bwana
Yosia alikuwa na umri wa miaka minane wakati alipofanywa kuwa mfalme wa Yuda. Alikuwa mfalme mwema aliyempenda Bwana. Alitaka kuwasaidia watu wake, Waisraeli, kumtii Bwana na kuacha kuabudu sanamu. Alipokuwa mkubwa, yeye na watu wake walianza kukarabati hekalu na kulirembesha tena.
2 Wafalme 22:1–2; 2 Mambo ya Nyakati 34:3–7
Wakati watu wakifanya kazi katika hekalu, Hilkia kuhani mkuu akapata kitabu cha sheria, hati ndefu kama ya zamani ambayo ilikuwa na maandiko matakatifu.
Mtumishi anamsomea Yosia. Yosia alisikia yale maneno na alihuzunika kwa sababu watu wake hawakumtii Bwana. Akararua mavazi yake ili kuonyesha kuwa alihuzunika.
Alimwambia Hilkia amuulize Bwana alipaswa kufanya nini. Hilkia na watumishi wa mfalme walimtembelea Hulda. Alikuwa nabii mke, kiongozi mwaminifu aliyeongozwa na Mungu. Alisema Bwana alifurahishwa na Yosia kwa sababu alikuwa akiwasaidia watu kutii. Bwana aliahidi kwamba Mfalme Yosia angeishi katika amani.
Mfalme Yosia alitaka watu wake kushika ahadi zao kwa Bwana. Aliwaomba washerehekee Pasaka ili iwasaidie kukumbuka jinsi Bwana alivyoaachilia huru Waisraeli miaka mingi iliyopita huko Misri.