“Musa juu ya Mlima Sinai,” Hadithi la Agano la Kale (2022)
“Musa juu ya Mlima Sinai,” Hadithi za Agano la Kale
Kutoka 19–20; 24; 31–34; Kumbukumbu la Torati 4–7
Musa juu ya Mlima Sinai
Kuwasaidia watu kumkumbuka Bwana
Musa na Waisraeli walisafiri kupitia nyikani. Wakafika kwenye mlima ulioitwa Mlima Sinai.
Musa alipanda mlimani ili kuongea na Bwana. Bwana alimwambia Musa kwamba alitaka kuongea na Waisraeli uso kwa uso.
Waisraeli walifika hadi chini ya Mlima Sinai, na Bwana akasababisha wingu la moshi kuuzunguka ule mlima. Bwana alikuwa katika lile wingu. Alisema na Waisraeli na kuwapa amri. Mlima ulitikisika alipokuwa akiongea.
Kutoka 19:16–19; 20:1–17; Kumbukumbu la Torati 4:12–13, 33; 5:4–5
Waisraeli waliogopa. Walimwomba Musa aongee na Bwana ili Musa aweze kuongea na wao kile ambacho Bwana alikitaka.
Musa alimchukua Haruni na wazee 70 wa Waisraeli kwenda juu ya mlima ili kupokea mafundisho zaidi ya Bwana. Bwana aliwatokea.
Kisha Bwana alimwambia Musa kuwaacha wale wazee hapo na kwenda juu zaidi ya mlima. Musa alitii. Bwana alitumia kidole Chake kuandika sheria Yake na amri juu ya zile mbao za mawe. Kwa siku 40, Bwana alimfundisha Musa mambo mengi.
Wakati Musa akiwa juu ya Mlima Sinai, watu wa Israeli walichoka kumsubiri. Walimwambia Haruni awatengeneze sanamu waiabudu kama walivyokuwa nayo kule Misri. Haruni akakusanya dhahabu yao yote na akatengeneza sanamu ya ndama.
Waisraeli walimwabudu yule ndama wa dhahabu na wakatoa dhabihu. Walisema ndama wa dhahabu, sio Bwana, aliwatoa utumwani kutoka Misri.
Bwana alijua Waisraeli walikuwa wakiabudu sanamu na wanamsahau Yeye. Akamwamuru Musa kurudi na awaambie watu watubu.
Musa aliposhuka chini kutoka Mlima Sinai na kuona Waisraeli wakiabudu ndama wa dhahabu. Alifadhaika sana. Watu hawakuwa tayari kutii sheria na amri ambazo Bwana aliziandika. Musa alizivunja zile mbao za mawe na akamwangamiza yule ndama wa dhahabu. Aliwasaidia Waisraeli kutubu na kumkumbuka Mungu wao wa kweli.
Musa alimwomba Bwana awasamehe Waisraeli na afanye ahadi nao tena. Musa aliahidi kuwaongoza na kuwafundisha.
Bwana aliwaambia Musa atengeneze mbao za mawe mpya na aende tena kwenye Mlima Sinai. Bwana akafanya ahadi mpya na Waisraeli na akawapa Amri Zake Kumi.
Kutoka 20:2–17; 34:1–17, 28; Kumbukumbu la Torati 6:24–25; 7:12–13