Hadithi za Maandiko
Danieli na Tundu la Simba


“Danieli na Tundu la Simba,” Hadithi za Agano la Kale (2022)

“Danieli na Tundu la Simba,” Hadithi za Agano la Kale

Danieli 6

Danieli na Tundu la Simba

Ujasiri wa kuomba wa mtu mmoja

Danieli akizungumza na mfalme

Dario alikuwa mtawala wa Babeli. Alimpenda Danieli na alitaka kumfanya kiongozi juu ya ufalme wote. Baadhi ya watu wenye hekima wa mfalme walikuwa na wivu.

Danieli 6:1–4

watu wenye hekima wakipanga njama

Watu wenye hekima walifahamu kwamba Danieli aliomba kwa Mungu, hivyo walimtega mfalme kwenye kutengeneza sheria mpya. Yeyote ambaye aliomba kwa Mungu angetupwa kwenye tundu la simba.

Danieli 6:5–9

Danieli akiomba

Danieli aliamua kuomba kwa Mungu licha ya yote. Watu wenye hekima wa mfalme walimuona Danieli akiomba na wakamwambia mfalme kwamba Danieli alikuwa akivunja sheria. Mfalme aligundua kuwa watu wake wenye hekima walikuwa wamemwekea mtego. Alijaribu kutafuta njia ya kumuokoa Danieli, lakini mfalme alipaswa kufuata sheria yake mwenyewe.

Danieli 6:10–15

Danieli katika tundu la simba

Danieli alitupwa ndani ya tundu la simba. Mfalme alikaa macho usiku kucha, akifunga ili kwamba Danieli aweze kulindwa.

Danieli 6:16–18

mfalme akimtazama Danieli ndani ya tundu la simba

Mapema asubuhi iliyofuata, mfalme aliharakisha kwenda kwenye tundu la simba. Alimwita Danieli ili kuona kama alikuwa bado hai. Danieli aliitika! Alimwambia mfalme kwamba Mungu alimtuma malaika kufunga midomo ya simba. Simba hawakumdhuru.

Danieli 6:19–23

mfalme akimkumbatia Danieli

Mfalme alikuwa na furaha kwamba Danieli alikuwa salama. Aliwaadhibu wale watu wenye hekima ambao walimtega na akasitisha sheria. Aliwafundisha ufalme wake kuhusu nguvu na wema wa Mungu.

Danieli 6:23–27