Scripture Stories
Familia ya Adamu na Hawa


“Familia ya Adamu na Hawa,” Hadithi za Agano la Kale (2022)

“Familia ya Adamu na Hawa,” Hadithi za Agano la Kale

Mwanzo 4; Musa 5–6

Familia ya Adamu na Hawa

Kuchagua kumfuata Bwana

Picha
Familia ya Adamu na Hawa

Baada ya Adamu na Hawa kuondoka kwenye Bustani ya Edeni, waliendelea kujifunza kuhusu mpango wa Baba wa Mbinguni kwa ajili yao hapa duniani. Walikuwa na watoto wengi na waliwafundisha yote waliyojua kuhusu Bwana. Baadhi ya watoto wa Adamu na Hawa walichagua kumtii Bwana. Lakini baadhi yao walichagua kutomtii.

Musa 5:1–12; 6:15

Picha
Adamu na Hawa pamoja na watoto, Adamu akiandika maandiko matakatifu

Familia ya Adamu na Hawa walitunza kitabu cha kumbukumbu Waliandika historia ya familia katika kitabu. Waliandika kuhusu jinsi Bwana alivyowasaidia.

Musa 6:5–6

Picha
Kaini na Abeli

Kaini na Abeli walikuwa wana wawili kati ya wana wa Adamu na Hawa. Abeli alimpenda Bwana na alichagua kumfuata Yeye. Kaini hakumtii Bwana. Yeye alichagua kuasi.

Mwanzo 4:1–16

Picha
mwanaume akiangalia mji

Familia ya Adamu na Hawa iliendelea kukua. Watu wengi zaidi walizaliwa. Wote walikuwa na uhuru wa kufanya maamuzi. Wakati ulifika, baadhi ya watu waliasi dhidi ya amri za Bwana. Bwana aliwatuma manabii wafundishe watu kutubu.

Mwanzo 4:25–26; Musa 5:13; 6:23

Chapisha