Agano la Kale 2022
Aprili 25–Mei 1. Kutoka 24; 31–34: “Uso Wangu Utakwenda Pamoja Nawe”


“Aprili 25–Mei 1. Kutoka 24; 31–34: ‘Uso Wangu Utakwenda Pamoja Nawe’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Kale 2022 (2021)

“Aprili 25–Mei 1. Kutoka 24; 31–34,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2022

Picha
Yehova anamtokea Musa na wazee wa Israeli

Kielelezo cha Yehova akimtokea Musa na wazee 70 wa Israeli, na Jerry Harston

Aprili 25–Mei 1

Kutoka 24; 31–34

“Uso Wangu Utakwenda Pamoja Nawe”

Musa alipokuwa anajiandaa kuwaongoza wana wa Israeli kwenda nchi ya ahadi, Bwana alisema, “Uso Wangu Utakwenda Pamoja Nawe” (Kutoka 33:14). Unapojiandaa kufundisha watoto katika darasa lako, fikiria jinsi unavyoweza kualika uwepo wa Bwana “kwenda pamoja [nawe].”

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Muombe kila mtoto kuchagua karatasi iliyo na namba bila ya utaratibu. Tumia hizi namba kuweka mpangilio ambao watoto wanaweza kushiriki kitu wanachojifunza kutoka kwenye maandiko, iwe nyumbani au katika Msingi.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Kutoka 31:13, 17

Kuitukuza Sabato ni ishara ya upendo wangu kwa Bwana.

Bwana alimwambia Musa kwamba wakati wana wa Israeli waliishika siku ya Sabato kwa utakatifu, walimwonyesha Yeye kwamba wanataka kuwa watu Wake.

Shughuli Yamkini

  • Chora moyo ubaoni, na waulize watoto kile ishara hii inaweza kuwa inamaanisha. Wasaidie wafikirie vitu vingine ambavyo vinaweza kuwa ishara ya upendo, kama kumbatio au kitendo cha huduma. Wasomee Kutoka 31:13. Wasaidie kuelewa kwamba tunapoishika siku ya Sabato kwa utakatifu, ni ishara kwa Bwana kwamba tunampenda Yeye.

  • Waambie watoto baadhi ya njia unazojaribu kuonyesha upendo wako kwa Bwana siku ya Sabato. Waache washiriki jinsi wao na familia zao wanafanya hivi. Waalike wao watumie ukurasa wa shughuli ya wiki hii kushiriki mawazo zaidi.

    Picha
    watoto na wazazi nyumbani

    Kwa kutukuza Sabato, tunaonyesha upendo wetu kwa Bwana.

Kutoka 32:1–8, 19–24

Ninaweza kumweka Bwana kwanza katika maisha yangu.

Wakati Musa alikuwa kwenye Mlima Sinai akizungumza na Bwana, wana wa Israeli walichagua kuabudu sanamu wa dhahabu badala ya Yeye. Hadithi hii inaweza kuwakumbusha watoto unawaowafundisha kwamba hatupaswi kuacha vitu vingine kuwa muhimu kwetu kumshinda Bwana.

Shughuli Yamkini

  • Pitia tena pamoja na watoto Amri Kumi, ukisisitizia mbili za kwanza (ona Kutoka 20:3–6). Tumia “Amri Kumi” (katika Hadithi za Agano la Kale) kushiriki pamoja nao hadithi kutoka katika Kutoka 32:1–8, 19–24. Kama inawezekana, waache watoto wakusaidie kusimulia hadithi hii. Wasaidie watoto kuona kosa la katika hadithi hii (unaweza kutaka kuwakumbusha watoto amri mbili za kwanza kati ya Amri Kumi). Je, Waisraeli wangepaswa wafanye nini badala yake?

  • Onyesha picha ya Yesu Kristo, pamoja na picha za vitu vingine ambavyo watoto wanaweza kutenga muda wao kwavyo, kama vile wanasesere, michezo, na vinginevyo. Waombe watoto wakusaidie kutafuta picha inayoonyesha kile kinachopaswa kuwa muhimu kwetu. Shiriki na watoto jinsi ulivyobarikiwa kwa kumweka Bwana kwanza katika maisha yako—hata mbele ya vitu vingine ambavyo ni vizuri.

Kutoka 33:11

Bwana alizungumza na Musa uso kwa uso.

Baada ya Musa kumharibu ndama wa dhahabu, “Bwana akasema na Musa uso kwa uso, kama vile mtu asemavyo na rafiki yake.” Kujua hili kunaweza kujenga imani ya watoto kwamba Bwana ni mtu halisi ambaye anatupenda.

Shughuli Yamkini

  • Waambie watoto jinsi unavyohisi unapozungumza na rafiki mzuri na waulize jinsi wanavyohisi. Wasomee sentensi ya kwanza katika Kutoka 33:11. Waulize watoto vile wanavyodhani nabii Musa alihisi. Waambie watoto kuhusu wakati ulihisi kuwa karibu na Bwana, hata kama hukumuona Yeye kwa macho yako.

  • Imbeni pamoja wimbo ambao unaonyesha jinsi Baba wa Mbinguni au Yesu huhisi juu yetu kama vile “Jesus Is Our Loving Friend” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 58). Onyesha picha za Mwokozi akionyesha wengine upendo (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 36, 41–43, 46–46). Wahimize watoto kushiriki jinsi wanavyohisi kuhusu Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Kutoka 31:12–17

Kuitukuza Sabato ni ishara ya upendo wangu kwa Bwana.

Kuishika siku ya Sabato kwa utakatifu inaweza kuwa rahisi—na furaha zaidi—kwa watoto wanapogundua kwamba ni ishara ya msimamo wetu kwa Bwana.

Shughuli Yamkini

  • Waulize watoto maswali machache kuwasaidia wao kuelewa ishara ni nini—kwa mfano, “Ni ishara gani zinakuonyesha kwamba msimu wa kuchipua unakuja au kwamba unashikwa na mafua?” Waalike wasome Kutoka 31:13 16–17 na kutafuta neno “ishara.” Ni nini Bwana alisema ndiyo ishara kati yetu na Yeye? Kwa nini ishara hii ni muhimu?

  • Waalike watoto kufanya zamu kuelezea kwa nini wanachagua kutukuza Sabato. Video kama “The Sabbath Is for You” au “Upon My Holy Day—Honoring the Sabbath” (ChurchofJesusChrist.org) zinaweza kusaidia.

  • Waalike watoto waandike vitu vingi wanavyoweza kufikiria ambavyo wanaweza kufanya siku ya Jumapili kumwonyesha Bwana kwamba wanampenda Yeye. Wahimize kushiriki vitu vichache kutoka kwenye orodha zao. Waombe waende na orodha zao nyumbani, wazishiriki na familia zao, na wazirejelee wanapohitaji mawazo kuhusu nini cha kufanya siku ya Sabato.

Kutoka 32:1–8, 19–24

Ninaweza kumweka Bwana kwanza katika maisha yangu.

Ujumbe mmoja kutoka kwenye simulizi katika Kutoka 32 ni umuhimu wa kuzitii amri mbili za kwanza kati ya zile Amri Kumi—usiabudu mtu yeyote au kitu chochote ila Bwana.

Shughuli Yamkini

  • Waombe watoto washiriki chochote kile wanachojua kuhusu hadithi ya Haruni akitengeneza ndama wa dhahabu kwa ajili ya Waisrael kuabudu. Kama wanahitaji msaada, warejeshe kwenye Kutoka 32:1–8, 19–24, au shiriki nao “Amri Kumi” (katika Hadithi za Agano la Kale). Kwa nini ilikuwa kosa kwa Waisraeli kuabudu sanamu? (Unaweza kuwarejesha watoto kwenye amri mbili za kwanza za Amri Kumi katika Kutoka 20:3–6.)

  • Wasaidie watoto kufikiria mifano ya vitu ambavyo watu wanaweza kujaribiwa kuabudu badala ya Bwana—vitu ambavyo huondoa usikivu wetu mbali Naye. Kisha waombe watoto washiriki mifano ya vitu ambavyo vinawasaidia kufokasi kwa Mwokozi na kumwabudu Yeye.

Kutoka 32:1–5, 21–24

Ninaweza kusimama kwa ajili ya haki.

Wakati Waisraeli walipomwambia Haruni atengeneze sanamu ya dhahabu, alikubali kufanya hivyo hata ingawa hii ilikuwa makosa (ona Kumbukumbu la Torati 9:20). Fikiria jinsi utakavyowatia moyo watoto kusimama kwa ajili haki, hata wakati wengine wanawashinikiza kutofanya hivyo.

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto wasome Kutoka 32:1–5, 21–24, kibinafsi au wawili wawili, na kushiriki kile wanachofikiri Haruni alipaswa kufanya wakati Waisraeli walipomuomba atengeneze ndama wa dhahabu. Je, Haruni angewasaidia watu vipi?

  • Wasaidie watoto wafikirie hali ambazo wanaweza kukumbana nazo wakati watu wengine wanapowaomba kufanya kitu ambacho ni kosa. Waombe watoto washiriki mawazo wao kwa wao kuhusu nini cha kufanya katika hali kama hizo.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Wahimize watoto kushiriki na familia zao mawazo yoyote waliyoyasikia leo kuhusu jinsi ya kuishika siku ya Sabato kwa utakatifu.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Waalike watoto kutoa ushuhuda. Maswali utakayouliza yanaweza kuwatia moyo watoto kushiriki jinsi wanavyohisi kuhusu Mwokozi na jinsi kuishi injili kulivyowabariki. Wanapofanya hivi, wanatoa ushuhuda. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 1132.)

Chapisha