Agano la Kale 2022
Mei 9–15. Hesabu 11–14; 20–24: Msiasi dhidi ya Bwana, Wala Msiogope”


“Mei 9–15. Hesabu 11–14; 20–24: ‘Msiasi dhidi ya Bwana, Wala Msiogope’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Kale 2022 (2021)

“Mei 9–15. Hesabu 11–14; 20–24,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2022

Picha
bonde la jangwani

Mei 9–15

Hesabu 11–14; 20–24

“Msiasi dhidi ya Bwana, Wala Msiogope”

Muhtasari huu haunuiwi kuwa mswada. Badala yake, utumie kupata mawazo na msukumo kwa ajili ya kujifunza shughuli ambazo zitaweza kuwabariki watoto katika darasa lako.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waoneshe watoto mojawapo ya picha zilizo katika muhtasari huu au katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Waache wao washiriki pamoja nawe chochote wanachokijua kuhusu kile kinachotendeka katika picha.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Hesabu 11:4–10

Ninaweza kuwa na shukrani kwa ajili ya kile Mungu amenipa.

Hata ingawa Bwana alikuwa amewafanyia mambo ya ajabu wana wa Israeli, mara nyingi walizingatia kile ambacho hawakuwa nacho. Wasaidie watoto kujifunza kuwa na shukrani kwa ajili ya kile Mungu amewapa.

Shughuli Yamkini

  • Waulize watoto kama wanakumbuka baadhi ya miujiza Bwana alifanya kuwabariki wana wa Israeli huko nyikani. (Kama watoto wanahitaji msaada, waoneshe picha kutoka kwenye muhtasari wa Aprili 4–10 katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia; ona pia Kutoka 14:21–22; 15:23–25; 16:4.) Kisha fupisha kwa ajili yao Hesabu11:4–10, ukisisitiza kwamba Bwana hakufurahi kwa sababu wana wa Israelli walikuwa wananung’unika. Wasaidie watoto kufikiria njia wanazoweza kuonesha shukrani kwa Bwana.

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu shukrani, kama vile “Count Your Blessings“ (Nyimbo za Kanisa, na. 241). Mwalike kila mtoto achore picha ya baraka ambazo Bwana amewapa wao au familia zao. Wahimize wao kufikiri kuhusu picha zao au waziangalie wakati wowote wanapojaribiwa kunung’unika kuhusu kitu ambacho hawana.

Hesabu 13:17–33; 14:6–9

Imani inaweza kunisaidia kutoogopa.

Wakati Musa alipowatuma wanaume kumi na wawili kuchunguza kuhusu nchi ya ahadi, 10 kati yao walirudi kwa uoga kwa sababu ya majitu ambayo yalikuwa yanaishi huko. Wawili kati yao, Kalebu na Yoshua, hawakuogopa, kwa sababu walikuwa na imani katika Bwana.

Shughuli Yamkini

  • Tumia picha au michoro ya zabibu, asali, majitu na panzi kuwasimulia kwa kifupi watoto kuhusu wale wanaume 12 Musa aliowatuma kuchunguza nchi ya ahadi (ona Hesabu 13:17–13; ona pia “Miaka Arobaini Nyikani” katika Hadithi za Agano la Kale). Elezea kwamba walipata matunda mengi na vyakula vingine (waalike watoto wajifanye wanakula chakula), lakini pia walikuwa na uoga kwa sababu watu huko walikuwa wakubwa sana na wenye nguvu (waalike watoto wajifanye wanaogopa). Onyesha picha ya Yesu, na useme wazi kwamba Waisraeli wawili, Kalebu na Yoshua, hawakuogopa, kwa sababu walikuwa na imani katika Yesu Kristo.

  • Wasomee watoto Hesabu 14:9 na uzungumze kuhusu wakati ambapo ulikuwa na uoga lakini imani yako katika Yesu Kristo ilikusaidia kuwa jasiri. Wasaidie watoto kufikiria juu ya uzoefu sawa na huo ambao wamekuwa nao.

    Picha
    wanaume wakimwonyesha Musa matunda

    Kumi kati ya wapelelezi wa Waisraeli walikuwa na uoga; Yoshua na Kalebu walikuwa na imani. © Lifeway Collection/licensed from goodsalt.com

Hesabu 21:6–9

Ninaweza kumtegemea Yesu Kristo.

Kama vile tu wana wa Israeli waliponywa kwa kumtazama nyoka wa shaba, watoto katika darasa lako wanaweza kupokea wokovu kwa kumtazama Mwokozi.

Shughuli Yamkini

  • Ukitumia ukurasa wa shughuli au picha katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia, waambie watoto kile kilichotendeka wakati “nyoka wakali” walipokuja katika kambi ya Waisraeli (ona Hesabu 21:6–9). Wasaidie kuona jinsi nyoka wa shaba ni kama Yesu Kristo (ona Yohana 3:14–15). Kisha waache watoto wachukue zamu kwa kutumia picha kusimuliana hadithi wao kwa wao.

  • Waombe watoto wafumbe macho yao wakati ukiweka picha ya Mwokozi mahali fulani katika chumba. Kisha waambie wafumbue macho yao, watafute picha hiyo, na kuitazama. Acha wao wachukue zamu ya kuiweka picha hiyo. Kila wakati watoto wanapoipata picha hiyo, wasaidie kufikiria kitu wanachoweza kufanya kumtegemea Mwokozi.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Hesabu 12

Bwana ananitaka nimfuate nabii Wake.

Hesabu 12 ina baadhi ya masomo ya thamani ambayo yanaweza kuwasaidia watoto wanapowasikia watu wakisema mambo yasiyo ya ukarimu kuhusu nabii wa Bwana au viongozi wengine wa Kanisa.

Shughuli Yamkini

  • Waambie watoto kwamba wakati mmoja, Bwana alikasirishwa na Haruni na Miriamu, kaka na dada wa Musa. Waalike wasome Hesabu 12:1–2 ili kujua kwa nini. Kulingana na mstari wa 5–8, ni insi gani Bwana alijisikia kuhusu Haruni na Miriamu wakisema dhidi ya nabii Wake?

  • Wasaidie watoto kufikiria mifano ya watu katika maandiko ambao walimfuata nabii na wakabarikiwa (kwa ajili ya mifano, ona Mwanzo 7:7; 1 Nefi 3:7). Ni baadhi ya mambo gani ambayo nabii wetu aliye hai ametufundisha? Ni kwa jinsi gani tunabarikiwa tunapofuata mafundisho yake?

Hesabu 21:4–9

Yesu Kristo ana uwezo wa kuniponya kiroho.

Waisraeli wengi walikufa kwa sababu hawakuwa na imani kwamba Bwana angewaponya kama wangemtazama nyoka wa shaba (ona Alma 33:18–20). Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kuwa na imani katika Yesu Kristo?

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto wachore picha za kile walichosoma katika Hesabu 21:4–9. Waache wao watumie picha zao kusimulia hadithi hiyo. Muombe kila mtoto achague mojawapo ya maandiko yafuatayo na kushiriki kile yanachoongeza katika uelewa wa hadithi hiyo: Yohana 3:14–15; 1 Nefi 17:41; Alma 33:18–20; Helamani 8:13–15; Mafundisho na Maagano 6:36.

  • Andika ubaoni swali kama Tunaweza kufanya nini “kumtegemea Mwana wa Mungu kwa imani”? (Helamani 8:15). Mpe kila mtoto kipande cha karatasi, na waombe waandike majibu mengi kwa kadiri wanavyoweza kwa swali hilo. Kusanya karatasi hizo, usome majibu machache kwa sauti, na uwaalike watoto wazungumze kuhusu ni jinsi gani kufanya mambo haya kunaweza kutusaidia tunapohitaji nguvu za uponyaji za Mwokozi.

Hesabu 22–24

Ninaweza kufuata mapenzi ya Mungu, hata kama wengine wanajaribu kunishawishi nisifanye hivyo.

Balaki alijaribu kumshawishi Balaamu kuwalaani Waisraeli, lakini Balaamu alijua kwamba hii ilikuwa kinyume na mapenzi ya Mungu. Mfano wa Balaamu unaweza kuwasaidia watoto wanapopatwa na shinikizo la kutokumtii Mungu.

Shughuli Yamkini

  • Wafanyie watoto muhtasari wa Hesabu 22:1–18 ukisisitiza jinsi Balaamu alivyokataa kuwalaani watu wa Mungu, hata ingawa Balaki, mfalme wa Moabu, alitaka kumpa hadhi na utajiri. Waombe watoto wapekue mistari ifuatayo kwa ajili ya vifungu vya maneno ambavyo wanahisi vinaonyesha dhamira ya Balaamu ya kumfuata Mungu: Hesabu 22:18; 23:16; 24:13. Waalike watoto wachague kifungu kimoja cha maneno wanachokipenda na kuandika kwenye kadi ili kuwasaidia wao kukumbuka kumtii Bwana.

  • Zungumza na watoto kuhusu hali ambapo marafiki au wengine wangeweza kujaribu kuwashawishi wafanye kosa, kama Balaki alivyomfanyia Balaamu. Ni kwa jinsi gani dhamira ya Balaamu kwa Bwana ilimsaidia kuepuka shinikizo kutoka kwa Balaki? Waalike watoto wafanye zoezi la hali hizi wakitumia maneno kama ya Balaamu.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kushiriki kitu pamoja na familia zao, kama vile picha, andiko, au wimbo ambao unaonyesha kile walichojifunza katika Msingi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Kuwa tayarii kupokea ushawishi toka kwa Roho. “Mara nyingi nafasi nzuri zaidi za kufundisha huja bila kutarajia—kwa mfano, wakati mtu anaposhiriki uzoefu au anapouliza swali linaloelekeza kwenye majadiliano muhimu. … Uwe radhi kubadili mipango yako kama inabidi ili kufuata ushawishi unaoupokea” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 10).

Chapisha