Agano la Kale 2022
Mei 2–8. Kutoka 35–40; Mambo ya Walawi 1; 16; 19: “Utakatifu kwa Bwana”


“Mei 2–8. Kutoka 35–40; Mambo ya Walawi 1; 16; 19: ‘Utakatifu kwa Bwana’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Kale 2022 (2021)

“Mei 2–8. “Kutoka 35–40; Mambo ya Walawi 1; 16; 19,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2022

Picha
Hekalu la São Paulo Brazil

Mei 2–8

Kutoka 35–40; Mambo ya Walawi 1; 16; 19

“Utakatifu kwa Bwana”

Unapojifunza kwa maombi maandiko wiki hii, fikiria kuhusu watoto unaowafundisha. Roho Mtakatifu anaweza kukusaidia kujua kweli zipi wanahitaji kujifunza na jinsi unavyoweza kufundisha kweli hizo kwao.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Weka jina la kila mtoto ndani ya chombo. Muombe mtoto mmoja kuchukua mojawapo ya majina, na umwalike mtoto ambaye jina lake limetwaliwa kushiriki kitu alichojifunza hivi karibuni kutoka kwenye Agano la Kale. Zungumza na watoto kuhusu jinsi vitu wanavyojifunza vinawasaidia kuwa karibu na Yesu Kristo. Endelea mpaka kila mtoto awe amepata nafasi ya kushiriki.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Kutoka 36:1

Ninaweza kusaidia katika kazi ya Bwana.

Watoto wadogo wana vipawa ambavyo wanaweza kuvitumia kuchangia katika kazi ya Bwana duniani. Unawezaje kuwasaidia watoto kuhisi shauku ya kushiriki kile Bwana amewapatia?

Shughuli Yamkini

  • Wasomee watoto, Kutoka 36:1 na uwaombe wasikilize kile Bwana alichompa Bezaleli na Oholiabu ili kuwasaidia kujenga “mahali patakatifu” (tabenakulo). Mwambie kila mtoto kuhusu kipawa alichonacho (inaweza kusaidia kuwauliza wazazi). Shuhudia kwamba Mungu “ameweka” vipawa ndani ya watoto Wake.

  • Waambie watoto kwa nini unataka kusaidia katika kazi ya Bwana. Wasaidie wafikirie njia wanazoweza kushiriki pia (kama vile kujifunza kuhusu babu, kumwelezea mtu kuhusu Yesu, au kuhudumia mwanafamilia). Andika mawazo yao kwenye vipande vya karatasi, uviweke ndani ya chombo, na umwalike kila mtoto achague kimoja na kufanya tendo lililo kwenye kipande cha karatasi.

Kutoka 40:17–34

Ninaweza kuhisi uwepo wa Mungu katika sehemu takatifu.

Bwana aliwaamuru wana wa Israeli kujenga tabenakulo ili Yeye aweze “kukaa miongoni mwao” (Kutoka 25:8). Unaweza kuwasaidia watoto kujifunza kuhusu sehemu takatifu ambazo Mungu ametupa leo ili kutusaidia kuhisi uwepo Wake.

Shughuli Yamkini

  • Onesha picha ya tabenakulo la kale (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia.). Waombe watoto watafute sehemu tofauti za tabenakulo katika picha hiyo, kama vile mshumaa au madhabahu, na uelezee kwamba vitu hivi vilikusudiwa kuwasaidia Waisraeli kumfikiria Bwana (kwa taarifa zaidi kuhusu tabenakulo, ona Kutoka 40:17–34). Ni sehemu gani takatifu tulizonazo leo ambazo zinatusaidia kufikiria kuhusu Bwana?

  • Onesha picha ya hekalu, na uwasomee watoto Kutoka 25:8. Elezea kwamba katika siku yetu, Mungu ametupa sehemu takatifu ambapo tunaweza kuwa karibu Naye. Wasaidie watoto kuorodhesha baadhi ya sehemu hizi. Waulize watoto jinsi wanavyohisi wakati wanafikiria kuhusu sehemu hizi takatifu. Shiriki pamoja nao kwamba tunaweza pia kuhisi kuwa karibu na Mungu wakati tunasali, bila kujali tuko wapi.

  • Kamilisha ukurasa wa shughuli pamoja na watoto. Mnapofanya hivyo, imba wimbo pamoja nao kuhusu hekalu, kama vile “I Love to See the Temple” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 95).

    Picha
    Hekalu la Roma Italia

    Kama vile tabenakulo la kale, hekalu hutuelekeza kwa Mwokozi.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Kutoka 3:20–29; 36:1

Mungu amenipa vipawa vya kiroho kunisaidia kufanya kazi Yake.

Kila mmoja wa watoto wa Baba wa Mbinguni ana kitu cha kuchangia katika kazi Yake. Watoto unaowafundisha wanaweza kuhitaji msaada wako kutambua jinsi wanavyoweza kutumia vipawa vyao kusaidia katika kazi Yake.

Shughuli Yamkini

  • Onesha picha ya tabenakulo (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia.). Waulize watoto ni vifaa gani vingeweza kuhitajika ili kujenga tabenakulo. Soma pamoja na watoto Kutoka 35:20–29, na waombe watafute jinsi vifaa vilivyohitajika vilivyopatikana. Shuhudia kwamba kila mtoto ana kitu fulani cha kuchangia katika kazi ya Bwana.

  • Waombe watoto wasome Kutoka 36:1 ili kujua kile ambacho Bwana aliwapa wale ambao waliitwa ili kusaidia kujenga tabenakulo. Waalike watoto kushiriki kile wanachohisi Bwana amewapa ili kusaidia kujenga ufalme Wake (toa mapandekezo kama yanahitajika). Ni kwa jinsi gani tunaweza kutumia vitu hivi kuwabariki wengine?

Kutoka 40:17–33

Ninaweza kuwa zaidi kama Yesu Kristo na Baba wa Mbinguni.

Tabenakulo halikuwaruhusu tu wana wa Israeli kuwa kwenye uwepo wa Mungu, bali pia liliwafunza vitu ambavyo wangefanya ili kuwa zaidi kama Mungu

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto watumie Kutoka 40:17–33 na kutambua vitu ambavyo vilikuwa sehemu ya tabenakulo na watafute baadhi ya picha za tabenakulo la kale (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Waalike watoto kuchora picha zao wenyewe za tabenakulo. Zungumza jinsi gani kila sehemu ya tabenakulo inaweza kufunza kuhusu Mwokozi au Baba wa Mbinguni. Kwa mfano, sanduku la ushuhuda linaweza kutukumbusha amri za Mungu, madhabahu yanaweza kutukumbusha dhabihu ya Yesu Kristo, kinara cha mshumaa kinaweza kutukumbusha kwamba Mwokozi ndiye Nuru ya Ulimwengu na kadhalika.

  • Waombe watoto wasome Kutoka 25:8 ili kujua kwa nini Bwana aliwataka wana wa Israeli kujenga “mahali patakatifu” (au tabenakulo). Wasaidie watoto kuorodhesha mahali na mazingira ambapo tunaweza kuhisi uwepo wa Bwana. Je, ni kwa namna gani sehemu hizi zinatusaidia kuwa zaidi kama Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo?

Mambo ya Walawi 1:1–4

Kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, ninaweza kusamehewa.

Sadaka za wanyama zilizofanywa katika Agano la Kale zilikusudiwa kuwafundisha wana wa Israeli kuhusu msamaha uliowezeshwa kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo.

Shughuli Yamkini

  • Onesha picha za Yesu Kristo katika Gethsemane na kwenye msalaba (ona Kitabu cha Sanaa za Injili, na. 5657). Elezea kwamba Bwana aliwaamuru wana wa Israeli kutoa sadaka ili kuwafunza kwamba wanaweza kusamehewa dhambi zao kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo. Soma pamoja na watoto Mambo ya Walawi 1:1–4, na uwaombe watafute maneno au vifungu vya maneno ambavyo vinawakumbusha dhabihu ya Yesu Kristo.

  • Onyesha picha ya Yesu Kristo akiwatembelea watu wa Amerika (kama vile Kitabu cha Sanaa za Injili, na. 82). Elezea kwamba baada ya Yesu Kristo kusulubiwa na kufufuka, aliwafundisha watu wa Amerika kwa nini hawakuhitaji tena kutoa sadaka za wanyama. Someni pamoja 3 Nefi 9:19–20, na uwaulize watoto kile tunachoamriwa kutoa kama mdadala wa sadaka za kuteketeza. Je, inamaanisha nini kutoa dhabihu ya moyo uliopondeka na roho iliyovunjika? Pendekeza kwamba watafute “Moyo Uliopondeka” katika Mwongozo wa Maandiko (scriptures.ChurchofJesusChrist.org) kwa msaada wa kujibu swali hili. Waalike watafakari jinsi wanavyoweza kutoa moyo uliovunjika na roho iliyopondeka kwa Bwana.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kumuuliza Baba wa Mbinguni wiki hii jinsi Yeye angetaka wao wachangie katika kazi Yake katika familia zao.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Waelekeze watoto kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Lengo lako kubwa linapaswa kuwa ni kuwasaidia watoto unaowafundisha kuimarisha imani yao katika Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Je, unaweza kufanya nini ili kuwasaidia wao kuelewa jinsi gani kuishi kweli za injili kutawasaidia kuwa zaidi kama Baba na Mwana?

Chapisha