Agano la Kale 2022
Mei 9–15. Hesabu 11–14; 20–24: “Lakini Msimwasi Bwana, Wala Msiwaogope”


“Mei 9–15. Hesabu 11–14; 20–24: ‘Lakini Msimwasi Bwana, Wala Msiwaogope,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2022 (2021)

“Mei 9–15. Hesabu 11–14; 20–24,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2022

Picha
bonde la jangwani

Mei 9–15

Hesabu 11–14; 20–24

“Lakini Msimwasi Bwana, Wala Msiwaogope”

Muhtasari huu unaonyesha baadhi ya kanuni za thamani katika kitabu cha Hesabu. Kuwa muwazi pia kwa zingine ambazo Roho anaweza kukusaidia kuziona.

Andika Misukumo Yako

Hata kwa miguu, isingewezekana kwa kawaida kuchukua miaka 40 kusafairi kutoka nyika ya Sinai hadi nchi ya ahadi ya Kanaani. Ila huo ndio muda ambao wana wa Israeli walihitaji, sio kukamilisha umbali wa kijiografia ila kukamilisha umbali wa kiroho: umbali kati ya wao walikuwa nani na nani Bwana alitaka wawe kama watu Wake wa agano.

Kitabu cha Hesabu kinaelezea baadhi ya kile kilichotokea wakati wa miaka hiyo 40, ikijumuisha masomo ambayo wana wa Israeli walihitaji kujifunza kabla ya kuingia nchi ya ahadi. Walijifunza kuhusu kuwa waaminifu kwa watumishi wateule wa Bwana (ona Hesabu 12). Walijifunza kuhusu kutumainia nguvu za Bwana, hata wakati siku zijazo zilipoonekana hazina tumaini (ona Hesabu 13–14). Na walijifunza kwamba kutokuwa na imani au kutotumaini huleta maumivu ya kiroho, ila wangeweza kutubu na kumtegemea Mwokozi kwa ajili ya uponyaji (ona Hesabu 21:4–9).

Wote tuko kama Waisraeli katika baadhi ya njia. Wote tunafahamu inavyokuwa kuwa katika nyika ya kiroho, na masomo kama hayo waliyojifunza yanaweza kutusaidia kujiandaa kuingia katika nchi yetu ya ahadi: uzima wa milele pamoja na Baba yetu wa Mbinguni.

Kwa ajili ya muhtasari wa kitabu cha Hesabu, ona “Hesabu” katika Kamusi ya Biblia.

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Hesabu 11:11–17, 24–29; 12

Ufunuo unapatikana kwa wote, lakini Mungu analiongoza Kanisa Lake kupitia nabii Wake.

Katika Hesabu 11:11–17, 24–29, tazama tatizo Musa alilokabiliana nalo na suluhisho alilopendekeza Mungu. Unafikiri Musa alimaanisha nini aliposema alitamani “kwamba watu wote wa Bwana wangekuwa manabii”? (mstari wa 29). Unapotafakari mistari hii, zingatia maneno haya ya Rais Russell M. Nelson: “Je, Mungu kweli anataka kuongea na wewe? Ndiyo! … “Ee, kuna mengi zaidi Baba yako wa Mbinguni anataka wewe uyajue” (“Ufunuo kwa ajili ya Kanisa, Ufunuo kwa ajili ya Maisha Yetu,” Liahona, Mei 2018, 95).

Ingawa, kusema kwamba kila mmoja anaweza kuwa nabii haimaanishi kuwa wote wanaweza kuwaongoza watu wa Mungu kama alivyofanya Musa. Tukio lililoandikwa katika Hesabu 12 linaweka wazi jambo hili. Unaposoma sura hii, ni tahadhari ipi unaipata? Unahisi ni nini Bwana anakutaka wewe kufahamu kuhusu ufunuo binafisi na kumfuata nabii?

Ona pia 1 Nefi 10:17; Mafundisho na Maagano 28:1–7; Dallin H. Oaks, “Njia Mbili za Mawasiliano,” Liahona, Nov. 2010, 83–86.

Hesabu 13–14

Kwa imani katika Bwana, naweza kuwa na tumaini la baadaye.

Unaposoma Hesabu 13–14, jaribu kujiweka mwenyewe katika nafasi ya Waisraeli. Kwa nini unafikiri walitaka “kurudi Misri”? (Hesabu 14:3). Je, wewe uko kama wale ambao walikosa rajua kuhusu kuingia nchi ya ahadi? Je, ungeielezeaje “roho” nyingine aliyokuwa nayo Kalebu? (Hesabu 14:24). Ni nini kinakufurahisha kuhusu imani ya Kalebu na Yoshua, na unawezaje kutumia mifano yao katika hali unazokabiliana nazo?

Ona pia Teachings of Presidents of the Church: Gordon B. Hinckley (2016), 75–76.

Hesabu 21:4–9

Ikiwa nitamtegemea Yesu Kristo kwa imani, Yeye anaweza kuniponya kiroho.

Manabii wa Kitabu cha Mormoni walijua hadithi iliyorekodiwa katika Hesabu 21:4–9 na walielewa umuhimu wake kiroho. Ni nini 1 Nefi 17:40–41; Alma 33:18–22; na Helamani 8:13–15 inaongeza katika uelewa wako wa hadithi hii? Unaposoma vifungu hivi, fikiria kuhusu uponyaji wa kiroho unaoutumainia. Waisraeli walipaswa “[kutazama] nyoka wa shaba” (Hesabu 21:9) ili kuponywa. Unahisi msukumo wa kufanya nini ili kwa ukamilifu zaidi “umtazame Mwana wa Mungu kwa imani”? (Helamani 8:15).

Ona pia Yohana 3:14–15; Mafundisho na Maagano 6:36; Dale G. Renlund, “Sheheni kwa Baraka,” Liahona, Mei 2019, 70–73.

Picha
nyoka wa shaba

Waisraeli walipona kwa kumtazama nyoka wa shaba.

Hesabu 22–24

Naweza kufuata mpenzi ya Mungu, hata kama wengine wanajaribu kunishawishi mimi nisifanye hivyo.

Wakati Balaki, mfalme wa Moabu, alipojua kuwa Waisraeli walikuwa wanakaribia, alimwita Balaamu, mtu aliyejulikana kwa kutamka baraka na laana. Balaki alitaka yeye awadhoofishe Waisraeli kwa kuwalaani. Tazama jinsi Balaki alivyojaribu kumshawishi Balaamu (ona Hesabu 22:5–7, 15–17), na fikiria kuhusu majaribu unayokabiliana nayo kwenda kinyume na mapenzi ya Mungu. Nini kinakupa hamasa kuhusu mwitikio wa Balaamu katika Hesabu 22:18, 38; 23:8, 12, 26; 24:13?

Kwa bahati mbaya, inaonekana kwamba Balaamu hatimaye alishindwa kwa shinikizo na kuisaliti Israeli (ona Hesabu 31:16; Yuda 1:11). Tafakari ni kwa namna gani unaweza kuendelea kuwa mwaminifu kwa Bwana bila kujali shinikizo kutoka kwa wengine.

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Hesabu 11:4–6.Je, mtazamo wetu daima upo sawa na mtazamo wa Waisraeli unaoelezewa katika Hesabu 11:4–6? Ni kwa jinsi gani ushauri katika Mafundisho na Maagano 59:15–21 unasaidia?

Hesabu 12:3.Ni kwa jinsi gani Musa alionyesha kwamba alikuwa “mpole sana” katika Hesabu 12 au katika maandiko mengine uliyosoma? Unaweza kurudia maelezo ya Mzee David A. Bednar kuhusu upole katika ujumbe wake “Upole na Unyenyekevu wa Moyo” (Liahona, Mei 2018, 30–33) au katika “Upole, Unyenyekevu” katika Mwongozo wa Maandiko (scriptures.Church ofJesusChrist.org). Tunajifunza nini kuhusu namna tunavyoweza kuwa wapole zaidi? Ni baraka zipi zinaweza kuja tukifanya hivyo?

Hesabu 13–14.Wawili (au) wanafamilia zaidi wa familia yako wangejifanya “kupeleleza” (Hesabu 13:17) sehemu nyingine ya nyumba yenu kama vile ilikuwa ni nchi ya ahadi. Na wangeweza kutoa taarifa yenye msingi katika Hesabu 13:27–33 au Hesabu 14:6–9. Tunajifunza nini kuhusu imani kutoka kwenye taarifa mbili tofauti katika mistari hii? Tunawezaje kuwa zaidi kama Kalebu na Yoshua?

Hesabu 21:4–9.Baada ya kusoma Hesabu 21:4–9, sambamba na 1 Nefi 17:40–41; Alma 33:18–22; na Helamani 8:13–15, familia yako ingeweza kutengeneza nyoka kutokana na karatasi au udongo na kuandika juu yake au kwenye karatasi vitu rahisi mnavyoweza kufanya “kuangalia juu kwa Mwana wa Mungu na imani ” (Helamani 8:15).

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “Jesus, the Very Thought of Thee,” Nyimbo za Kanisa, na. 141.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wasaidie familia yako kujenga kujitegemea kiroho. “Badala ya kupashana taarifa tu, wasaidie [wanafamilia yako] kugundua kweli za injili wao wenyewe katika maandiko na maneno ya manabii” (Kufundisha katika Nija ya Mwokozi, 28).

Picha
Musa na nyoka wa shaba

Musa na Nyoka wa Shaba, na Judith A. Mehr

Chapisha