“Mei 16–22. Kumbukumbu la Torati 6–8; 15; 18; 29–30; 34: ‘Ujitunze, Usije Ukamsahau Bwana,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafisi na Familia: Agano la Kale 2022 (2021)
“Mei 16–22. Kumbukumbu la Torati 6–8; 15; 18; 29–30; 34,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2022
Mei 16–22
Kumbukumbu la Torati 6–8; 15; 18; 29–30; 34
“Ujitunze, Usije Ukamsahau Bwana”
Musa aliwaamuru wana wa Israeli kufundisha maneno ya Bwana kwa watoto wao (ona Kumbukumbu la Torati 6:7). Unapojifunza Kumbukumbu la Torati wiki hii, tafuta njia za kushiriki kile ulichojifunza na washiriki wa familia yako.
Andika Misukumo Yako
Huduma ya Musa ya duniani ilianzia mlimani, wakati Mungu alipozungumza naye kutoka kwenye kichaka kinachowaka moto (ona Kutoka 3:1–10). Pia iliishia mlimani, zaidi ya miaka 40 baadae, wakati Mungu alipompa Musa mtazamo kidogo tu wa nchi ya ahadi kutoka juu ya Mlima Nebo (ona Kumbukumbu la Torati 34:1–4). Musa alikuwa ametumia maisha yake akiwaandaa wana wa Israeli kuingia ile nchi ya ahadi, na kitabu cha Kumbukumbu la Torati kimeandika maelekezo yake ya mwisho, ukumbusho, ushauri, na kusihi kwa Waisraeli. Kusoma maneno yake huweka wazi kwamba malengo halisi ya huduma ya Musa—maandalizi watu waliyoyahitaji—hayakuwa tu kuhusu kunusurika nyikani, kushinda mataifa, au kujenga jamii. Ilikuwa ni kuhusu kujifunza kumpenda Mungu, kumtii Yeye, na kubaki waaminifu Kwake. Hayo ndiyo maandalizi wote tunayohitaji ili tuweze kuingia kwenye nchi ya ahadi ya uzima wa milele. Kwa hiyo wakati Musa hakuwahi kukanyaga kwa miguu katika “nchi ijaayo maziwa na asali” (Kutoka 3:8), kwa sababu ya imani yake na uaminifu, aliingia kwenye nchi ya ahadi ambayo Mungu ameiandaa kwa ajili ya wote wanaomfuata Yeye.
Kwa ajili ya muhtasari wa Kumbukumbu la Torati, ona “Kumbukumbu la Torati” katika Kamusi ya Biblia.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko
Kumbukumbu la Torati 6:4–7; 8:2–5, 11–17; 29:18–20; 30:6–10, 15–20
Bwana anataka mimi nimpende Yeye kwa moyo wangu wote.
Katika mafundisho yake ya mwisho, Musa aliwakumbusha wana wa Israeli, “Miaka arobaini hii alikuwa nawe Bwana, Mungu wako; hukukosa kitu,” hata ulipokuwa nyikani (Kumbukumbu la Torati 2:7). Sasa kwamba Waisraeli walikuwa wanaingia nchi ya ahadi, yenye “miji mikubwa mizuri wasiyoijenga [wao], na nyumba zimejaa vitu vyema vyote wasizojaza [wao]” (Kumbukumbu la Torati 6:10–11), Musa aliogopa kwamba wangeweza kushupaza mioyo yao na kumsahau Bwana.
Fikiria hali ya moyo wako mwenyewe unaposoma ushauri wa Musa. Unaweza kuhitaji kuzingatia juu ya mistari ifuatayo na kuandika misukumo yako:
Unaweza kufanya nini ili kulinda moyo wako usiwe mgumu na kumpenda Mungu kwa moyo wako wote? Je, ni uhusiano gani unaouona kati ya Kumbukumbu la Torati 6:5–6 na Mathayo 22:35–40? (ona pia Mambo ya Walawi 19:18).
Ona pia Dieter F. Uchtdorf, “Hamu ya Nyumbani,” Liahona, Nov. 2017, 21–24.
Kumbukumbu la Torati 6:4–13, 20–25
“Ujitunze, Usije Ukamsahau Bwana.”
Wengi wa kizazi cha Waisraeli ambacho kingeingia katika nchi ya ahadi hakikuwahi kushuhudia mapigo ya Misri au kuvuka Bahari ya Shamu. Musa alijua kwamba wao—na vizazi vijavyo—wangehitaji kukumbuka miujiza ya Mungu na amri za Mungu ikiwa watabaki kuwa watu wa Mungu.
Ni ushauri gani Musa anautoa katika Kumbukumbu la Torati 6:4–12, 20–25 ambao ungeweza kukusaidia kukumbuka mambo makubwa ambayo Mungu amekufanyia? Unapata ushawishi wa kufanya nini ili kwamba neno la Bwana daima litakuwa “ndani ya moyo wako”? (mstari wa 6).
Utawezaje kurithisha imani yako kwa vizazi vijavyo?
Ona pia Kumbukumbu la Torati 11:18–21; Gerrit W. Gong, “Daima Umkumbuke Yeye,”Liahona, Mei 2016, 108–11; Kamusi ya Biblia, “Utepe au hirizi.”
Kuwasaidia wenye mahitaji kunahusisha mikono ya ukarimu na moyo wa utashi.
Kumbukumbu la Torati 15:1–15 inatoa ushauri wa namna ya kuwasaidia maskini na wenye mahitaji, ikijumuisha matendo maalum ambayo hayafuatwi siku hizi. Lakini gundua kile mistari hii inachofundisha kuhusu kwa nini tunapaswa kuwasaidia maskini na jinsi gani mtazamo wetu kuhusu kuwasaidia ni muhimu kwa Bwana. Unahisi ni nini Bwana anakutaka wewe kujifunza kutoka kwenye mistari hii kuhusu kuwasaidia wengine?
Ona pia Russell M. Nelson, “Amri Kuu ya Pili,” Liahona, Nov. 2019, 96–100.
Yesu Kristo ni Nabii ambaye angeinuliwa kama Musa.
Petro, Nefi, Moroni, na Mwokozi mwenyewe wote walizungumza juu ya unabii katika Kumbukumbu la Torati 18:15–19 (ona Matendo ya Mitume 3:20–23; 1 Nefi 22:20–21; Joseph Smith—Historia ya 1:40; 3 Nefi 20:23). Unajifunza nini kuhusu Mwokozi kutoka kwenye mistari hii? Ni kwa jinsi gani Mwokozi “ni kama” Musa? (Kumbukumbu la Torati 18:15).
Ni nini kilimtokea Musa?
Japokuwa Kumbukumbu la Torati 34:5–8 inasema kwamba Musa alikufa, ufahamu wa siku hizi za mwisho unafafanua kwamba alihuishwa, au kubadilishwa ili asiweze kupatwa na maumivu au kifo mpaka atakapofufuliwa (ona Alma 45:18–19; Kamusi ya Biblia, “Musa”; Mwongozo wa Maandiko, “Viumbe Waliohuishwa,” scriptures.ChurchofJesusChrist.org). Ilikuwa ni lazima kwa Musa kuhuishwa kwa sababu alihitaji kuwa na mwili wa nyama ili aweze kuwapatia funguo za ukuhani Petro, Yakobo na Yohana katika Mlima wa Kugeuka Sura (ona Mathayo 17:1–13).
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani
-
Kumbukumbu la Torati 6:10–15.Mistari hii inaweza kuchochea wanafamilia wako kufikiria njia ambazo kwazo familia yako imebarikiwa. Ni kwa jinsi gani tunaweza kufuata ushauri wa “ujitunze, usije ukamsahau Bwana” ? (Kumbukumbu la Torati 6:12). Unaweza kutaka kuandika hisia zako kuhusu baraka zako, labda katika shajara yako au kwenye FamilySearch.
-
Kumbukumbu la Torati 6:13, 16; 8:3.Mistari hii ilimsaidia Mwokozi kwenye nyakati muhimu katika maisha Yake, ili kuona ni kwa jinsi gani someni pamoja Mathayo 4:1–10. Ni vifungu vipi vimetusaidia sisi wakati wa uhitaji?
-
Kumbukumbu la Torati 7:6–9Fanya jambo lolote ili kuwasaidia wanafamilia wako wajisikie maalumu, kama vile kuandaa chakula wanachokipenda. Kisha mngeweza kusoma Kumbukumbu la Torati 7:6–9 na kujadili inamaanisha nini kuwa “watu maalum” (mstari wa 6) kwa Bwana.
-
Kumbukumbu la Torati 29:12–13.Kuzungumzia kuhusu Kumbukumbu la Torati 29:12–13 kunatoa nafasi kwa wanafamilia wako kujadiliana maagano watakayofanya au ambayo wamefanya na Baba wa Mbinguni. Inamaanisha nini kuwa watu wa Mungu? Ni kwa jinsi gani maagano yetu “yanatuweka [sisi] … kuwa watu kwa [Mungu]”? (mstari wa 13).
Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.
Wimbo uliopendekezwa: “I Want to Live the Gospel,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 148.