Agano la Kale 2022
Nyenzo za Ziada


“Nyenzo za Ziada,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2022 (2021)

“Nyenzo za ziada,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2022

Picha
familia ikijifunza maandiko nyumbani

Nyenzo za Ziada

Nyingi ya nyenzo hizi zinaweza kupatikana katika app ya Maktaba ya Injili na kwenye ChurchofJesusChrist.org.

Nyimbo za Kanisa na Kitabu cha Nyimbo za Watoto

Muziki mtakatifu humwalika Roho na hufundisha injili katika njia ya kukumbukwa. Katika kuongezea kwenye kutumia toleo lililochapishwa la Nyimbo za Kanisa na Kitabu cha Nyimbo za Watoto, unaweza kupata rekodi za sauti na video za nyimbo nyingi za kanisa na nyimbo za watoto kwenye music.ChurchofJesusChrist.org na katika app za Music na Gospel Media.

Vitabu vya Kiada vya Seminari na Chuo

Vitabu vya Kiada vya Seminari na Chuo hutoa chimbuko la kihistoria na maoni ya kimafundisho kwa kanuni na matukio yanayopatikana katika maandiko.

Majarida ya Kanisa

Magazeti ya Rafiki, Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, na Liahona hutoa hadithi na shughuli ambazo zinaweza kuelezea kanuni unazofundisha kutoka katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia.

Mada za Injili

Kwenye Mada za Injili (topics.ChurchofJesusChrist.org) unaweza kupata taarifa muhimu kuhusu mada mbali mbali za injili, pamoja na viunganisho kwenye nyenzo saidizi kama vile mahubiri ya mkutano mkuu yanayoshabihiana, makala, maandiko, na video. Unaweza pia kupata Insha za Mada za Injili, ambazo hutoa maelezo ya kina ya maswala ya injili na ya kihistoria.

Hadithi za Agano la Kale

Hadithi za Agano la Kale zinaweza kuwasaidia watoto kujifunza mafundisho na hadithi zilizopatikana katika Agano la Kale. Unaweza pia kupata video za hadithi hizi katika app ya Maktaba ya Injili na kwenye MediaLibrary.ChurchofJesusChrist.org.

Kitabu cha Kupaka Rangi cha Agano la Kale

Nyenzo hii ina kurasa za shughuli zilizokusudiwa kuongeza kujifunza kwa watoto kutoka kwenye Agano la Kale.

Video na sanaa

Kazi ya sanaa, video, na vyombo vingine vya habari vinaweza kuisaidia familia yako kuelewa mafundisho na hadithi zenye uhusiano na maandiko. Tembelea Gospel Media katika MediaLibrary.ChurchofJesusChrist.org ili kupitia pitia mkusanyiko wa nyenzo za habari za Kanisa. Gospel Media pia inapatikana kama app ya simu ya mkononi. Picha nyingi ambazo unaweza kutumia zinapatikana katika Kitabu cha Sanaa ya Injili

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi inaweza kukusaida kujifunza kuhusu, na kutumia kanuni za kufundisha kama Kristo.

Chapisha