Agano la Kale 2022
Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia


“Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia,Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2022 (2021)

“Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia,Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2022

Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia

Nyenzo Hii Ni Kwa Ajili ya Nani?

Nyenzo hii ni kwa ajili ya kila mtu binafsi na familia katika Kanisa. Imetengenezwa ili kukusaidia wewe kujifunza injili—iwe peke yako au na familia yako. Kama hujajifunza injili mara kwa mara hapo awali, nyenzo hii inaweza kukusaidia kuanza. Kama tayari una mazoea mazuri ya kujifunza injili, nyenzo hii inaweza kukusaidia kuwa na uzoefu mwingi wa maana.

Je, Ni Kwa Namna Gani Ninapaswa Kuitumia Nyenzo Hii?

Tumia nyenzo hii katika njia ambayo ina manufaa kwako. Unaweza kuona ina manufaa kama mwongozo au msaada wa kujifunza maandiko kwako binafsi na kifamilia. Unaweza pia kuitumia kwa ajili ya jioni ya familia nyumbani. Mihutasari huonyesha kanuni muhimu zinazopatikana ndani ya Agano la Kale, hupendekeza mawazo ya kujifunza na shughuli kwa ajili ya watu binafsi na familia, na hutoa sehemu za kuandika mawazo yako.

Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia haikusudiwi kuwa mbadala au kushindana na mambo mazuri unayofanya. Fuata mwongozo wa Roho ili kuamua jinsi ya kuanza kujifunza kwako mwenyewe neno la Mungu.

wanandoa wakisoma maandiko

Ni Kwa Jinsi Gani Nyenzo Hii Inahusiana na Kile Kinachotokea Kanisani?

Mihutasari katika nyenzo hii imepangwa kulingana na ratiba ya kusoma kila wiki. Njoo, Unifuate nyenzo kwa ajili ya Msingi, kwa ajili ya Shule ua Jumapili, na kwa ajili ya madarasa ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni na Wasichana hufuata ratiba hiyo hiyo. Ili kusaidia juhudi zako za kujifunza na kuishi injili nyumbani, walimu wako kanisani watakupa fursa za kushiriki uzoefu wako, mawazo, na maswali kuhusu vifungu vya maandiko ambavyo umekuwa ukijifunza ukiwa nyumbani.

Kwa sababu Shule ya Jumapili inafundishwa mara mbili tu kwa mwezi, walimu wa Shule ya Jumapili wanaweza wakachagua kuunganisha au kuacha mihutasari ili kwenda sambamba na ratiba ya kila wiki. Hii yaweza pia kuwa ya muhimu (kwa zote Shule ya Jumapili na Msingi) katika wiki ambapo mikutano ya kawaida ya Kanisa haifanyiki kwa sababu ya mkutano wa kigingi au kwa sababu zinginezo. Katika muda wa wiki hizi unaalikwa kuendelea kujifunza Agano la Kale nyumbani.

Je, Ninahitaji kufuata Ratiba?

Ratiba itakusaidia kusoma chaguzi kutoka Agano la Kale na Lulu ya Thamani Kuu mwishoni mwa mwaka. Kwa kuongezea, kufuata ratiba sawa na vingine kunaweza kuongoza kwenye uzoefu wa maana nyumbani, kanisani, na kwingineko. Lakini usijisikie kufungwa na ratiba au kulazimishwa kusoma kila mstari; ratiba ni mwongozo wa kukusaidia kirahisi kujipima mwenyewe. Kitu cha muhimu ni kwamba unajifunza injili wewe binafsi na kama familia.

Kumbuka kuhusu Ratiba ya Usomaji wa Agano la Kale

Mpangilio uliopendekezwa wa ratiba ya usomaji wa Njoo, Unifuate kwa mwaka 2022 haujumuishi kila sura katika Agano la Kale. Kwa sababu Agano la Kale ni refu kuliko ujazo mwingine wa maandiko, sura na vitabu vingine vimeachwa ili kufanya ratiba ya kusoma iwezekane kwako na kwa familia yako.

Sura na vitabu vilichaguliwa ili kuepuka upungufu wa kazi na kuangazia vifungu vinavyoshuhudia juu ya Yesu Kristo, vina mafundisho mengi na vinafaa sana kwa siku zetu. Kwa mfano, ratiba ya usomaji uliopendekezwa haijumuishi 1na 2 Mambo ya Nyakati kwa sababu mengi ya yaliyomo katika vitabu hivyo yanarudia nyenzo zinazopatikana katika 1na 2 Wafalme. Ratiba hiyo pia haijumuishi Wimbo wa Sulemani, kwa sababu Nabii Joseph Smith alifundisha kuwa sio maandiko yaliyoongozwa (ona Mwongozo wa Maandiko, “Wimbo wa Sulemani,” scriptures.ChurchofJesusChrist.org). Hata hivyo, kumbuka kwamba hili ni pendekezo tu la ratiba ya kusoma. Mafunzo yako ya kibinafsi na ya familia yanapaswa kuongozwa na ufunuo wa kibinafsi.