“Jumuisha Muziki Mtakatifu katika Kujifunza Injili Kwako,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2022 (2021)
“Jumuisha Muziki Mtakatifu katika Kujifunza Injili Kwako,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2022
Jumuisha Muziki Mtakatifu katika Kujifunza Injili Kwako
Imba Nyimbo za Msingi na nyimbo za Kanisa kunaweza kukubariki wewe na familia yako kwa njia nyingi. Mawazo haya yanaweza kukusaidia kutumia muziki mtakatifu unapojitahidi kujifunza na kuishi injili.
-
Jifunze kanuni za mafundisho. Tafuta ukweli unaofundishwa katika nyimbo unazoimba au kusikiliza. Hii inaweza kupelekea majadiliano ya injili juu ya kweli hizi siku nzima. Imba au usikilize nyimbo za Msingi au nyimbo za kanisa zinazofundisha juu ya Yesu Kristo na injili yake Zingatia njia ambazo Roho Mtakatifu anashuhudia juu ya Mwokozi na mafundisho Yake.
-
Tambua nguvu ya muziki. Kuimba au kusikiliza nyimbo za Msingi na nyimbo za Kanisa kunaweza kuwa baraka wakati wa mahitaji. Kwa mfano, kuimba wimbo kunaweza kumtuliza mtoto wakati wa kulala, kuleta furaha wakati familia yako inafanya kazi pamoja, kuinua jirani ambaye ni mgonjwa, au kumfariji mtu anayehisi wasiwasi.
-
Shiriki uzoefu. Shiriki uzoefu wa kibinafsi na wa familia ambao unahusiana na ujumbe wa nyimbo. Unaweza pia kushiriki hadithi zinazohusiana za maandiko.
-
Shirikisha familia yako Familia yako itajifunza zaidi kutoka kwa nyimbo ikiwa wanashiriki kikamilifu. Ili kuwashirikisha wanafamilia, unaweza kumwalika mtoto mkubwa kusaidia kufundisha wimbo kwa wadogo au kuwaalika watoto kufundisha familia wimbo ambao walijifunza katika Msingi. Unaweza pia kuruhusu wanafamilia kuchukua zamu kuongoza wimbo.
-
Kuwa mbunifu. Tumia njia anuwai za kujifunza muziki mtakatifu kama familia. Kwa mfano, unaweza kutumia ishara zinazoendana na maneno na virai katika wimbo. Au unaweza kuchukua zamu kuigiza sehemu za wimbo wakati wanafamilia wakijaribu kubahatisha wimbo huo. Familia yako inaweza kufurahia kuimba nyimbo kwa kasi au sauti kubwa. Programu ya Maktaba ya Injili na programu ya Injili kwa watoto ina rekodi na video ambazo zinaweza kukusaidia kujifunza nyimbo. Unaweza pia kutengeneza orodha ya muziki mtakatifu wa kusikiliza.
Kwa mawazo zaidi, ona sehemu “Kutumia Muziki Kufundisha Mafundisho” na “Kuwasaidia Watoto Kujifunza na Kukumbuka Nyimbo za Msingi na Nyimbo za Dini,” hupatikana katika “Maagizo ya Wakati wa Kuimba na Uwasilishaji wa Muziki wa Sakramenti wa Watoto” katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili Ya Msingi.